Malumbano ya Spika Sitta na Mzee Mrema

Keshapata cha kusingizia akikosa ubunge huko vunjo!
 
Hivi kwani si kweli Mrema ameathirika? Kweli ana hali mbaya, amechoka ndo maana anatafuta pa kutokea.
 
Huyu mzee anaumwa kimwili, kiakili na kihali na mali. Hii kokoro yote anayofanya ni katika kutaka kufanikisha yafuatayo:
1. Kupata kuungwa mkono na kundi la mafisadi ya CCM ili apate kugombea jimbo la Vunjo. Anajua kabisa mbunge wa sasa mafisadi hawamtaki kwa hiyo anajaribu kubahatisha hapo. Mara anamsifia JK, mara anamshambulia Sitta, yote kuwajulisha mafisadi mimi niko hapa nitumieni.
2. Kupata hisani ya mafisadi kwa ajili ya mkate wake wa kila siku, anajua akimvaa Sitta lazima mafisadi watafurahi na japo kumrushia hapo chochote. Njaa mbaya jamani!

Si muda mrefu utasikia mzee huyu karudi kundini, labda mafisadi wamdharau na wasihitaji kumtumia.

Najuuuuta kulisukuma gari la Mrema 1994 kwenye vilima vya UDSM...kiu ya mabadiliko ingetuponza kuwa na rais pambafu kama huyu!
 
Mrema ataka alipwe Sh bilioni 1 na Sitta

i
Mrema amempa Sitta taarifa ya kusudio la kumfungulia kesi ya madai mahakamani endapo hatatimiza masharti ya kumfidia na kumwomba radhi.

Katika barua aliyoiandika juzi, Mrema amempa Sitta siku saba hadi Jumatatu ijayo, kutimiza masharti yake kabla ya kumfikisha mahakamani.

“Naomba kukufahamisha, kwamba ninakusudia kukufungulia kesi ya madai Mahakama Kuu ya Tanzania kutokana na wewe Mheshimiwa Sitta kunitukana, kunikashifu, kunivunjia heshima na kunidhalilisha kupitia magazetini,” inasema sehemu ya barua ya Mrema kwa Spika Sitta.

Barua hiyo inaendelea: “Vinginevyo, uniombe radhi kupitia magazeti yale yale na kwa uzito ule ule katika kipindi cha siku saba tangu utakapopokea barua hii; unilipe fidia ya Sh bilioni moja.”

Akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu katika Serikali ya Awamu ya Pili, Mrema alikuwa na kawaida ya kutoa siku saba kwa wahusika kutekeleza maagizo yake kabla hajachukua hatua.

Alinukuu gazeti la Mwananchi la Machi 5 mwaka huu, ambalo lilimkariri Sitta akimwita Mrema mhuni na aliyepitwa na wakati, aliyefilisika kisiasa na kifedha na kwamba sasa anatafuta njia ya kujinasua kutoka hali hiyo.

Mrema anadai kwamba kauli hizo, akiwa Mwenyekiti wa Taifa wa TLP, zimesababisha wanachama wapatao 500,000 nchini wakose imani naye. Na pia kauli hizo anadai zimemvunjia heshima aliyojijengea kutokana na utumishi wake wa zaidi ya miaka 30 akiwa Ofisa Usalama wa Taifa, Mbunge, Waziri na Naibu Waziri Mkuu.

Alisisitiza: “Kauli zako zimeniathiri, kwa sababu nimeshajitangaza kugombea ubunge wa jimbo la Vunjo.

Hivyo kauli zako zinaweza kutumiwa na wapinzani wangu dhidi yangu.” Akizungumza na gazeti hili, Mrema alisema anaendelea na mchakato wa kuandaa mwanasheria atakayesimamia shauri lake.

Alisema Mahakama pekee ndiyo itakayotoa tafsiri halali kama Sitta alimdhalilisha au la. Gazeti hili lilimtafuta Spika Sitta kwa simu kwa lengo la kumuuliza kama amepokea taarifa ya Mrema, lakini simu yake haikupatikana.

Mazingira ya kutofautiana kati ya Spika Sitta na Mrema yamekuwa yakidhihirika kupitia vyombo vya habari.

Mrema aliitisha mkutano wa waandishi wa habari hivi karibuni na kudai kwamba Sitta ni mchochezi, mjenga makundi na mtu anayehatarisha amani na usalama wa nchi, kauli ambayo inadaiwa pia Spika aliijibu kupitia Mwananchi.

