Malipo ya kukodisha Trekta kwa heka yakoje?

Malipo ya kukodisha Trekta kwa heka yakoje?

Brigit86

Member
Joined
Feb 26, 2018
Posts
47
Reaction score
59
Habari zenu wadau. Poleni na majukumu. Nna trekta nakaribia kukamilisha ununuzi wake rasmi kwa ajili ya kuchapa kazi na mpango wangu ni kulikodisha kwa wadau wataolima kwa kutumia trekta naomba mwongozo kwa wenye experience na eneo hili je malipo kwa heka ni kiasi gani na kuhusu maintenance ya chombo ni kipi nizingatie na kama kuna ya ziada naomba tuelimishane.
Nawasikiliza na Mungu awabariki kwa mda na mawazo mtakayonipa 🙏🏿
 
Ilitakiwa kwanza uulize bei na maeneo nidyo unue hilo tractor. Sasa ww unafanya kinyume
 
kuhusu bei zinatofautiana kila mikoa ila sehemu zenye trekt anyingi bei huwa chini kidogo ila hucheza 40,000 mpaka 60,000, namna ya kutunza ni kuwa makini na kila kitu kihusikacho na tractor, Mungu akikujalia jitahidi kulima mashamba yako mwenyewe utapata saida maradufu kuliko vibarua,
Fanya hivi lima heka zako ka 50 na kuendele alafu ulime na vibarua vya watu ikiwa ni kutafuta hela kwaajili ya kuhudumia shamba lako
 
mkuu jitahidi ufanikishe lengo mapema, naona ka unachelewa kushika pesa
 
Habari zenu wadau. Poleni na majukumu. Nna trekta nakaribia kukamilisha ununuzi wake rasmi kwa ajili ya kuchapa kazi na mpango wangu ni kulikodisha kwa wadau wataolima kwa kutumia trekta naomba mwongozo kwa wenye experience na eneo hili je malipo kwa heka ni kiasi gani na kuhusu maintenance ya chombo ni kipi nizingatie na kama kuna ya ziada naomba tuelimishane.
Nawasikiliza na Mungu awabariki kwa mda na mawazo mtakayonipa 🙏🏿

Kisarawe tunalimishwa ekari moja kwa shilingi 60,000 hadi 70,000.00 karibu Kisarawe
 
Mvomero kulima heka moja shamba la mpunga ni Tsh 40,000, shamba likiwa jipya au liliachwa kulima zaid ya mwaka tunaita kukatua ni Tsh 45,000, kulima kwa kutumia harrow ni 35,000, kupiga rija ni 35,000, kulima shamba la mahindi ni 30,000 hadi 40,000 kwasababu ulimaji wa mashamba ya mpunga na mahindi mashamba yanatofautiana. Na Malipo ya operator wa trekta huwa 5,000 hadi 7,000 kwa kila heka. Heka moja kwa trekta la 4 wheel akilima bila kutumia 4 wheel huwa linatumia mafuta kiasi gani shamba la mpunga na mahindi na shamba la mahindi watakuja wadau wengine
 
Eka moja tractor la HP 75 linatumia mafuta kiasi gani, naona bei za kulima zipo chini ukilinganisha na gharama
 
Huku kwetu inategemeana na ardhi na jembe linalotumika mashamba ya mahindi ni 35,000 (harrowing), 50,000 (disc ploughing). Mashamba ya mpunga ni 60,000 (harrow) na 70,000 (disc). Karibu sana Mbarali
 
Back
Top Bottom