Naomba kueleweshwa hapa. Kisheria, mali ambayo mwanandoa amekukuta nayo say kiwanja/ shamba inahesabika au haihesabiki kama sehemu ya mali ya wanandoa? Kuna ahadi fulani husemwa kanisani (baadhi ya dini za kikristo) kuwa " nakushirikisha kwa mwili wangu na Mali zangu za duniani" hii huwa ni Mali zipi kama sio ulizonazo kabla ya ya ahadi?. Je, hii ahadi ina mashiko yoyote kisheria?