Maliasili mambo safi - Kigwangala kubeba gharama za honeymoon ya Ali Kiba huko Venice - Italy

Tang Zhou

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2018
Posts
1,206
Reaction score
2,588
Wakati Rais Magufuli hushangaa Majaji kuwa na fedha za kutosha kumudu kwenda likizo nje ya nchi, Waziri wake Mh.Hamis Kigwangallah ametoa ahadi ya kulipia honeymoon ya wanandoa Ali Kiba na mkewe katika mji wa maraha wa Venice Italy, kwa kipindi cha wiki 2 katika mazingira ya kitalii yoyote yale yatakayopendekezwa na wanandoa hao. Watu wana hela zao bana Rais aache wivu!

Habari zaidi soma hapa:

Minister offers to foot Alikiba's honeymoon in Venice - PHOTOS - Nairobi News
 
[emoji28] [emoji28] ngoja akina nanii wajee utaona chunguu hii post yako
 
kwani hujui kama alikiba na mkewe ni kivutio cha watalii hapa nchini?

Akitoka huko kwa papa atawekwa kwenye mbuga za wanyama watalii waongezeke.

Hizi ndio sera zetu

hapa kazi tu.
 
Kama sikosei king kiba ni balozi wa utalii hapa tz na basis kama ni hivyo anastahili.
 
Lakini Kigwa alisema wahague moja ya hifadhi hapa nchini..kwahiyo habari ya Italy ni kama imetengenezwa, hata kama watakwenda Italy nadhan si kwa gharama za Kigwa!!
 
Kwanini isiwe Ruaha ama kalambo falls??
 
kuna ubaya gani balozi wa wanyama kupewa kakipande kadogo ka shukrani.

alafu mambo ya kuweka sijui majaji hawana mkwanja siju nini ni upuuzi tu.
 
Atakuwa kashikishwa ule mgao wa 1.5 trillion huyu walizokwapua hazina.

 
Kuna mambo ya ajabu sana nchi hii!
Watakuambia wanakwenda kutangaza nchini huko Kuhusu utalii

Ova
 
Pesa za kutalii honeymoon ughaibuni zipo ila sitahiki za Tundu Lissu hakuna hadi leo,sijui hizi zimeizinishwa kwa utaratibu gani ambao ni rahisi kuliko kwa Lissu!!

Halafu utamuona bwana Jiwe akijigamba yeye mpenda haki na habagui, no wonder leo kwenye majabari ya Iringa imesikika sauti ikikana kuahidi masurufu maradufu kwani jiwe letu linachohubiri sicho linachotenda na jepesi kusahau wakati formula ya kudanganya inataka uwe na kumbukumbu!! !
 
Kiba ni balozi wa Tembo na tembo ni mnyama mwenye ufadhili mkubwa kkwa sbb ya janga lao la kuuliwa hovyo so inawezekana kabisa kupitia hyo akapata udhamini. Acheni unaaa
 
Kigwa kawapa ofa ya kutembelea hifadhi moja nchini hizo porojo za italy kudhaminiwa na kigwa ni endelezo la utimu tu kurushana roho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…