CHANZO: HABARILEO
 
naona kama Mrema anaelekea kuchanganyikiwa, namuona ni kama mtu anaehitaji faraja na upendo
 
Jamani Huyu Mrema mimi binafsi naona kafulia si mchezo! Ivi tangu lini na ni wapi, hapa na hii hali tuliyonayo mtu wa upinzani tulitarajia kuwa angekuwa anaangalia upande wa pili eti anaunga mkono serikali.
Angekuwa sahihi kama angekuwa anatangaza sera zakepoa. lakini kimsingi naona anaimisi sana CCM na pia yupo upande fulani wa CCM.
Lakini ni vema tu avue uenyekiti wa TLP arudi mbona huwa hawakatazi?
Anatupotosha tu,
 
Mrema hana jipya, anataka kutoka kupitia mgongo wa Sitta na 6 nadhani bado hajashtuka!

Naona hii skendo yake na 6 inampa airtime za kutosha kwenye media kila sehemu,

I can say it's a good move on his side
 
Alianza mwenyewe kumchokoza sasa amerushiwa makombora anaanza kuhaha!

Pengine alianza kusudi ili yaje haya. Yeye hana wafadhili, magazeti wala viongozi wa dini kumpatia hela ya uchaguzi hivyo janja hii inaweza ikamsaidia.
 
Mrema naona sasa anaisha kabisaaaa...anaelekea kufulia kisiasa asijeshangaa hata huko vunjo akakosa ubunge...
Kisingi Vunjo ashashindwa, na huo ndo mwiso wake. Japo inategemea hao watu wa vunjo kama watamtaka mtu wa aina hii. Sidhani kwanza kama ni vema kumlinganisha Kimaro na "Komedian" Mrema
 
Huyu jamaa anatumiwa 'kumchafua' Sita, mmesahau kazi zake mara hii? hamjiulizi kwa nini wakati huu Mrema anamwandama sana Sitta na sio mwingine? ana nguvu gani za kisheria kudai fidia kabla hata kesi haijaenda mahakamani? mahakama si ndo inatoa haki?

Anataka hicho kitita ili asiende mahakamani yaani wayamalize nje ya mahakama. Ni haki ya Sitta kuangalia kipi bora kulipa, kufanya mazungumzo ateremshiwe dau au akapambane mahakamani kama kweli Mrema atakuwa na ubavu wa kwenda mahakamani.
 
Nakubaliana nawe nafikiri ulikuwa mvuto tu.
Nikweli kaathirika na kama ingekuwa ni hayo ya HIV mbona kwa sasa siyo tatizo. ni hili lake na jinsi ambavyo halina dawa ila faraja tu. Kwa huyu bwana uelekeo wake hauna turn about. ndo anaelekea kuwekwa katika histiria hivo!
 
Nani atampa ubunge mtu aliyefilisika kisiasa na kiuchumi

Watanzania hatutabiriki! Hivyo hao wabunge wote walikuwa matajiri walipokwenda huko? au wengi waliupatia utajiri huko?
 

Kwanini tumlaani Mrema kwa siasa za Tanzania ? Viongozi wetu na hata watu maarufu wamekalia kulalamika kuonewa, kufanyiwa hujuma na kuomba kuonewa huruma na wananchi. Hivyo Mrema wacha aendelee kuendeleza Siasa za Kibongo, wacheni kumuandama.
Hili suala ni lake na Sitta na wala hajafanya kipya tulichokuwahatujakiona. Ana haki ya kwenda mahakamani na ana haki ya kuomba kuchaguliwa. Tuache kumuhukumu kwa chuki zetu binafsi.
 
Ngongo hivi kwani Mrema kaanza leo kwenda mahakamani kudai hizo fidia unaweza kutuambia hadi leo ameshalipwa kiasi gani lengo hasa la Mrema ninavyoona mimi huwa si kulipwa ni kuonekana kwa watu kwa lugha ya kileo ni sehemu ya kutokea anajua akiwa anaandikwa kila siku magazetini ndiyo raha yake

Hao uliowataja mbona walishaitana wehu machizi papa manyangumi na fahamu kuwa kwenye siasa hicho ni kitu cha kawaida sijaona kashifa nzito ya kumwingiza Sitta kwenye matatizo nadhani hata mahakama si kama jaa kila kitu kutupiwa italitupilia mbali ombi la Mrema
 
hivi inawezekana kafulia kweli? SASA BILIONI MOJA KWELI YA NINI?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…