Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Mkazi wa Kijijii cha Namanjele mkoani Mtwara, Somoe Mohamed amemchoma mikono mtoto wake mwenye umri wa miaka mitano kwa madai ya kudokoa mboga na kuiba sh. 250.
Akizungumza na Mwananchi kijijini hapo leo Oktoba 4, Somoe amekiri kufanya ukatili huo, akisema lengo lake lilikuwa ni kumwadhibu mtoto kwa tabia mbaya aliyoonyesha.
"Nilikuwa namwadhibu kwa tabia yake. Siku ya kwanza alichukua sh. 50 na siku ya pili alichukua sh. 200 na baadaye akaanza kudokoa dagaa nikamuonya, lakini hakusikia mpaka sasa mtoto anasiku tatu tangia amechomwa moto,” amesema.
Baba wa mtoto huyo, Juma Lubega amesema kuwa yeye alisikia kuwa mwanaye amechomwa moto na mama yake hakuamini, lakini alipofika nyumbani alimuona mtoto akiwa ameungua sehemu ya mikono yake vikiwemo vidole.
“Nilisikia uchungu kama baba nilipouliza nikaamibiwa kuwa kaiba sh. 250 na kudokoa dagaa, yaani inaonyesha kuwa alimfunga kamba mikononi akaweka nyasi akamchoma mtoto na inaonyesha alipowasha moto aliondoka ndio maana mtoto amepata madhara makubwa,” amesema Lubega.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa kijiji hicho, Mussa Mkadimba amesema kuwa tukio hilo siyo zuri kwakuwa halifundishi mtoto bali linaweza kumfanya akawa katili.
“Nimelipokea vibaya hili jambo kwakuwa halikuletwa kwangu, nilisikia niliamua kulifatilia mwenyewe ili kuona kuna ukweli kiasi gani nikakuta ni kweli mtoto ameunguzwa na moto kwa maeneo ya mikono yake.
“Huyu mtoto tangia uchomwe hajapelekwa hosptiali yoyote wala hajapata dawa zaidi ya miti shamba wanayotumia kumuwekea mikononi, kutokana na imaini kuwa atapona kwakutumia dawa za asili,” amesema.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, ACP Nicodemus Katembo alipoulizwa na Mwananchi kuhusu tukio hilo alisema kuwa yuko safarini na akifika atalifatilia na kulitolea maelezo.
Chanzo: Mwananchi