Mama Diamond aeleza alivyomdunda Mobeto

Mama Diamond aeleza alivyomdunda Mobeto

don88

Member
Joined
Jan 22, 2013
Posts
53
Reaction score
84
Eti aeleza alivyomvua wigi na kumtupia viatu nje Madale, asema anamchukia ile mbaya ch akuchekesha sasa eti amemsifia Zari.

Ubuyu wa moto moto unasema kuwa baada ya kuvuma kwa taarifa mitandaoni kuwa mama wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kassim ‘Sandra’ amempa ‘vitasa’ mwanamitindo Hamisa Mobeto, Ijumaa limemtafuta bi mkubwa huyo na kufanya naye mahojiano maalum (exclusive) ambapo amefungukia sakata hilo kwa kirefu.

Mama Diamond alifungukia hilo la kumpiga Mobeto ambaye amezaa mtoto mmoja na mwanaye, Jumanne iliyopita katika mahojiano maalum yaliyofanyika katika duka la bintiye, Esma Khan ‘Esma Platnumz’ lililopo maeneo ya Afrika Sana jijini Dar.

ISHU ILIPOANZIA

Mama Diamond alisema ishu hiyo ilianzia Mei 13, mwaka huu mara baada ya yeye pamoja na Diamond kutoka kwenye shoo ya msanii wa Kundi la Wasafi Classic Baby (WCB), Mbosso.

Alisema, kwa kuwa walirudi nyumbani kwao Madale usiku, yeye alilala katika chumba chake bila kujua Diamond amelala na Mobeto chumbani kwake.

KULIPOPAMBAZUKA

Bi mkubwa huyo alisema, kulipopambazuka, alikwenda kwenye mishemishe zake na aliporejea ndipo alipoliamsha dude baada ya kushtukia mrembo huyo amelala nyumbani hapo.

Mama Diamond: Hayo mambo ya mzazi mwenzie ni huko, pale Madale ni kwangu na simtaki nyumbani kwangu kabisa.

Gazeti la Ijumaa: Kuna kosa lolote alishawahi kufanya kwako labda?

Mama Diamond: Kitendo cha kuniitia mimi Shilawadu (kipindi cha udaku cha Televisheni ya Clouds) kilinikera sana halafu nikaanza kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii.

KWA NINI KILIMUUMA?

Kwa muda mrefu mashabiki wa ubuyu Bongo walikuwa hawajui kiini cha ugomvi wa mama Diamond na Mobeto lakini sasa ameweka bayana.

Iko hivi, mapema mwaka jana, wakati Hamisa alipokuwa amenasa ujauzito wa Diamond ambaye wakati huo alikuwa kwenye uhusiano mzito na Zari, walikubaliana kufanya siri jambo hilo ili Zari asiusome mchezo.

Mama Diamond inaonekana alikuwa kwenye huo ‘mpango mkakati’ wa kuficha ujauzito wa Mobeto hivyo kitendo cha kuwaita Shilawadu wamshuti alipokwenda kumuona hospitalini wakati Mobeto alipojifungua ndicho kilichomkera zaidi mzazi huyo.

Baada ya habari za Diamond kutembea na Mobeto kuvuma chini kwa chini kwa muda mrefu, kupitia vipande video vilivyorushwa na Shilawadu, vilimfanya Zari athibitishie pasi na shaka kwamba kweli Mobeto amezaa na Diamond.

TUENDELEE NA MAHOJIANO…

Gazeti la Ijumaa: Sasa inawezekana alishajua kosa lake ameamua kujirudi mama, huoni kama unapaswa kumsamehe?

Mama Diamond: Yaani kiufupi simpendi na simtaki na kila akikanyaga hapa kwangu ni kipigo tu.

Gazeti la Ijumaa: Kuna mtu yeyote alikutonya kuwa Mobeto yuko ndani siku ya tukio?

Mama Diamond: Ni kama zari tu. Mimi nafikiri kama mganga wake kamtuma aje anijaribu afike tena kwangu aone kama sitomfanya kitu kibaya.

Gazeti la Ijumaa: Kwa sababu gani lakini umfanyie kitu mbaya kwani kulala na Diamond ni kosa?

Mama Diamond: Alipokuja kiwizi usiku ule na kulala nyumbani kwangu, alipaswa kuondoka kabla sijamuona kwa nini alisubiri mimi nimkute maana siku hiyo asubuhi yake nilitoka na nilivyorudi ndipo nikamkuta.

