Malinzi afanya fitna, Ndimbo afukuzwa kazi Times fm

Jeff Gemo

Member
Joined
Jul 11, 2015
Posts
34
Reaction score
26
Salam wana JF.

Kuna taarifa inasema Mtangazaji nguli wa michezo hapa nchini na aliyepata kuwa msemaji wa Club ya Simba Clifford Mario Ndimbo amefukuzwa Radio Times Fm ambapo ndio alikuwa akiendesha kipindi chake cha michezo kiitwacho "Wizara ya Michezo"

Taarifa za ndani zinasema kuwa Mkurugenzi wa radio hiyo amefikia hatua hiyo kwa kile kinachosemekana kuwa ni kulinda maslahi ya viongozi wa michezo hasa mpira wa miguu waliokuwa wakianikwa hadharani "uozo" wao kupitia segment ya "Dokodoko" ambayo ilijikita katika kueleza ukweli wa masuala mbalimbali ya mpira wa Tanzania.

Wafuatiliaji wa kipindi cha Wizara ya michezo wanasema wana muda mrefu sana hawajasikia segment ya "Dokodoko" ambayo ndio iliibua skendo kubwa ya Rushwa TFF na mambo mengine, na kupelekea kesi kwenda mahakamani na TFF wakashinda.

Washabiki wa kipindi hicho wanasema kwa siku tatu sasa hawajamsikia Ndimbo hewani na kipindi kinaendeshwa na Mtangazaji mwingine huku kikiwa na sura tofauti na kupoteza mvuto.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ndimbo aliandika "Dokodoko Next Destination loading......" akiwa na maana kipindi chake sasa kinahama na kwenda radio nyingine, hili linathibitisha uvumi huu ulioanza kusambaa tangu wiki iliyopita.

Watu wanaamini mkurugenzi wa Times Fm ametumiwa na baadhi ya viongozi wa mpira ili alinde maslahi yao bila kujua anaharibu Radio yake mwenyewe na kuvunja heshima iliyojijengea.

Safari ya mpira wadau ni ndefu sana sitashangaa nikisikia vipindi vya michezo vinatangaza matokeo tu, maana mpaka wakurugenzi sasa wanatumika kwa njama za hawa majamaa... Hiyo Times radio mimi ndio sisikilizi tena maana boss mwenyewe hajielewi, badala ashangilie na kuwapa sapoti watu wake, yeye ndio anawafukuza.

Hili suala kama Malinzi kaweka mkono wake itafahamika tu, lakini lazima ajue watu wa mpira tumemchoka, aondoke zake na rushwa zake !! Alitumia media wakati anaingia, naona sasa tena kamuweka Kwapani Mkurugenzi wa Times Fm ili atumie Radio yake kuingia kwa kudhoofisha makali ya kipindi cha michezo.

Wanamichezo na wapenda mabadikiko bado tutamkumbuka mzee wa "Dokodoko" Clifford Mario Ndimbo na team yake, na popote mnapokwenda ninaamini mtaendelea kusimamia haki na kusaidia kuokoa michezo nchini. Tanzania nzima inajua kazi yenu, watanzania wanajua bila nyinyi ile skendo ya upangaji matokeo ingekuwa ni siri, mmeonesha mwanga kwa watangazaji wengine wa vipindi vya michezo na watajifunza kupitia nyinyi.

Watu wa mpira sasa tuna haja gani ya kusikiliza michezo ya radio kama Times? Michezo itakayokuwa inachujwa ili kumfurahisha Malinzi na watu wake.. Yaani baada ya kushinda kesi tu ndio yanatokea haya ?? Dokodoko haipo tena, na Ndimbo hayupo tena !! Mwisho wenu unakaribia.
 
Ni muda huyu jamaa sikumsikia kwenye kipindi chao. Sema kila Siku ilikuwa ni kuisema vibaya simba. Pole yake na kila la heri kwake.
 
