Malipo ya TFDA - Mamlaka ya dawa na chakuka

ommy15

JF-Expert Member
Joined
Jan 23, 2011
Posts
674
Reaction score
1,017
Habari wadau. Natumaini ni wazima. Naomba kupata ifahamu toka kwenu kwamba ni vigezo gani au biashara gani zinazotakiwa kulipia TFDA kwani tulizoe kwamba wanaolipia hicho kitu ni wale wanaouza vyakula kama migahawa,hotel,fresh food,maduka ya madawa nk.

Lakini mwaka huu naona tumeongezwa na sisi wenye maduka ya vitu vya matumizi ya nyumbani yaani maduka yanayouza sabuni,mafuta,sukari,chumvi nk tena reja reja.

Sasa nilitaka kujua nini hasa kimetokea hadi na sisi tukaingia huko au kipindi cha nyuma nini kilishindikana kututoza?

Kwa sasa inaanzia sh 100,000/. Hapo jumlisha kodi ya tra,leseni ya biashara unakuta jumla sio chini ya laki 6.
 
Aisee..na huko wamefika ?? Nzuri kujua sheria yake inasemaje ! Wajuzi embu njooni...
 
Labda na wao wamewekewa lengo la makusanyo
 
Aisee..na huko wamefika ?? Nzuri kujua sheria yake inasemaje ! Wajuzi embu njooni...
Aisee acha tu inaumiza sana unajibana bana ujiajiri lakin makodi na matozo ni mengi hatari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…