Mali za Mke katika Ndoa

Mali za Mke katika Ndoa

CAMARADERIE

JF-Expert Member
Joined
Mar 3, 2011
Posts
4,419
Reaction score
1,923
Hivi tuseme umepata mpenzi wako.Ukagundua kuwa anamiliki mali kama nyumba na magari na wewe huna kitu. Mkakubaliana kuoana. Ukahamia kwake wewe na Rambo yako. Hali huwaje baadae? Tunaweza rejea wimbo wa Simba wa Nyika ''utakuja nitafuta....mashariki na magharibi''.Hiki ni kisa cha kweli cha mwanamuziki marehemu George Peter Kinyonga aliyetupiwa virago nje na mkewe baada ya kutofautiana.
 
Kwani pale mwanamke anapohamia kwa mwanamme na rambo yake inakuwaje?
 
It all depends. . .
Kama ambavyo wapo wanaume ambao hua wanawanyanyasa wake zao na mali,nyumba ndivyo ambavyo hata wanawake wapo wa aina hiyo. Na pia wapo ambao hawafanyi hivyo.

Ila sasa sababu ya huyo mtu kufukuzwa nayo lazima iangaliwe, siwezi kushabikia kwamba mwanamke/mwanaume kafanya hivyo kwasababu tu yeye ndie mwenye mali wakati mhusika anaweza akawa amefanya mambo ambayo mwenzake ameshindwa kuvumilia. Hata kama ingekua yao wote angeweza akafukuzwa vile vile.

Alafu tatizo la watu wengine wake kwa waume ni kubweteka. Yani akishapata pa kukaa kana hivyo anadhani basi hayo ndio maisha badala ya kujituma ili nae awe na kitu ambacho anaweza akajivunia amekitolea jasho.
 
hali itaendelea kuwa nzuri kama mtaendelea kuishi kwa kuheshimiana kama mlivyokutana mali sio kitu
tatizo linakuja kunapotokea mabadiliko kati ya mke/mume inawezekana unaingia ndani na rambo baada ya mazoea unaanzisha matatizo/dharau unategemea kifuate nini kama sio kuondoka kama ulivyoingia
 
Hivi tuseme umepata mpenzi wako.Ukagundua kuwa anamiliki mali kama nyumba na magari na wewe huna kitu. Mkakubaliana kuoana. Ukahamia kwake wewe na Rambo yako. Hali huwaje baadae? ...
Endapo mkiachana kila mmoja atabaki/atachukua/atapewa stahili yake! Muhimu ni kuhakikisha kwa pamoja mnadumisha ndoa yenu na pia kujipatia mali zaidi kwa pamoja ili hata kama ikitokea mnaachana basi pawepo na kitu cha kugawana.

Hata hivyo kwa tamaduni za makabila mengi ya ki bantu/kiafrika mwanamke ndiye "anayeolewa" na hivyo kuhamia kwa mwanaume/kiumeni. Hili la mwanaume kuhamia kwa mwanamke unaweza "kuchekwa" na pengine "kukosa heshima" kama mwanaume mbele ya jamii yako. Well, tamaduni hizi pengine zinapitwa na wakati sasa lakini bado zipo!
 
Kwenye mji wangu asilimia kubwa ya mali nimenunua mimi......lakini KIDAWA wangu wa KIPAWA namsikia akisema kila kitu ni chake....nyumba yangu,gari yangu,hela zangu (tuna joint bank account),watoto wangu........ila kasoro mama yangu mzazi hasemi mama yangu :lol::lol::lol:
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Inategemea makubaliano yenu imekuwaje toka mwanzo

Ila mie mmmhhh sikubali kuhamia kwa mwanamke hata iweje
wanawake wana visa sana hawa pale mnapokosana
atakwambia unapanga sheria hapa ni kwako, na maneno
mengii yakukuudhi bora nijikaze kiume nitafute vyangu
 
Inabidi kila wakati uwe ''Yes Ma'am'' kind of man
 
Hivi tuseme umepata mpenzi wako.Ukagundua kuwa anamiliki mali kama nyumba na magari na wewe huna kitu. Mkakubaliana kuoana. Ukahamia kwake wewe na Rambo yako. Hali huwaje baadae? Tunaweza rejea wimbo wa Simba wa Nyika ''utakuja nitafuta....mashariki na magharibi''.Hiki ni kisa cha kweli cha mwanamuziki marehemu George Peter Kinyonga aliyetupiwa virago nje na mkewe baada ya kutofautiana.
Unajuwa wanawake ni wavumulivu sana kwenye hili neno...... UMEKUJA NA RAMBO YAKO HAPA HALAFU UNANILETEA USExxxx.... Kuliko ilivyo kwa wanaume. Katika hali halisi one day mama litamtoka tu hilo........... by the way unadhani kwa nini ndoa za wananwake wenye nazo huwa zina misukosuko sana?? USIONE WABABA WANATOKA NA ma-VX... kinachowakuta ndani ya nyumba ni siri yao. Na ndiyo maana wanawake maarufu/wenye fweza kulinda ndoa zao ni ishu sana....... wachache sana wenye uwezo huo............. NA OLE WAKO UFANYE KITU KITAKACHOHARIBU UMAARUFU WAKE.............. UtajiJEIJEI.....
 
Ninamjua jamaa mmoja macheni kibao shingoni na mapete vidoleni........saa mbili kamili ndani ya geti......yaani mkikaa naye kikao ikifika saa mbili kasoro machozi yanamtoka........na anakuja na V8
 
hamna tofauti na pale mwanamke anapohamia kwako
Ndugu asikudanganye mtu......... tofauti ipo kijamii...... na mbaya zaidi jamii inakubali mwanamke kuhamia kwa mwanaume kuliko mwanaume kuhamia kwa mwanamke........... UTAWASIKIA.......... UNAMZUNGUMZIA NANI....? .... Badili Tabia.......? Kaolewa yule na Lizzy..........
 
Ndugu asikudanganye mtu......... tofauti ipo kijamii...... na mbaya zaidi jamii inakubali mwanamke kuhamia kwa mwanamke kuliko mwanaume kuhamia kwa mwanamke........... UTAWASIKIA.......... UNAMZUNGUMZIA NANI....? .... Badili Tabia.......? Kaolewa yule na Lizzy..........

Huyu Lizzy nimeona mpaka mmemfungulia thread yake.......bolingo complique eeh?
 
Back
Top Bottom