Mimi nimeshangaa kuona hilo jina la Crifford Mario Ndimbo kumbe yupo bado!!! Miaka imepita sana tangu nimsikilize mara ya mwisho tena sikumbuki nilimsikia kituo gani cha radio!!!
 
Masikini pole yake, lakini Ndimbo hawezi kukosa kazi, na vipi demu wake Mariam si yupo TIMES nae au walishaachana? Daah alinichukulia demu wangu huyu mshikaji lakini siyo mbaya maisha yanasonga, Haya Mama Cole bado nakukumbuka.
 
Akiwa Magic Fm eh? Au kipindi kile uko TBC,
 
Radio gani nayo hiyo ina miaka karibu 7 frequency 1 tu wenzao e fm juz tu leo wamepewa mikoa9
 
Mimi nimeshangaa kuona hilo jina la Crifford Mario Ndimbo kumbe yupo bado!!! Miaka imepita sana tangu nimsikilize mara ya mwisho tena sikumbuki nilimsikia kituo gani cha radio!!!
Magic Fm mkuu
 
Sema Times nao hawasikiki sana, wamejificha
 
Masikini pole yake, lakini Ndimbo hawezi kukosa kazi, na vipi demu wake Mariam si yupo TIMES nae au walishaachana? Daah alinichukulia demu wangu huyu mshikaji lakini siyo mbaya maisha yanasonga, Haya Mama Cole bado nakukumbuka.
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Radio gani nayo hiyo ina miaka karibu 7 frequency 1 tu wenzao e fm juz tu leo wamepewa mikoa9
Mkuu siyo saba tu, ina kama miaka kumi na tano lakini kifrequency kimoja tu huwa hawajielewi hawa.
 
Mahakama ndo imetoa uamuzi wa mwisho na imeonekana walidanganya umma, kawajibika kwa makosa yake hata sio kufukuzwa huku.
 
Salam wana JF.

Kuna taarifa inasema Mtangazaji nguli wa michezo hapa nchini na aliyepata kuwa msemaji wa Club ya Simba Clifford Mario Ndimbo amefukuzwa Radio Times Fm ambapo ndio alikuwa akiendesha kipindi chake cha michezo kiitwacho "Wizara ya Michezo"

Taarifa za ndani zinasema kuwa Mkurugenzi wa radio hiyo amefikia hatua hiyo kwa kile kinachosemekana kuwa ni kulinda maslahi ya viongozi wa michezo hasa mpira wa miguu waliokuwa wakianikwa hadharani "uozo" wao kupitia segment ya "Dokodoko" ambayo ilijikita katika kueleza ukweli wa masuala mbalimbali ya mpira wa Tanzania.

Wafuatiliaji wa kipindi cha Wizara ya michezo wanasema wana muda mrefu sana hawajasikia segment ya "Dokodoko" ambayo ndio iliibua skendo kubwa ya Rushwa TFF na mambo mengine, na kupelekea kesi kwenda mahakamani na TFF wakashinda.

Washabiki wa kipindi hicho wanasema kwa siku tatu sasa hawajamsikia Ndimbo hewani na kipindi kinaendeshwa na Mtangazaji mwingine huku kikiwa na sura tofauti na kupoteza mvuto.

Katika ukurasa wake wa Instagram, Ndimbo aliandika "Dokodoko Next Destination loading......" akiwa na maana kipindi chake sasa kinahama na kwenda radio nyingine, hili linathibitisha uvumi huu ulioanza kusambaa tangu wiki iliyopita.

Watu wanaamini mkurugenzi wa Times Fm ametumiwa na baadhi ya viongozi wa mpira ili alinde maslahi yao bila kujua anaharibu Radio yake mwenyewe na kuvunja heshima iliyojijengea.

Safari ya mpira wadau ni ndefu sana sitashangaa nikisikia vipindi vya michezo vinatangaza matokeo tu, maana mpaka wakurugenzi sasa wanatumika kwa njama za hawa majamaa... Hiyo Times radio mimi ndio sisikilizi tena maana boss mwenyewe hajielewi, badala ashangilie na kuwapa sapoti watu wake, yeye ndio anawafukuza.

