KERO Malipo yaliyokwama kwa Yas kwa zaidi ya saa 24 yananiongezea gharama zisizo za lazima

KERO Malipo yaliyokwama kwa Yas kwa zaidi ya saa 24 yananiongezea gharama zisizo za lazima

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nimelipia huduma za Serikali kupitia Lipa Namba kwa miamala miwili ili kumtoa mgonjwa wangu hospitalini.

Nimeelezwa kuwa malipo hayo hushughulikiwa ndani ya saa 24, lakini hadi sasa zaidi ya saa 24 zimepita na bado sijafanikiwa kumtoa mgonjwa kwa sababu malipo hayajaonekana.

Sina fedha nyingine za kufanya malipo mapya. Tatizo hili limenisababishia usumbufu na gharama zisizo za lazima kutokana na mtandao wa Yas.

Pia, malipo yanapofanyika mara mbili baada ya muamala wa kwanza kushindikana, fedha za muamala uliofeli hazirejeshwi.

Naomba mamlaka husika ziingilie kati na kulifanyia kazi tatizo hili haraka.
 
Back
Top Bottom