Malkia Elizabeth II na Afrika

Malkia Elizabeth II na Afrika

Yussufhaji

Member
Joined
Sep 9, 2018
Posts
35
Reaction score
28
“UHUSIANO WENYE PANDE MBILI ZA SARAFU”

10/09/2022
1662753989875.jpg

Ukiniuliza kuhusu uhuisano wa Malkia Elizabeth wa Pili na Afrika basi nitakujibu kuwa ni uhusiano wenye pande mbili za sarafu, kwa upande wa kwanza wa sarafu umegubikwa na masuala tata kama:-
Ukoloni; Hakuna shaka yeyote kuwa lawama za kulitawala bara la Afrika kwa nguvu hazikwepeki kwa Uengereza na Malkia Elizabeth wa Pili kama kiongozi wake mkuu hatoki kwenye lawama hizo, ukizingatia kipindi ambacho alichoingia mamlakani kama Malkia wa Uengereza ndio kipindi haswa cha purukushani za mapambano baina ya wanaharakati wa kudai uhuru wa Afrika dhidi ya vikosi kandamizi vya mkoloni Muengereza zilipo pamba moto, kule Kenya Mapambano makali dhidi ya vikosi vya mkoloni Muengereza yalioitwa “Mau Mau” yakiongozwa na mwana wa Afrika Didan Kimathi yalifanyika, Didan Kimathi alifariki kwa kunyongwa na utawala wa mkoloni Muengereza mwaka 1957,
Hakuna asiyejua maumivu na madhara ya ukoloni kwa Afrika.

Vita vya Biafra; Wengi wanaelekeza lawama kwa Malkia Elizabeth wa Pili kwa kushindwa kutumia ushawishi wake kuzuia mauaji ya watu zaidi ya milioni moja katika vita vya Biafra miaka ya 1960s-70, kama Uengereza ingelibaki na kutochagua upande na kuwa mpatanishi huenda mauaji ya Biafra yangekwepeka, lakini badala yake iliangalia upande upi utalinda maslahi yake ya kibeberu na kufadhili kwa kuupatia silaha mbalimbali,

Ukoloni mambo leo; Malkia Elizabeth wa Pili amekuwa akishutumiwa na baadhi ya wanasiasa na wanahistoria wa Afrika juu ya uhusika wake katika kuendeleza ukoloni kwa Afrika, huku Jumuiya ya madola (Umoja wa nchi zilizokuwa chini ya utawala na ukoloni wa Uengereza + nchi zinazozungumza kiengereza) imekuwa ikinyooshewa vidole juu ya kuendeleza ukoloni kwa Afrika, Malkia Elizabeth wa Pili amekuwa Mkuu wa Jumuiya ya Madola katika miaka yote ya Uongozi wake, aliyekuwa Rais wa nchi huru ya Zimbabwe, Robert Mugabe aliwahi kunukuliwa kuwa;
„The Commonwealth is a mere club, but it has become like an 'Animal Farm' where some members are more equal than others. How can Blair claim to regulate and direct events and still say all of us are equals?“
-Robert Mugabe
Zimbabwe ilijitoa katika Jumuiya ya Madola mwaka 2003.

Upande mwengine wa sarafu unapambwa na sifa njema lukuki, kama:-
Utayari wa kuzungumza na Afrika; Kiburi si maungwana, utayari wake wa kukaa meza moja na wanasiasa na wapigania uhuru wa Afrika kulirahisisha nchi mbalimbaii za Afrika kujipatia uhuru wake, na kubadilisha haiba ya Malkia Elizabeth wa Pili kwa Afrika, miaka mitano baada ya kutawazwa kwakwe kuwa malkia wa Uengereza, Ghana ilikuwa nchi ya kwanza Kusini mwa Jangwa la Sahara kupata uhuru wake mwaka 1957 kutoka kwa mkoloni Muingereza, zaidi muafaka wa kukabidhi nchi ya Zimbabwe kwa Robert Mugabe kutoka serikali ya Ian Smith mwaka 1980,
1662753960378.jpg

Uhusiano mpya baina ya Uengereza na Dola huru za Afrika; Ziara alizozifanya katika nchi za bara la Afrika mara baada ya nchi hizo kupata uhuru ziliweka njia na barabara mpya ya uhusiano baina ya aliyekuwa mkoloni na koloni, sasa uhusiano ni baina ya nchi na nchi zilizo huru, mara baada ya serikali ya kikaburu ya Afrika Kusini kuondoka mamlakani, aliitembelea nchi hiyo mara 2, jambo ambalo limesaidia kuboresha mahusiano baina ya Uengereza, Afrika Kusini na nchi nyengine za Afrika.

NB: Maoni yangu binafsi juu ya uhusiano wa Afrika na Malkia Elizabeth II.

#Maonibinafsi
#Mtizamobinafsi

@Syn_krestiyanina
+2557777158131
hajjyussuf2@gmail.com
 

Attachments

  • 1662753915542.jpg
    1662753915542.jpg
    28.9 KB · Views: 9
Back
Top Bottom