Mama achagua umasikini, Mtoto kachagua kujiua

Mama achagua umasikini, Mtoto kachagua kujiua

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
28,297
Reaction score
68,017
MAMA ACHAGUA UMASIKINI, MTOTO ACHAGUA KIFO

Na, Robert Heriel


Tukio la kusikitisha lililotokea Mkoani Katavi ambapo Mtoto amejiua kwa kujinyonga kisa na Mkasa ni mgogoro baina yake na Mama yake mzazi. Mtoto anashauri Mama aiache CCM na ahamie CHADEMA kwa madai kuwa CCM haijamsaidia chochote zaidi ya kuendelea kumfanya masikini. Mama anakataa kuiacha CCM kwani yeye ni Mzalendo licha ya kuwa CCM haijamsaida.

Mtoto anaamini kuwa, kuichagua CCM ni kuchagua kuwa masikini. Hoja ya Mtoto inamashiko kwa kiasi kikubwa kwani ni kweli familia hiyo ni masikini.

Mtoto aliamini kuwa, CCM ndio imemfanya yeye asiendelee na shule. Hoja hii ni kweli kwa sababu ni kweli mtoto huyo alishindwa kupelekwa shule kwa sababu ya umasikini wa familia yao.

Mtoto aliamini kuwa, CCM ni adui wa maendeleo yake na maisha yake kwa ujumla. Hivyo anapoona Mama yake aliyemzaa akiungana na CCM Ambayo anaiona ni adui wa kwanza kwenye maisha yake, ni dalili kuwa Mama yake hana mapenzi na yeye.

Mtoto aliamini kuwa, CCM ndio imesababisha ndoto yake ya kusoma iyeyuke kama barafu. Hivyo Mama kuungana na CCM ni dalili ya Mama kutotaka mwanaye asisome.

Kwa Upande wa Mama, Yeye anaamini kuwa Kuwa CCM ni Uzalendo hata kama ni masikini. Mama anaamini kuwa umasikini ni moja ya sifa ya Uzalendo. Mama ni aina ya wale wafia dini wanaoamini kuwa tajiri hataenda mbinguni hivyo kuwa masikini ndio utakatifu. Au wale wasela wanaoamini kuwa mchafu ndio usela.

Mama anaamini kuwa CCM ni sifa hata kama CCM inakuletea madhara. Ni sawa na wale watu wanaovuta sigara kwa sifa wakidhani ni ujanja huku wakisahau uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya zao.

Mama kachagua umasikini unaosabaishwa na CCM. Huku Mtoto akiamua kuchagua kufa kuliko kuishi akiwa masikini anaoamini unasababishwa na CCM.

Matokeo yake; Mama kapoteza mtoto aliyemzaa mwenyewe, kisa CCM ambayo kamwe haijawahi na haitawahi kumsaidia.

Mama amesikika akilalamika kuwa ni kweli yeye ni masikini, Mama amesikika akilalamika kuwa ni kweli ameshindwa kuwasomesha watoto wake, na sababu anaijua. Hicho kinaweza kisimuumize, lakini maneno yake yanayoashiria kuumia zaidi ni haya: "Nimempoteza mwanagu kwa uzembe, nimeshindwa kumuokoa mwanangu niliyemzaa mwenyewe"

Mama anaonekana kujutia mambo kadhaa; Lakini kubwa zaidi ni kushindwa kujua na kuthamini hisia za mtoto wake aliyemzaa. Kushindwa kumuelewa mwanaye kile kinachomtatiza.

Mama anaumia kwa sababu ni kweli Ameshindwa kumsomesha mwanaye kisa umasikini ambao mwanaye anaamini umesababishwa na CCM.

Mama anamuona mwanaye ni shujaa na anamapenzi na yeye (mama) kwa sababu licha ya yeye kushindwa kumsomesha mtoto wake(kimsingi ni jukumu lake) lakini mwanaye hajamuachia lawama bali lawama amezipeleka kwa CCM kuwa ndio chanzo cha yeye kushindwa kumsomesha.

Mtoto angeweza kumuambia Mama yake ni mzembe, asiyeweza kulea(ambapo ni sahihi kabisa) lakini kwa upendo hakumhusha Mama yake ni kushindwa kumsomesha isipokuwa CCM.

