Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
Baada ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole, kuendelea kutoa kauli kuhusu mwelekeo wa kisiasa nchini, Mwanachama wa CCM na aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Asasi za Kiraia mkoani Morogoro, Maliki Marupu, amemjibu vikali Polepole na kumtuhumu kwa upotoshaji.
Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mbeya, Marupu amesema Polepole alitoa madai ya uongo kuhusu wizi wa kura kwenye uchaguzi mkuu wa 2020, akidai kuwa mfumo uliotumika kuiba kura ulitegemea kuunganishwa kwa database ya CCM, Tume ya Uchaguzi na NIDA — jambo ambalo Marupu amelitaja kuwa halina ukweli wowote.
Marupu amesema kuwa mwaka 2020 CCM ilitumia kadi za kawaida za chama kwa ajili ya kura za maoni, na kwamba mfumo wa kadi za kidigitali haukuwa umeanza kutumika. Amesisitiza kuwa database za chama zilikuwa katika matawi, zikihifadhi makati ya wanachama tu.
Kauli hii ya Marupu imeibua mjadala kuhusu ukweli wa madai ya Polepole, ambaye hivi karibuni ameonekana kueleza kwa kina maoni yake kuhusu siasa za ndani ya chama chake na nchi kwa ujumla.