KWELI Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba

KWELI Malori yakwama bandarini Dar, madereva walalamikia ukiritimba

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Mwananchi Digital imeripoti kuwa katika bandari ya Dar es Salaam kuna malori (magari makubwa ya mizigo) yamekwama kwa siku kadhaa hivyo kusababisha madereva wa maroli kulala na kuamka hapo hadi kufikia siku nne, madereva hao wamedai kulala na kula kwenye magari yao na kuomba kujisadia katika vyoo vya ofisi za jirani kwa kuwa hapo bandarini hakuna vyoo.

Madereva hao wamedai chanzo cha uchelewashaji huo wa mizigo unatokana na ucheleweshwaji wa kupakua na kupakia mizigo na na ucheleweshwaji wa vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.

1658210425300.png
 
Tunachokijua
Mei 11, 2021 Madereva wa magari ya mizigo wamelalamikia ucheleweshwaji wa utoaji huduma katika bandari ya Dar es Salaam. Suala hilo liliwafanya wakae muda mrefu na kusababisha foleni. Moja kati ya chombo cha habari nchini, Mwananchi Digital walipiga picha msururu wa magari yaliyokuwa bandarini, hata hivyo video hiyo iliondolewa katika mtandao wa YouTube.

Video ya msururu wa magari unaweza kuiona HAPA.

Chanzo cha adha hiyo ilikuwa ni pamoja na ucheleweshwaji katika kupakia na kupakua mizigo pamoja na kupatikana vibali vinavyoruhusu mizigo kusafirishwa.

Baada ya malalamiko ya adha hiyo, Mei 12, 2021 Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa alifanya ziara bandarini hapo ili kujionea hali ilivyokuwa na aliagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Mamlaka ya Serikali Mtandao kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuboresha utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam.

Akiwa Bandarini hapo Waziri Mkuu alisema, TPA endeleeni kuiimarisha bandari yetu, hii ni sura ya uchumi wa nchi yetu, zungumzeni lugha moja ya uwajibikaji, TRA muwepo maeneo yote yanayohitaji uwepo wenu na muda wote wateja wetu wahudumiwe ili bandari yetu iendelee kuwa bora. Nchi nyingi zinatutegemea”

Amesema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania ihakikishe mfumo wa pamoja wa forodha Tanzania (TANCIS) unafanya kazi kwa ufanisi ili kupuinguza malalamiko ya wateja kuhusu mfumo huo.

“Dosari zote za mfumo wa TANCIS zifanyiwe kazi, mfumo usituharibie, mnapoona kuna madhaifu fanyeni marekebisho ya haraka, tunataka wateja waingie na kutoka kwa muda mfupi” Alisema.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Eric Hamissi amefafanua hatua ambazo tayari TPA imechukua katika kuhakikisha Bandari inatoa huduma zenye tija na ufanisi ambapo pia amewaomba Wadau kuwa na uvumilivu wakati kazi ya kukarabati magati ikitarajiwa kukamilika mwezi Agosti mwaka huu.

Kwa upande mwingine Waziri Mkuu amemuagiza Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania kuhakikisha mifumo yote ya utoaji mizigo Bandarini hususani mfumo wa TANSIC unaimarishwa ili kuiwezesha Bandari na Wadau wengine nao kufanya kazi kwa ufanisi na tija.
Back
Top Bottom