Mama Fatma Karume ashangazwa Makonda kuondolewa mkuu wa mkoa

Mama Fatma Karume ashangazwa Makonda kuondolewa mkuu wa mkoa

Anachoweza Makonda ni kufanya uwekezaji wa kujipendekeza kwa watu sahihi.

Akifanikiwa kupata nafasi sio humble kabisa ni madharau na kejeli hata kwa viongozi wake.

Mgeni rasmi hapo Dr Nchimbi, kwa raia (average Tanzanians) mpaka leo ni mtu wa wakawaida tu, labda sasa hivi ulinzi umeongezeka.

Sio Makonda yaani anajionaga mtu fulani hivi very special mbele ya mungu na serikalini, wakati hana lolote zaidi ya kujua kujipendekeza tu.
 
Mke wa Rais wa Kwanza wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Abeid Karume, Mama Fatma Karume amesema amepokea kwa mshtuko taarifa ya mabadiliko ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan Juni 23, 2025, hususan kuondolewa Paul Makonda kama Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Akizungumza leo Juni 24, 2025 katika Jukwaa la Wanawake lililofanyika jijini Arusha, Fatma amesema;

“Nilishtuka sana… mmh basi, lakini mwanasiasa ni mwanasiasa tu. Nikapata habari nikawaambia nikakumbuka pia, hayo yapo… lakini nataka niseme neno moja, sijui ni siri? (akiimba) Tunae na Makonda tunae mkoa huu… na koti tutamvika… tutampeleka kwingine atusemee mkoa huu,” amesema huku ukumbini washiriki wakiangua vicheko.

Soma,pia: Mama Fatma Karume amtembelea RC Makonda, aongoza dua nzito kumuombea kheri
View attachment 3381401
Chanzo: Mwananchi​
Mmh huu uchawa, nafasi ya ukuu wa mkoa ni nafasi ya uteuzi wa rais, muda wowote aweza ondolewa
 
1905-2025= 120 .

Kama Abeid Aman karume angekuwa hai angekuwa na miaka 120

Najiuliza huyo mke wake walipishana miaka mingapi ??? Au alioa mwanamke ambaye ni sawa na mtoto wake
 
TAIFA liko mikononi mwa mashangingi na waimba mipasho. Unategemea nn?
KAZI ni kipimo cha utu
 
Ni sawa lengo ni kujipanga na kutafuta Jimbo la uchaguzi, kwa ajili ya kugombea Ubunge kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
Back
Top Bottom