Malinzi:Wachezaji Taifa Stars ndio wabovu

Malinzi:Wachezaji Taifa Stars ndio wabovu

Hayo kayajua leo?
Kwa nini aligombea urais wa TFF asiendelee na ngumi ambako pia alichemsha?
Baada ya TFF, sijui ataibukia wapi? Labda kwenye kuogelea!
 
Kibaya zaidi hana mission wala vision, binafsi nimemshusha thamani kwa kuwa mtangulizi wake aliweka misingi yeye kaja na ubabaishaji mwingi. Mara Maboresho, mara kubadili jezi mara kufukuza timu iliyofanya kazi na Tenga. Amejaa fitna tu. Kazi ikifanyika matunda huonekana hadharani sio kama hivi kila siku tunarudi nyuma kwa kasi ya roketi!!!!
 
Malinzi alishasema amewekeza mpira kuanzia mwaka 2019 ndio tutaanza kupata matokeo mazur kushirik afcon kwa mara ya pili, mashndano ya olympics, na hatimaye kushiriki kombe la dunia 2026. Hayo ndio maono yake ila kwa sasa tuendelee kufungwa fungwa mwisho itakuwa 2019.
 
Mimi ni mhaya,naomba malinzi asihukumiwe kwa uhaya wake bali kwa ywezo wake,mtu unavyokuja hapa na kutushambulia wahaya kwa kosa la mtu mmoja unakuwa haututendei haki.!
Wala haitendei haki Taifa Stars, haitendei haki Tanzania, hatutendei haki Watanzania.
 
Back
Top Bottom