Malisa GJ: Rais Samia anawakaanga MATAGA

Huu mchanganuo umfikie Mwenyekiti wa CDM Freman Mbowe. Mama ana akili sana au amezungukwa na watu wenye akili na weledi. Hongera Malisa GJ
 
Siasa za vyama vya upinzani zinasikitisha sana,sioni dalili za chama cha upinzani kushika Dola.

Kutokana na katiba yetu na baadhi ya sheria zetu,zinaweka mazingira magumu ya demokrasia ya vyama vingi,kiasi kwamba hakuna usawa katika mizani ya ushindani.

Kwenye awamu ya tatu wapinzani walikuja na baadhi ya madai ya kimsingi kabisa,wakitaka mabadiliko ya katiba na mabadiliko ya baadhi ya sheria za jamhuri na kanuni zinazosimamia sheria mbalimbali hasa za kiuchaguzi ili kuweka mizani ya kidemokrasia sawa.

Matokeo hatukuyaona zaidi waliishia kuvurugana tu,wakigombea ruzuku mwisho kusambaratika kabisa,hadi kufika uchaguzi wa 2005,hawakuwa na mgombea urais mwenye nguvu wala hawakuwa na agenda inayoeleweka hivyo hata madai yao kukosa nguvu,hivyo mgombea Urais wa CCM wakati huo mh. Kikwete kushinda kiulaini kabisa.

Katika miaka mitano ya kwanza ya awamu ya nne,wakaachana na madai ya katiba,na marekebisho ya sheria za uchaguzi na kanuni zake!!wakaja na agenda ya kuibua ufisadi iliyoasisiwa na katibu mkuu wa chadema enzi hizo DK Slaa.Agenda hio ikapata umaarufu sana,wananchi wakawaelewa,uchaguzi wa mwaka 2010 wakaleta changamoto kubwa kwa chama cha mapinduzi japo walishindwa ila walipata wabunge si haba.

Miaka mitano ya pili ya awamu ya nne wakaibua agenda yao ya toka awamu ya tatu, ya kutaka mabadiliko ya katiba wakaanzisha maandamano nchi nzima, mpaka mh.kikwete akakubali mchakato wa mabadiliko ukaanza,japokuwa walishindwa kujipanga vizuri mchakato ukafia njiani,tena mmoja wa aliesababisha mchakato ufie njiani ndie alikuja kuwa mgombea wao wa Urais mwaka 2015, na mwingine leo ndio mh. Rais wa jamhuri ya muungano wa awamu ya sita.

Mwaka 2015,kwenye uchaguzi mkuu katika hali isiyo ya kawaida dakika za mwisho kuelekea uchaguzi!! wakaleta mtu ambae wengi hawakutalajia ambae amekulia na kulelewa kwenye chama cha mapinduzi,ambae siku zote walikuwa wanamsema ni fisadi mkubwa.

Mtu mliekuwa mnamsema ni fisadi,mnamleta ili asimamie agenda yenu ya kukomesha ufisadi!!maajabu makubwa!! Mwisho wa siku wakokosa agendas ya kusimamia kwenye uchaguzi,wakaishia kuvurugana na mwisho kupoteza uchaguzi wenyewe, na CCM kuibuka mshindi kupitia kwa mgombea wake Hayati Magufuli.

Miaka mitano ya kwanza ya awamu ya tano, ilikuwa migumu sana kwao maana walikosa kabisa agenda,licha ya kupata wabunge wengi wakakosa namna ya kujipanga wakawa wanatoka bungeni hovyo bila sababu,wakakosa mbinu ya kupambana na utawala wa Hayati Magufuli,ambae alionyesha kutekeleza mambo mengi hivyo wananchi wengi walijenga imani nae,hasa baada ya wao kushindwa kusimamia agenda yao ya ufisadi waliokuwa Wana jaribu kuihubiri miaka yote.

Uchaguzi mkuu wa mwaka 2020,japokuwa walikuwa na mgombea mzuri upande wa chadema ila walikuwa hawana sera zinazoeleweka,zaidi mgombea wao alikuwa anahubiri tu madhara yaliyompata kutokana na kupinga sera za Hayati Magufuli!!kuliko kuwaeleza wananchi hatawafanyia nn?!!kuwaletea maendeleo.

Tunajua uchaguzi huo ulikuwa na changamoto kubwa sana,ila changamoto zingine zilisababishwa na wao kushindwa kujipanga na hasa kujifunza CCM uwa inafanya nini hasa inapokaribia kwenye uchaguzi mkuu!!walitegemea CCM ipate mpasuko,wanasahau CCM ndio mabingwa wa sayansi ya siasa. Na ili kukabiliana nao inabidi ufanye siasa za kisayansi zaidi pia ili uweze kuwashinda.