Mtoto anamuona Mama yake kama mtu anayeshirikiana na CCM kusimamisha ndoto zake. Mama hili huenda mpaka sasa hajalijua, lakini analihisi.

FUNDISHO KUTOKA KWENYE MKASA HUU

Ni uzembe kwa mzazi kushindwa kumlea mtoto(Huu ni ukweli mchungu) Unashindwaje kumsomesha mtoto? Utasingizia umasikini, Sawa. Umasikini unasababishwa na nini, na nani? Alafu mtoto(ambaye umeshindwa kumlea kwa uzembe wako) anakuambia Mama/ Baba umeshindwa kunilea, kunisomesha, kuniachia urithi, kunipa maisha mazuri kwa sababu ya mtu au kikundi fulani unachokishabikia(CCM) alafu wewe unakuwa mkali, au huelewi. Unafikiri mtoto ataonaje; Ni wazi atajua umefanya makusudi kutomsomesha, umefanya makusudi kutomuachia urithi, umefanya makusudi kutompa maisha mazuri.

Kwenye maisha, Mambo mawili ndio yanaweza mfanya mtu kuwa Masikini kwa asilimia 90%. Mambo hayo ni;

1. Wazazi
2. Serikali

1. Wazazi
Ukizaliwa na wazazi masikini, wazembe, wajinga, upo uwezekano wa 90% ya wewe kuwa masikini. Ukitaka kubisha bisha. Lakini huo ndio ukweli. Ushaambiwa Ng'ombe wa masikini hazai, na akizaa hufa.

10% Iliyobaki ndio wachache hubahatisha kuwa na pesa na maisha mazuri. Na ipo hivi kama umetokea kwenye familia masikini ukabahatisha kuwa na pesa basi uwezekano wa wewe kufa kabla ya kufikisha miaka 60 ni asilimia 90%. Wengi hufa mapema zaidi ya hapo. Unajua kwa nini? hilo tutalisema wakati mwingine. Ila ipo hivyo, watoto waliobahatisha kufanikiwa kwenye familia zao zilizomasikini hufa mapema(nawe waweza kuwa shahidi).

Hii ni tofauti na familia tajiri ambapo watoto wao zaidi ya asilimia 90% hufika miaka 70 kuendelea. 10% hufa chini ya hapo. Unajua kwa nini? Hahahah! Tutalijadili hilo.

2. Serikali

Kwa asilimia 75% Serikali ndio husababisha jamii yake kuwa masikini. Ukubali au ukatae. Ukiona jamii fulani ni masikini kupitiliza basi tambua kuwa Serikali ya jamii hiyo ndio chanzo cha umasikini. Serikali huzalisha umasikini au utajiri. Serikali nyingi za nchi masikini. Hazijioni kama ni wajibu wao kufanya jamii zao kuwa tajiri, bali zinaona ni wajibu wa jamii zao(watu) kuwatoa pesa ili viongozi waishi maisha mazuri.

Ukijiona wewe ni masikini, basi tambua serikali na wazazi wako ndio wameamua kuwa hivyo ulivyo. 10% (exceptional) hawa hawategemei wazazi au serikali. Wao hata serikali iwaandame vipi lazima wawe na maisha mazuri, Hawa hata wazazi wawalaani vipi ni lazima wawe na pesa.

Serikali za nchi masikini, zikishaona baadhi ya watu wake wanaanza kutajirika, badala ya kuwasaidia wazidi kupata pesa ili wasaidie wengine. Serikali huwaandama na kutafuta namna ya kuzichukua pesa zao ili kujineemesha wao(viongozi wenyewe) na mwishowe mtu hufilisika na kurudi chini zaidi.

Embu angalia mtu akistaafu jinsi atakavyozungushwa kulipwa mafao yake. Wengine humaliza miaka miwili kuhangaika wakizungushwa na watu wa serikali wasiowaaminifu.

Embu angalia mfanyakazi anapokufa alafu jinsi ilivyokuwa tabu kufuatilia mirathi ya mume/mke. Utazungushwa huku ukipoteza pesa za nauli, chakula, na muda wako hata miaka miwili mitatu.

Hii yote ni kwa sababu serikali za nchi masikini nyingi hudhamiria kwa makusudi watu wake wawe masikini na viongozi wazidi kuneemeka.

