A
Anonymous
Guest
Mimi ni mzazi wa mwanafunzi anayesoma katika shule yenu. Ninaomba kuwasilisha hoja yangu kuhusu malipo ya Shilingi 90,000 yaliyotakiwa kwa ajili ya masomo ya ziada kipindi hiki cha likizo.
Kwanza, tulielezwa kuwa fedha hizo zilikuwa kwa ajili ya masomo ya ziada ya kipindi chote cha likizo. Hata hivyo, watoto wamesoma kwa takribani wiki mbili pekee. Hali hiyo inaleta swali la msingi kuhusu uhalali wa kulipisha kiasi kile kile kilichopangwa awali bila kuzingatia muda halisi wa masomo yaliyotolewa.
Pili, tumeelezwa kuwa kila mzazi analazimika kulipa Sh. 90,000 hata kama mtoto wake hakuhudhuria masomo hayo.
Aidha, tumeambiwa kwamba asipolipa, fedha hizo zitakatwa kwenye ada ya shule. Hatua hii inaonekana si ya haki kwa wazazi ambao watoto wao hawakunufaika na huduma hiyo.