Leo tunaona wengi wa wapinzani wakishangilia kuondoka kwa mtawala wa awamu ya tano, Hayati Magufuli,ila wanasahau kuwa CCM ni ile ile ambayo inajibadili kama kinyonga,mama yetu mh.Rais Samia,kipindi cha kampeini uko mbeya alinukuliwa akisema kuwa:hata wananchi wasipoipigia CCM kura lakini wajue ndio itakayotangazwa na ndio itakayoongoza serikali!!na kweli tuliona CCM ikitangazwa kushinda katika baadhi ya majimbo na kata katika mazingira yaliyozua maswali mengi.

Lakini leo hii wapinzani hao hao ndio wanaomshangilia mama mh.Rais wakidai wana imani nae sana,hasa baada ya hotuba yake,pale aliposema atawaita ikulu waje wajadiliane nae!! Sasa maswali ni mengi je mama mh.Rais.hajui madai yao?!!je toka waanze kwenda ikulu enzi za mh kikwete ni nini walichokuwa wanajadili mpaka leo hawajawahi kupata muafaka?!!je sio kwamba ni mbinu za kisayansi za CCM kupoozesha washindani wake?!!

Wapinzani hawana agenda kiasi cha kutaka huruma ya mtawala ili wafanye siasa zao?!! Maswali ni mengi ila tunachoweza kuona ni kuwa wapinzani bado hawajawa na watu wakufanya siasa za kweli,wanachotaka tu ni huruma za mtawala ili wapate ruzuku na opportunities nyingine za kisiasa kwa manufaa yao na familia zao kwa mgongo wa upinzani.
 
Ujinga wa Malisa ni kuwa hana issue yeye kabaki mtu wa matukio kurukia yale yasiyo mhusu,aongelee sera za SACCOSS yake badala ya kupoteza bando zake kushadadia mambo yasiyo na tija kwa SACCOSS yao,nadhani kama ni katibu mwenezi au mtu wa propaganda kazi imemshinda.
 
Hapa Dj Mbowe ameumia sana kuona Mama Samia hayuko tayari kumsaliti Magufuli.
Mbowe amefoka Twita kwa uchungu sana.
Sidhani kama ataenda kwenye hicho kikao atakachoitwa ikulu.

Nyumbu ni nyumbu kwa akili ya Malisa anqdhqni Samia ni rais anayetokana na Chadema!!!
 
Kwaiyo mama amegeuka nge anafuna na kuvunguia, mataga walipiga makofi sana na vinyimbo vya kike kike ajabu na wanaume nao wanademka demka ata wakitajwa wanawake na wao wanainuka tafran tupu
 
QUOTE="Mkaruka, post: 38812318, member: 123346"]
Vijana wa CHADEMA sometimes inasikitisha tu.

CHADEMA ya kina Zitto, Slaa, Mnyika, haitakuja kujirudia

Kweli kila awamu na kitabu chake.
[
Nyerere alituachia CCM Safi,Sasa hivi imekua Mafioso, intarahamwe,genge la utekaji na uuaju.
 
HATA KAMA MTU ATAPINGA UCHAMBUZI HUU, ATAFANYA HIVYO KUJIPA AFUAENI NA FARAJA BANDIA KWA MOYO WAKE. UMECHAMBUA VEMA NA HUO NDIO UHALISIA.
 
Hakika💯💯💯💯
 
Haya ni mawazo ya Malisa,kilamtu ana mawazo yake hata mwenyekiti jana alitweet mawazo yake ambayo ni tofauti na haya ya Malisa.
Namuunga mkono Malisa katika mtazamo wake huu. Mama ameonesha kuwa anaamini kuwa TANZANIA NI TAIFA MOJA LINALOFUATA UTAWALA WA SHERIA NA DEMOKRASIA YA VYAMA VINGI! Najua kuna makosa yaliyofanywa na mwendazake ambayo hawezi kuyarekebisha lakini atahakikisha kuwa hayarudiwi siku zijazo. Kwa mfano hawezi kusema kuwa turudie chaguzi zile zilizopokwa na mwendazake, laki pindi uchaguzi mwingine ukifika hayatarudiwa tena. Kwa ujumla hotuba yake onadhihirisha kuwa ana nia njema kwa taifa. Anatengeneza taasisi badala ya uimla wa mwendazake.

Nilikuwa natamani kusikia mtizamo wa mama kuhusu KATIBA MPYA. Anatuambia atafanya nini kuhusu hilo hata kama sio kesho?
 
Unapoandika weka facts zote mezani. Mwendazake hakuruhusu vyama vya upinzani kushiriki shughuli za Siasa kwa miaka yote 5 na akaishia kujiandikia matokeo ya uchaguzi bila kuhesabu kura na kujipa 84%.

Ulitaka vyama vya upinzani viingie mwituni?
 
Wewe chadema inakuhusu nini mwanaccm tena taga la marehemu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…