BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
#Updates
Usiku wa kuamkia leo Juni 7, 2024, Malisa amefikishwa Moshi Mjini, na Jeshi la Polisi limempeleka moja kwa moja Ofisi ya RCO.
Taarifa kutoka CHADEMA zinaeleza kuwa Wakili Peter Kidumbuyo ameambatana na Malisa katika mahojiano hayo.
Picha tofauti za Malisa na Boni wakiwa na Wadau mbalimbali walipofika Mahakamani katika suala lao.
====
Kinachoendelea kuhusu tuhuma za Malisa
Taarifa kutoka Moshi zinaeleza kuwa Malisa alihojiwa kwa takribani Saa tano (5 hours) jana usiku (Usiku wa kuamkia Juni 7, 2024) juu ya andiko lake la Desemba 28, 2023 kuhusu mauaji ya Beatrice wa Rombo.
Katika taarifa ya kifo hicho, Godlisten Malisa anadaiwa aliandika "Inadaiwa kuwa kijana aliyesababisha mauaji ya Beatrice ni shamba Boy wa Waziri wa Elimu, Profesa Mkenda.
Leo Juni 7, 2024, Mawakili wamefika kwa RCO kutaka kupata uwezekano wa dhamana lakini RCO ameeleza kuwa wanawasubiri Polisi kutoka Dodoma, Arusha na Dar es Salaam ambao wako njiani Kwenda kumhoji.
RCO amedai kwamba Naibu DCI yuko njiani kwenda kumhoji Malisa Moshi.
Kwa ufupi Malisa anadaiwa kuwa na tuhuma tatu tofauti, ya taarifa ya kifo cha Beatrice, inadaiwa kuna taarifa nyingine ya kifo cha Mwanafunzi pamoja na matokeo ya kidato cha nne kwamba kuna upangaji wa matokeo.
===============
Alichoandika Boniface Jacob kwenye ukurasa wake wa Twitter:
NAIBU MKURUGENZI MAKOSA YA JINAI HANA KAZI ZA KUFANYA....?
Nimejaribu kusoma andiko la @MalisaGJ_ ambalo nimetaarifiwa na Mawakili kuwa ni shitaka la pili la Malisa ambalo atahojiwa na Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai mwenyewe.
ambaye anasafiri kutoka Dodoma kwenda Kilimanjaro kumuhoji Malisa sababu ya Kukosoa na kutoa maoni kuhusu Combinations mpya za Masomo ya Kidato cha tano na Cha Sita.
Nimejikuta namuonea huruma Naibu Mkurugenzi bure,na nimesikitika gharama za posho za safari na mafuta na rasilimali za Taifa zinavyotumika Vibaya.
Najiuliza Jeshi la Polisi wapo serious kweli.? Wanajua wajibu wao..? Na Je Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai hana shughuli zingine za kufanya..?
Andiko la Malisa linawezaje kuwa tishio la Usalama wa raia na mali zao..?
Nguvu ya kusoma na kukamata wakosoaji wa Serikali kwanini zisitumike kutafuta wanaoteka na kupoteza watu..?
SOMA NA WEWE UNIAMBIE,KUNA KESI HAPA...? 👇👇👇👇👇
Angalia hawa vishohia wa TAMISEMI "wanavyokoroga" mambo. Anayesoma HGK atasoma Kiswahili (Sarufi na Fasihi), lakini anayesoma HGFa atasoma Fasihi peke yake. Maana yake ni kwamba anayesoma HGK akiona Sarufi inamshinda anaachana nayo anabaki na Fasihi tu, halafu combination inabadilika kutoka HGK kuwa HGFa.
Na wa HGL atasoma Kingereza (Grammar na Literature), lakini yule wa HGLi atasoma Literature tu. Maana yake ni kwamba mtu wa HGL akiona Phonology, Syntax na Semantics zinamsumbua anapiga chini Grammar anabakia na Literature tu, halafu combination inabadilika kutoka HGL kuwa HGLi. Ujinga gani huu?
Hivi hawa watu wametumia akili kweli? Au hawajali kwa sababu watoto wao wanasoma mitaala ya Cambridge na International Baccalaureate? Katika hili "Mkwe" kazingua, na ametukosea sana Watanzania. Aondoe huu mkeka akausuke upya kwa kushirikisha wataalamu. Vinginevyo Historia itakuja kumhukumu kama ilivyomhukumu Mungai kwa kufuta michezo shuleni, au kama inavyomhukumu Kawambwa kwa kuunganisha Physics na Chemistry. "Mkwe" ana nafasi ya kurekebisha makosa, asisubiri Historia imhukumu.!
Pia soma: