Malkia Elizabeth (1926 - 2022) Katika Nyaraka za Sykes

Malkia Elizabeth (1926 - 2022) Katika Nyaraka za Sykes

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
MALKIA ELIZABETH (1926 - 2022) KATIKA NYARAKA ZA SYKES 1953

Katika nyaraka za Sykes kuna nakala ya barua ya tarehe 2 June, 1953 kutoka TAA kwenda kwa Malkia Elizabeth iliyotiwa saini na viongozi wote wa TAA 1953:

Rais: Julius Nyerere
Makamu wa Rais: Abdulwahid Sykes
Katibu Mkuu: Dome Okochi Budohi
Naibu Katibu: W. Dossa Aziz
Mweka Hazina: John Rupia Naibu Mweka Hazina: Ally SykesBarua hii inampongeza Malkia Elizabeth kwa kutawazwa kuwa Malkia wa Uingereza.

1662675265625.png
1662675406737.png
1662675426744.png
1662675450110.png
1662675517705.png
1662675543406.png
1662675566855.png
1662675594518.png
 
Attachments

  • 1662675478374.png
    1662675478374.png
    420.5 KB · Views: 22
Kwa waliosahau nawakumbusha kuwa Mwingereza alikuwa msimamizi wa Tanganyika.

Ndiyo maana utaona akina Nyerere wakiandika barua ya kirafiki kwa Malkia. Hapa nafikiria eti Dedan Kimathi amwandikie Malkia barua ya kumpongeza au Samora amwandikie Rais wa Ureno barua ya kumpongeza!
 
Plato...
Nimecheka.
Tofauti ipo katika namna ya ukoloni ulivyokuwa nchini.

Wazee wetu hapo wanasema wao ''raia watiifu.''
Wakikuyu kwa ile dhulma ya kuporwa ardhi yao waliamua kunyanyua silaha.

Uovu wa Wareno kwa watu wa Msumbiji na kwa hakika makoloni yao yote ndiyo uliosababisha adui mkubwa dhidi yao.
 
Kinyungu,
Katika hizi Nyaraza za Sykes nilikuta mambo mengi sana.

Laiti kama ningelipewa fursa ya kuzipitia upya nadhani ningeweza kuandika kitabu kingine.
Muda unao.
Naomba uganye hivyo kuanzia leo kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo
 
Muda unao.
Naomba uganye hivyo kuanzia leo kwa faida ya vizazi vilivyopo na vijavyo
Kinyungu,
Nimechoka kaka miaka 70 si mchezo.
Hiyo remote ya TV mpaka wajukuu zangu waniwashie.
 
Back
Top Bottom