Gazeti la Ijumaa: Ulivyomkuta ikawaje?

Mama Diamond: Mimi nilimsubiri tu getini na nilishajiapiza lazima nimpige.

Gazeti la Ijumaa: Sasa varangati lote Diamond alikuwa wapi?

Mama Diamond: Yupo na yeye ndiyo alimsaidia kumuamulia mimi nikabaki na wigi la sivyo ingekuwa shida.

Gazeti la Ijumaa: Kwa hiyo baada ya kubaki na wigi yeye alifanyaje?

Mama Diamond: Alikimbia na viatu mkononi, maana nilikuwa nimeshavitupa nje ya nyumba yangu.

Gazeti la Ijumaa: Kuna sababu nyingine kubwa ya kumchukia Mobeto?

Mama Diamond: Kwanza tu siyo mwanamke wa kuoa (wife material) hajui kutandika hata kitanda wala kufanya tu usafi ni shida.

Gazeti la Ijumaa: Ulimuona wapi mama hawezi kufanya hivyo vitu?

Mama Diamond: Si alishakaa hapa kipindi nipo Kigoma nilivyorudi ndani hakutamaniki kabisa.

Gazeti la Ijumaa: Lakini sasa huoni kama inaweza kuwa ni tatizo maana unaweza ukawa unamchukia lakini Diamond ndiyo kafika pale na ndio mtarajiwa wake?

Mama Diamond: Yaani atajua yeye mwenyewe maana mimi ndiyo nimemzaa Diamond na siyo yeye sasa sijui nani ana nguvu hapo.

Gazeti la Ijumaa: Je, Diamond akiamua leo kufumba macho na kumuoa Mobeto itakuwaje?

Mama Diamond: Siwezi kukanyaga kwenye hiyo harusi hata siku moja watasherekea wenyewe.

Gazeti la Ijumaa: Lakini pia si kuna madai wewe na mama Mobeto mlikuwa marafiki sana sasa kwa nini msilimalize hili kiutu uzima?

Mama Diamond: Hatujawahi kuwa marafiki hata siku moja maana mama Mobeto mwenyewe nilimuona kwenye bethidei yangu mara moja tu, hatuna uhusiano wowote kwanza mimi sina marafiki.

Gazeti la Ijumaa: Unaonekana unaposti sana picha za wajukuu zako ambao ni watoto wa Zari, unamzungumziaje Zari?

Mama Diamond: Ninamheshimu Zari kwa sababu ni mwanamke ambaye ndiyo wa kwanza kabisa kumfanya mwanangu aitwe baba.

Note: Ubuyu kamili upo huko facebook kwenye page ya Ijumaa.

Source: Page ya Gazeti la Ijumaa/facebook

Gazeti la Ijumaa
 

Attachments

  • Capture.PNG
    Capture.PNG
    52.7 KB · Views: 131
  • diamond-na-mama-yeke.jpg
    diamond-na-mama-yeke.jpg
    45.6 KB · Views: 173
  • wp-1468184079920-660x400.jpg
    wp-1468184079920-660x400.jpg
    33.2 KB · Views: 149
[emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23] [emoji23] [emoji23][emoji23] [emoji23] [emoji23] hii movie tamu jaman. Tununu usiachieeee shikilia hapo hapo tusikose ubuyu akina sieeee

Enzi za kigoma hatoki boiii kumbeee tununu alikua anaishi madale mujini kutamu

[emoji125] [emoji125] [emoji125] ngoja nikamshtue zari abatize akina tiffa drama ziishe
 
Ben10 anaonekana hamkazii vizuri uyu bi mdashi maana hatulii kabisa angeingia kwenye 18 zangu muda huu Diamond anategemea kupata mdogo wake.
 
Hahahaaaa!!hatari tupuu!![emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]nimecheka kama mazuri
 
Leo Hamisa mchafu,hajui kutandika kitandaa!saafi sanaa...kakukomeshaa...[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]ulimuona Zari hafai ukamtafutia mchepuko kiko wapi sasa?

Bibi hiyo ndo Karma pambana na gubu lakoo!

Bi Sandra usipoangalia mwanao hataoa kokote maana kila mkwe mbaya,nakumbuka ushasemaga Wema mvivu,Zari anaongea kingereza ana dharau,Hamisa mchafu[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] wacha wake wakukomeshee

Mama una gubu balaaq
 
Back
Top Bottom