Kabende Msakila
JF-Expert Member
- Oct 7, 2020
- 1,809
- 1,692
Wakuu, Kwema?
Huwa tunajadili mengi sana yenye tija kwa chama, Serikali na Jamii. Hii ni akili na matendo ya kiungwana sana.
Sasa leo naomba tukubaliane jambo dogo tu linalohusu wenyeviti, na wenezi wa wilaya na Mkoa
Ni huzuni kuona viongozi hawa kwa namna wanavyokiwezesha chama kubaki madarakani wakiwa hawana malipo sawa na makatibu wa Chama na Jumuiya. Kama sikosei Mwenyekiti wa Wilaya hulipwa tshs 50,000 kwa mwezi huku mwenezi akilipwa tshs 20,000/= kwangu mimi naona hii si nzuri kbs na uongozi wa CCM unapaswa kuangalia upya juu ya hili ili kazi zinazofanywa na viongozi hawa ziweze kuthaminiwa.
Ushauri wa jinsi ya kuwalipa wenyeviti na wenezi
(a). Fedha zao zikasimiwe kwenye mafungu ya self-help scheme au political vote za makatibu Tawala Wilaya;
(b). Fedha za maendeleo ya Jimbo - ambapo ndani ya fungu hili yatatolewa maagizo mahsusi toka Wizara ya Fedha kama ilivyofanyika kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa;
(c). Ruzuku ya Chama - kwamba kila zinapolipwe fedha kwa makatibu basi na wenyeviti na wenezi walipwe sawia.
Nimeshauri hivi kutokana na ukubwa wa kazi wanazofanya kila siku kwa miaka mitano ya kazi.
Nawasilisha.
Msakila M. Kabende
Kakonko - Kigoma
Tanzania.