Etugrul Bey
JF-Expert Member
- Aug 6, 2020
- 6,514
- 15,247
Dukani kwa Mangi nakutana na kijana mmoja barobaro hivi,anamwambia Mangi nipimie maharage,karanga, njugu mawe na nafaka nyingine mbali mbali huku anaendelea kuangalia orodha ambayo ametumiwa na mzazi mwenzake,ilikuwa na maandalizi ya kutengeneza unga WA lishe WA mtoto wao.
Kilichonipeleka Kwa Mangi ni kutuma hela sehemu kwahiyo nikiwa katika kusubiri nihudumiwe nikabahatika kupata mawili matatu.
Kijana akasema hawa watoto ambao tunawahudumia na Kula vizuri mara nyingi huwa Wajinga Wajinga Sana,tofauti na watoto ambao wanakulia katika shida Sana.
Kwa kawaida huwa napenda ukweli kwahiyo ikabidi nimuweke Sawa bwana mdogo Kwa kumuuliza,je hayo mambo umesikia wapi kuwa mtoto akila vizur anakuwa mjinga mjinga?
Akajibu huyu bwana mdogo kwakusema " unajua bro Sisi ambao tumekulia kwenye shida sio Wajinga Wajinga kama watoto wa siku hizi"
Nikamwambia hapana ujinga unatokana na malezi na si Kula vizuri ,kila mtoto anastahili Kula vizuri kwani ni msingi WA afya Bora.
Pembeni yetu alikuwepo mrembo mmoja amejistiri Kwa kuvalia baibui jeusi pamoja na mtandio wake kichwani,Akaona isiwe tabu ngoja nae achangie chochote.
Yule mrembo akasema "kwakuwa ulikulia kwenye shida haimaanishi na mwanao pia akulie kwenye shida,mbona Sisi zamani tulikuwa tunaenda shule hatupewi hela yoyote ya kula tunaenda na tunarudi lakini siku hizi watoto wetu hata WA primary lazima utampa walau shilingi Mia tano kila siku"
Kijana baro baro akaona isiwe tabu akafungua code;
" Mimi bwana nimeishi Kwa shida Sana,mama yangu amenilea yeye Peke yake,na kila nilipo muuliza kuhusu Baba yangu,aliniambia Baba yako amekufa"
Aliendele kijana kusema "kila nilipokuwa namuuliza mama yangu anionyeshe Baba yangu alikuwa ananijibu Baba yako amekufa,basi ikabidi niamini hivyo Tu,kwahiyo mama ndio alipambana na kunilea Kwa shida Sana. Lakini nilipo fikia kidato cha nne nilikuja kukutana na Baba yangu mzazi,na tunaenda Sawa vizuri mpaka Leo"
Nikamuuliza je Baba yako alikwambia nini kuhusu kutowajibika kwake kukulea mpaka umekuwa kijana mkubwa Tu? Kijana akasema Baba aliniambia kuwa upande wa mama ndio walizingua na hawakutaka kumuona kabisa.
Nikamwambia anyways huenda anajitetea Tu au anasema ukweli,lakini mwisho wa siku ukweli wanaujua wazazi wako.
Mimi na Yule mrembo aliyevaa baibui jeusi tukamwambia unafanya vizuri kumhudumia mwanao,kwakuwa wewe uliishi Kwa shida haimaanishi pia mwanao naye anapaswa kuishi Kwa shida,badilisha iyo ciycle na mtunze mwanao Kwa nguvu zako na mapenzi yako yote.
Mimi na mrembo Yule kila mtu akaondoka na kumwacha kijana anakusanya mazagazaga yake.
Ni hayo Tu.