Mama akataa zawadi ya gari kutoka kwa mwanawe, adai 'hili ni Jeneza', amshutumu kwa Freemason

Mama akataa zawadi ya gari kutoka kwa mwanawe, adai 'hili ni Jeneza', amshutumu kwa Freemason

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwanamke mmoja ambaye anadaiwa kuwa ni Mama wa msanii wa muziki Bongo, Hamisi 'Tajiri Chui' Mwelemi amekataa gari jipya alilopewa na mwanawe huyo, akidai kuwa zawadi hiyo inahusiana na shughuli za Freemason.

Akiwa na msimamo mkali, mama huyo alidai gari hilo "ni jeneza" na kuonya kuwa hataki kushiriki lolote linalohusiana na imani au makundi yasiyoeleweka.

IMG_2195.jpeg
 
Mda ukifika, atatolewa kafara kama kawaida, hata asipopanda hilo gari.. 🤒🤒
 
Kwanza ilikuwa simfahamu huyu msanii nadhani katumia njia hii kujulikana. Sasa kama mama kakataa zawadi kulikuwa na haja gani ya kutangazia uma, mbona ni wazazi wengi tu huwa wanakataa zawadi zetu na tupo kimya hatutangazi.
 
Yale matapeli yanayodai kuunganisha watu na ufreemason yameharibu akili za watu. Zile picha za maburunguti ya hela, majumba na magari zimewaaminisha watu kuwa huo utajiri wanatoa wao. Ikitokea kijana kapambana wee akapata gari au jumba watasema tayari amejiunga freemason, ataanza kuogopwa na ndugu zake kwa dhana kwamba watatolewa kafara. Kumbe hakuna kitu wala freemason hawahusiki, huko ni kutokujua dhana ya freemason in and out
 
Wale wapuuzi walioanza kuisema vibaya Freemason miaka ya 90's na 2000 mwanzoni wameharibu sana watu
Hasa kwenye jamii za wajinga Tanzania hii hata uwaambieje hawatakuelewa kuhusu freemason.
 
Back
Top Bottom