Wewe uliona wapi Wabunge wakifuatilia mafao yao miaka nenda rudi. Uliona wapi mawaziri wakihangaishwa, uliona wapi?

Huyu mtoto aliyejiua, kama wazazi wake wangekuwa na maisha mazuri asingediriki hata kusema habari za CCM kwani anaona ni kweli Uwepo wa CCM unamnufaisha Mama yake na yeye pia.

Sasa wewe mwenzangu na miye Mzazi;

Hujasomesha watoto, bado unalia CCM
Hujaacha urithi wa watoto, bado unalia CCM
Hujajenga nyumba wala huna kiwanja, bado unalia CCM
Mustakabali wa uzee wako hujui utaishije, bado unalia CCM
Mustakabali wa watoto wako huujui, bado unalia CCM
Watoto wako hawavai vizuri, bado unalia na CCM
Kizazi chako sio bora, bado unalia na CCM.

CCM inamiaka 59, mpaka sasa ati ukoo wenu wote hakuna mwenye maendeleo ya maana.
CCM inamiaka 59, ukoo wenu mwenye degree ni mmoja tena usikute hakuna hata mmoja.
CCM inamiaka 59, Ukoo wenu wote hakuna aliyewahi kupanda hata ndege.
CCM inamiaka 59, ukoo wenu hakuna mwenye gari hata la milioni 2
CCM inamiaka 59, hakuna mwenye nyumba ya kisasa, tena wenye nazo hata hizo za banda umiza hawazidi wawili.

Kila miaka mitano unadanganywa kuwa maendeleo yatakuja, maendeleo hayooo! Wewe na familia yako mnaishia kufa masikini.

Anayeishabikia CCM hana tofauti na waumini wanaoenda kanisani; Mchungaji akitaka kununua Gari waumini wanamchangia, lakini Muumini akitaka gari badala achangiwe yeye anaombewa. Waumini wenye akili wangemwambia Mchungaji kuwa subiri nasi tukuombee ili upate gari kwa maana ukiwa na imani Mungu atakupa Gari.

Sasa washabiki wa CCM wao wanaaminishwa kuwa wataletewa maendeleo kesho, wakati viongozi wanajipa maendeleo leo. Hahahahah! Dunia inavioja sana.

Niishie hapa, maana nikisema sana, wenye nacho wataniambia ninawashtua wapumbavu hivyo wataosa ulaji.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es Salaam
 
Sasa wewe mwenzangu na miye Mzazi;

Hujasomesha watoto, bado unalia CCM
Hujaacha urithi wa watoto, bado unalia CCM

Hujajenga nyumba wala huna kiwanja, bado unalia CCM

Mustakabali wa uzee wako hujui utaishije, bado unalia CCM

Mustakabali wa watoto wako huujui, bado unalia CCM

Watoto wako hawavai vizuri, bado unalia na CCM

Kizazi chako sio bora, bado unalia na CCM.
 
CCM inamiaka 59, mpaka sasa ati ukoo wenu wote hakuna mwenye maendeleo ya maana.

CCM inamiaka 59, ukoo wenu mwenye degree ni mmoja tena usikute hakuna hata mmoja.

CCM inamiaka 59, Ukoo wenu wote hakuna aliyewahi kupanda hata ndege.
CCM inamiaka 59, ukoo wenu hakuna mwenye gari hata la milioni 2
CCM inamiaka 59, hakuna mwenye nyumba ya kisasa, tena wenye nazo hata hizo za banda umiza hawazidi wawili.
 
Serikali za nchi masikini, zikishaona baadhi ya watu wake wanaanza kutajirika, badala ya kuwasaidia wazidi kupata pesa ili wasaidie wengine. Serikali huwaandama na kutafuta namna ya kuzichukua pesa zao ili kujineemesha wao(viongozi wenyewe) na mwishowe mtu hufilisika na kurudi chini zaidi.

Embu angalia mtu akistaafu jinsi atakavyozungushwa kulipwa mafao yake. Wengine humaliza miaka miwili kuhangaika wakizungushwa na watu wa serikali wasiowaaminifu.

Embu angalia mfanyakazi anapokufa alafu jinsi ilivyokuwa tabu kufuatilia mirathi ya mume/mke. Utazungushwa huku ukipoteza pesa za nauli, chakula, na muda wako hata miaka miwili mitatu.
 
Back
Top Bottom