Malinzi atupwa nje uchaguzi mkuu TFF!

Malinzi atupwa nje uchaguzi mkuu TFF!

Wonderful

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2015
Posts
7,347
Reaction score
5,986
Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais.

Malinzi hataweza kwa kuwa kesi iliyomfikisha mahakamani leo itasikilizwa tena Jumatatu Julai 3 na Malinzi atakaa rumande hadi siku hiyo.


Usaili wa viongozi wanaogombea uongozi TFF unafanyika kuanzia leo hadi keshokutwa wakati huo Malinzi atakuwa mahabusu.

Malinzi amefikishwa leo mahakamani akiwa na katibu wake, Mwesigwa Celestine.

Baadhi ya mashitaka hayo ni kughushi waraka wa kamati ya utendaji ulioonyesha kuwa imeridhia kubadilishwa kwa Signatories (watu wanaosaini nyaraka za benki kutoa fedha). Shitaka hilo linawahusu Malinzi na Mwesigwa.

Malinzi amedaiwa kugushi risiti za kwamba anaidai TFF na ziko risiti 20 ambazo anatuhumiwa kuzifoji.

Shitaka jingine ni utakatishaji na hii wote watatu, Malinzi, Mwesigwa na Nsian wanatuhumiwa kutakatisha kiasi cha dola 375418.
----------------------------------------------------

UPDATES:Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais kwa kuwa amepelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea baada ya kukosa dhamana hadi Jumatatu Julai 3 kesi yake itakaposikilizwa tena.

Malinzi pamoja na Katibu wake, Mwesigwa Celestine wanashitakiwa kwa makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha.

Wote wawiliw amepandishwa gari kwenda Segerea hadi Jumatatu kesi yao itakaposikilizwa tena.

Pamoja na wao, Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange 'Kaburu' wanaoshitakiwa kwa makosa ya utakatishaji, nao wamechukuliwa kupelekwa Segerea.

Kaburu na Aveva watakuwa mahabusu hadi Julai 13 baada ya kukosa dhamana kutokana na kesi inayowakabiri.
C__Data_Users_DefApps_AppData_INTERNETEXPLORER_Temp_Saved Images_IMG-20170629-WA0074.jpg
 
Vipi hawajafukua na la michango ya Serengeti Boys ilivyopigwa kwa kigezo cha kuwaweka kambi maeneo mbalimbali kwa ajili ya matayarisho ya mashindano nadhani hawatakiwi kuliacha na hili
 
Afrika kweli ni bara la giza, simtetei hata mmojawapo hapo, ila hayo makosa hayakuonekana wakati mwingine wowote isipokuwa sasa kwenye mchakato wa uchaguzi! Na ndo kusema wala hayadhaminiki kwamba hawawezi kuwa nje kwa dhamana! Kwamba wamekosa wadhamini au kujidhamini wenyewe!! Kweli 'dirty politics belongs in Africa!
 
Afrika kweli ni bara la giza, simtetei hata mmojawapo hapo, ila hayo makosa hayakuonekana wakati mwingine wowote isipokuwa sasa kwenye mchakato wa uchaguzi! Na ndo kusema wala hayadhaminiki kwamba hawawezi kuwa nje kwa dhamana! Kwamba wamekosa wadhamini au kujidhamini wenyewe!! Kweli 'dirty politics belongs in Africa!
Mkuu kwann wampenda kuchokonoa watu lkn, usione u huru kiasi hicho,
 
Back
Top Bottom