Malipo ya serikali na figure ambazo hazipo kwenye mzunguko wa fedha

Malipo ya serikali na figure ambazo hazipo kwenye mzunguko wa fedha

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Katika uchumi kila namba ina umuhimu mkubwa either ni kubwa au ndogo hivi sasa Tanzania kwenye currency system sarafu ya Tshs 50 ndio kima cha chini kama means of exchange na Noti ya 10000 ndio kima cha juu.

Katika concept ya kawaida tunatarajia malipo yote yatapangwa kutokana na uwepo wa sarafu na noti zilizopo kwenye mzunguko mfano badala ya kuwepo malipo ya 535 ambayo yatafanya mlipaji kudhulimiwa shilling 15 yake kutokana na sarafu hiyo kutotumika kwa sasa ni busara kuamua iwe 500 au 550.

Sasa Malipo mengi ya serikali yanayokuja kwa mfumo wa control number ndivyo yalivyo unakuta amount inakuja 88,955/= katika mazingira hayo unalazimika kulipa 89,000/= means umelipa zaidi hususani tunaotumia mawakala au mabenki kulipa means umelipa zaidi ambayo kiuchumi inaweza kukuaffect kama ni mtu unayefanya transaction nyingi na pia inaweza kuleta utata wakati wa auditing.

Ingekuwa sawa kama Tanzania tupo katika paperless money lakini hatupo huko. Ushauri wangu japo najua hauwezi kuzingatiwa sababu ya status yangu na ukizingatia nilipata mswaki katika somo la Mathematics ningependa serikali yangu iliangalie hili swala na ikiwapendeza walifanyie kazi.
 
Umasikini mbaya
Mfano mimi kwa Siku naweza kufanya malipo mara 300. nikiwa napoteza shilling 45 kwa kila transaction moja sasa fanya hesabu kwa Transaction 300 itakuwa shilling ngapi?

Ni 13500 per day times siku 30 itakuwa shilling ngapi ni kiwango kikubwa sio tu kwa masikini hata tajiri pia.

Sio umasikini wala utajiri.
 
Ndio maana nikasema lipa mwenyewe.

Huna haja ya kulaumu SERIKALI.
Sio lawama ni mapendekezo.. kama watakuwa wanaweke hizo figure waturudishie sarafu za shilling 5, 10 na 20 ili mtu apate kile anachodeserve..
 
Sio lawama ni mapendekezo.. kama watakuwa wanaweke hizo figure waturudishie sarafu za shilling 5, 10 na 20 ili mtu apate kile anachodeserve..
Mkuu kwa sasa kinchowezekana ni kuweka pesa kwenye akaunti yako kisha lipia kiasi kinachohitajika!

Hizo sijui 45, 15/= zitabaki kwenye akaunti yako!!

Hongera kwa pendekezo zuri pia..
 
Mimi nikitaka kutoa fedha kwa hawa mawakala kama ni Tsh elfu kumi natoa 9999 nakwepa makato yao basi kivumbi namuachia wakala anung'unike hadi anye
lakini lazima anipe elfu kumi.
 
Back
Top Bottom