Malinzi:Wachezaji Taifa Stars ndio wabovu

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
5,370
Reaction score
3,962
Rais wa TFF Jamal Malinzi amesema kua tatizo la soka la Tanzania sio makocha wala nini bali ni wachezaji wenyewe hawafundishiki.Akikazia point hiyo aliwauliza waandishi wa habari kua kuna anaejua kwamba kuna wachezaji wa stars walitapika wakati wanampana na Egypt??
Anasema kua kama wachezaji wanapewa kambi nzuri,wanasafiri vizuri,wanakataa hotel za five star sasa wanashindwa kutoa matokeo mazuri kwa nini??

Source: Star TV Habari.
 
Jukumu la kutafuta wachezaji wa stars ni la nani? sio TFF?

Tanzania nzima hao ndio watu wanaoweza kucheza mpira peke yao? Ni jukumu la nani kutengeneza timu nzuri ya taifa

Huyu malinzi ni mpuuzi...yeye ndiye tatizo
 
kutapika kunahusiana vipi na kutofundishika?

BTW hivi kumbe tuhuma kuwa jamaa karundika wahaya TFF zina ukweli fulani hivi, manake nilikuwa naangalia hapa michezo azam tv naona anatambulisha wahaya tupu
 
Mbona Evra alitapika mechi na spurs? Na bado akacheza
 
Mbona Evra alitapika mechi na spurs? Na bado akacheza

nini Evra, Messi mwenyewe kuna mwaka alikuwa anatapika kama hana akili sawasawa lakini akaishia kupata Ballon d'or...

Malinzi anazidi kujishushia hadhi sana kwa kauli za kitoto kama hizi.
 
Nani anabisha kwamba enzi za Marcio Maximo wachezaji walikuwa wakicheza Mpira unaoeleweka? Nani anabisha kwamba baadhi ya wachezaji haohao anaosema hawafundishiki huwa wanacheza mpira wa kufundishwa wanapokuwa na klabu zao? Misri hiyohiyo iliyotufunga kirahisi kwa timu yake ya Taifa ilipata upinzani wa kweli wakati klabu yake ilipokutana na wachezaji haohao wakiwa Yanga. Kopunovic, Stewart (mara mbili za awali) na Pluijm wote wamefundisha timu zilizothibitika kicheza mpira wa kufundishwa. Lakini kama kweli wachezaji wa Tanzania hawafundishiki, huyu Mbwana Makata alifundisha wachezaji wa wapi hadi TFF ikamtambua kuwa ni kocha bora wa mwaka?
 
Hili jamaa ni kiazi kweli,yaani 100% ya wachezaji umechagua mwenyewe kwa case ya 10% leo hii unatuambia wachezaji hawafundishiki ptuuuuu!!!unatia hasira sana malinzi ni vile siwezi kutana na wewe,ligi kuu tumeiona wote leo hii unampeleka mtu kama john boko timu ya taifa?kipa no 2 kwenye club ndio no1 taifa ajabu kweli hii,umeshafanikiwa kilichokupeleka tff ondoka sasa bila shuruti.
 
Hii ni dharau kubwa saana kwa WATANZANIA, hivi Yanga wachezaji wake wanatoka wapi????? Kuna umuhimu kama kweli wachezaji wetu wamemsikia, basi WASUSIE kuchezea TIMU YA TAIFA, mpaka huyu mpuuzi ameng'oka. Wandishi, hawa vijana wanahitaji msaada, huwezi kutumia lugha yua namna hii
 

Mimi pia nakuunga mkono mkuu. Nitawashangaa sana wachezaji watakaoitwa national team halafu wakubali. Huyu malinzi kachanganyikiwa kweli. Kama kweli hayo ameyatamka, kwa nini basi anaendelea kung'ang'ania kuongoza taasisi ambayo anaamini haitaleta matokeo mazuri?
 
Last edited by a moderator:

Mimi pia nakuunga mkono mkuu. Nitawashangaa sana wachezaji watakaoitwa national team halafu wakubali. Huyu malinzi kachanganyikiwa kweli. Kama kweli hayo ameyatamka, kwa nini basi anaendelea kung'ang'ania kuongoza taasisi ambayo anaamini haitaleta matokeo mazuri?
 
Last edited by a moderator:
Hili jamaa jinga.Nina hasira nae.yaani kutapika inahusiana vipi na uwezo wa kucheza? Messi ndiye mchezaji bora duniani na katapika mara kibao.Jinga halafu linaongea kwa sifa. Wachezaji gomeni kuchezea timu ya taifa
 
Huyu mhaya kakosa cha kutuambia kistaarabu mok aseme hayo kwl hii mijitu ina dharau wakipwakipewa uraisi wa nchi itakuwaje aisee
 
Jamal Malinzi wewe ndio mbovu,unaitia aibu tanzania.toka hapo tff wanaojua mpira waje kusongesha gurudumu nchi yetu ifike mbali.kwanza hata shepu ya mpira huna unang'ang'ania nini hapo ndorobo wewe usie na nia nzuri na taifa letu.unatia sana hasira ni heri wengine hatuna hizi bunduki, yaani inafikia hatua hutaki watu wajue kama wewe mtanzania kwa jinsi tunavyoboronga kila idara.sasa hatukutaki wahaya na mpira wapi na wapi
 
Last edited by a moderator:
Chama cha wachezaji Tanzania....Hamasisheni wachezaji wagomee kwenda timu ya taifa hadi huyu mbuzi aondoke
 
Narudisha kumbukumbu wakuu. Hivi si ndio sisi tulikuwa tunalalamika alipokatwa jina na uongozi wa Tenga? mbona watanzania tunakuwa wepesi kusahau? Ni kipi kilichotupelekea kumpigia debe kiasi hicho, au tulikuwa na mihemko kama huu wa watia nia! Binafsi natia mashaka sana tunapokuwa vinyonga lazima ifike muda tutambue tunapompigia debe mtu tujue ana kipi cha maana, mfano huyu Malinzi hakuwa na lolote la maana zaidi ya promo tu redioni.
 
Mimi ni mhaya,naomba malinzi asihukumiwe kwa uhaya wake bali kwa ywezo wake,mtu unavyokuja hapa na kutushambulia wahaya kwa kosa la mtu mmoja unakuwa haututendei haki.!
 
Jukumu la kutafuta wachezaji wa stars ni la nani? sio TFF?

Tanzania nzima hao ndio watu wanaoweza kucheza mpira peke yao? Ni jukumu la nani kutengeneza timu nzuri ya taifa

Huyu malinzi ni mpuuzi...yeye ndiye tatizo
For the sake of argument, naomba aje mtu abishe kuwa hakuyatamka hayo maneno!:doh: Ajipangage basi jamani kabla ya kwenda kuongea na vyombo vya habari!
 

watanzania tunaendeshwa na mihemko

Ingawa hata kuhimiza yeye asikatwe ni sahihi endapo taratibu zilikiukwa

Tatizo hapa ni kwamba anazidi kutupoteza...Awajibike....Mbona ataonekana mstaarabu tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…