Hili suala kama Malinzi kaweka mkono wake itafahamika tu, lakini lazima ajue watu wa mpira tumemchoka, aondoke zake na rushwa zake !! Alitumia media wakati anaingia, naona sasa tena kamuweka Kwapani Mkurugenzi wa Times Fm ili atumie Radio yake kuingia kwa kudhoofisha makali ya kipindi cha michezo.

Wanamichezo na wapenda mabadikiko bado tutamkumbuka mzee wa "Dokodoko" Clifford Mario Ndimbo na team yake, na popote mnapokwenda ninaamini mtaendelea kusimamia haki na kusaidia kuokoa michezo nchini. Tanzania nzima inajua kazi yenu, watanzania wanajua bila nyinyi ile skendo ya upangaji matokeo ingekuwa ni siri, mmeonesha mwanga kwa watangazaji wengine wa vipindi vya michezo na watajifunza kupitia nyinyi.

Watu wa mpira sasa tuna haja gani ya kusikiliza michezo ya radio kama Times? Michezo itakayokuwa inachujwa ili kumfurahisha Malinzi na watu wake.. Yaani baada ya kushinda kesi tu ndio yanatokea haya ?? Dokodoko haipo tena, na Ndimbo hayupo tena !! Mwisho wenu unakaribia.

Sitaki kuamini hizi propaganda zako ILA ninachojua ni kwamba Ndimbo Mkataba wake kufanya hapo umefikia Kikomo na kuna Kampuni moja ya Tajiri mkubwa hapa Tanzania imeanzisha pia Radio yake na kuna uwezekano huyo Clifford Mario Ndimbo wako kapata Ofa huko. Ninachoweza kukusaidia tu Mkuu ni kwamba hakuna Kampuni iliyombeba na kumsaidia kwa hali na mali huyo Mtangazaji wako alipokuwa ameugua hadi wengi Wetu tukakata tamaa nae kwamba angekufa tu kwa matatizo aliyokuwa nayo kama Times fm na kama uko hapo na huyo Ndimbo muulize atakuthibitishia hili ninalolisema hapa.

Hata hivyo tokea arudi Kazini na aanze kutangaza tena Clifford Mario Ndimbo bado hajawa vizuri kivile kitu ambacho pengine kimechangia labda yeye kuona hana tena mvuto wala nafasi hapo hivyo kaamua kubadili upepo wa Kiutangazaji au wa Kiutendaji kwani siyo lazima awe Mtangazaji na badala yake anaweza akafanya Kazi zingine za Kianahabari na maisha yakaenda vile vile hapa mjini Lakini yawezekana pia ni mkakati wa kupunguza Wafanyakazi labda wasio na tija Kazini uliosukumwa pia na hili Wimbi baya la Kiuchumi kwa sasa linaloikumba nchi yetu hivyo Times fm labda wameamua kubaki na Watu wachache na wenye tija, mvuto na ubunifu hasa kwa zama hizi za sasa.

Kuhusu kuwa na Kipindi cha kumsema Malinzi au TFF nadhani wanaofanya hivyo siyo Times fm tu peke yao na kama ingekuwa basi huo mpango uliousema upo kweli nadhani leo hii nusu ya Watangazaji wa Efm akiwemo Bodyguard binafsi Maulid Baraka Kitenge wangeshafukuzwa kwani kwangu Mimi Efm ndiyo radio pekee inayoyaibua mabaya mengi ya TFF na wameonyesha wazi wazi kutomkubali Rais wa TFF Jamal Malinzi hadi kuwa wa kwanza kuliibua lile sakata Kubwa na la aibu la Upangaji wa matokeo ambalo hadi leo linatiririka tu Mahakamani japo wale wahusika walishinda Kesi ambayo imekatiwa tena rufaa.
 
Ile kesi ya kina Matandika imekatiwa rufaa??
 
Back
Top Bottom