Malipo ya fidia yawatoa machozi wananchi Dar

Malipo ya fidia yawatoa machozi wananchi Dar

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
KWA UFUPI

  • Waiomba Serikali kuingilia kati ili waweze kupata malipo stahiki kulingana na ugumu wa maisha uliopo.



Dar es Saalam. Wananchi wa Mji Mpya Majohe, Guluka Kwalala na Ulongoni katika Manispaa ya Ilala wameiomba Serikali kuingilia kati na kumwamuru mwekezaji wa ujenzi wa njia ya umeme wa kilovoti 220 kutoka Somanga Mtama mpaka Kinyerezi, Kilwa Enegy kuwalipa gharama zinazoendana na hali ya maisha ya sasa.

Ombi hilo walilitoa jana walipokuwa wakijadili kuhusu dodoso la uhakiki wa mali zao na malipo, walilopewa lilivyokuwa na upungufu, mapunjo ya mali zao hasa thamani za nyumba kuwa kidogo tofauti na gharama za ujenzi na ununuzi wa kiwanja walizotumia.

Utathmini wa mali na nyumba za wananchi unadaiwa kufanywa na kampuni binafsi iliyofahamika kwa jina la Joransa, ambapo tathmini katika maeneo hayo ilifanyika mwaka 2011 na kutolewa ahadi kuwa malipo ya fidia yangeanza kulipwa baada ya miezi mitatu .

.Baruani Kanoze akilalamikia kulipwa fedha kidogo tofauti na thamani ya mali zake, alisema mwekezaji huyo awali aliwahi kusema kuwa atawalipa kwa kiwango kinachoendana na gharama za maisha zilivyo kwa wakati husika jambo ambalo limewashangaza sana. hasa kulingana na kiwango cha malipo kilichotolewa.

‘Ni jambo ambalo haliingii akilini baada ya kuangalia karatasi za tathmini na kukuta gharama zilivyowekwa za viwanja na kupangisha nyumba, kiwanja umewekewa Sh1 milioni na gharama ya kupanga nyumba eti Sh20,000 kwa mwezi, sijui unakwenda kupanga wapi nyumba’ alisema mkazi wa Guluka Kwalala ambaye hakutaka kutajwa gazetini.

Alisema yeye anamiliki nyumba ya vyumba vitano, yenye umeme, choo bora pamoja na kisima cha maji alivyovijenga kwa zaidi ya Sh40 milioni, kwenye dodoso la uhakiki wa mali anaambiwa thamani ya nyumba yake ni Sh6 milioni.

Aidha, walishauri kuliko Serikali kujiingiza katika maafa kwa kukubali mradi huo utekelezwe wakati wananchi hawajaridhika na fidia ao, ni vyema ikafanyika tathmini nyingine ambayo itakuwa ya haki .

Hata hivyo, uongozi wa Kilwa Energy ulipotafutwa kufafanua malipo hayo ya wananchi, simu zao hazikuweza kupatikana.

chanzo. Malipo ya fidia yawatoa machozi wananchi Dar - Kitaifa - mwananchi.co.tz
 
Kuna mambo hua yanauma sana! Watanzania ni moja Kati ya raia wasio na thamani zaidi ya siku ya kupiga kura! Kweli nyumba ya milioni 40 ukaithaminishe kwa M6?! Hii ccm hii endeleeni kuipenda tu kwakweli!!
 
Hii ni Serikali dhalimu kila siku iendayo kwa Mungu wanafanya udhalimu wa kutisha dhidi ya Watanzania katika sehemu mbali mbali nchini. Mtu kahangaika huku na kule kajenga nyumba yake kwa zaidi ya milioni 40 halafu fidia yake wanampa milioni 6 tu!!!!
 
Mimi nadhani katika jukwaa hili tunatakiwa kuwashauri waathirika kama wataalamu na siyo kuungana kulalamika maana haitasaidia kitu. Iko hivi valuation kwa ajili ya fidia inakua aproved na mthamini mkuu wa serikali ndipo iwe halali. So utaratibu ni kuamwathirika anatakiwa ku appeal kwa mthamini mkuu ndani ya siku 60 toka alipo kabidhiwa cheki au mchanganuo wake baada ya hapo anaenda high court land division
 
Back
Top Bottom