Mama Hamisa asema anataka mwanae aolewe na Mzungu, Waafrika hawafai

View attachment 747024

Mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema katika maisha yake alikuwa anamuombea mtoto wake huyo aolewe na mzungu.

Akizungumza na MCL Digital, Shufaa amesema sababu ya kutaka aolewe na mtu wa aina hiyo ni kutokana na wanaume wa kiafrika kutokuwa na mapenzi ya kweli.

“Unajua mtoto wangu ni mzuri, mrefu ana shingo nzuri nataka mwanaume atakayemuoa amuangalie kama malaika, kama malkia kwa kuwa ni mwanamke mwenye misimamo yake na ametulia sio muhuni kama watu wanavyomfikia.

“Wazungu hawana ‘stress’ wanajua namna ya kujali mwanamke, hawanaga mambo ya longolongo linapokuja suala zima la mapenzi tofauti na wanaume wetu wa kiafrika,”amesema.

Kuhusu suala la kuzaa na wanaume tofauti, mama Hamisa amesema hilo kwake halimpi shida na angependa amletee wajukuu wengi zaidi kwa kuwa yeye alijaliwa kumzaa peke yake na kudai kwamba hao ndio ndugu zake.

Ni kutokana na hilo, amesema anatamani amzalie watoto sita, kwa kuwa sasa hivi ana nguvu za kulea wajukuu zake na siku hayupo duniani hao ndio watakuwa ndugu zake na kuweza kumsaidia.

Mpaka sasa Hamisa ana watoto wawili.

Chanzo: Mwananchi
Mama ameshatembea na waafrika wangap mpaka kufikia kusema wanalongolingo bara nzima, ameshatembea na wazungu wangap na wa nchi zip ambao wamempa ukaki juu ya swala la mapnz kwao?dah mkataa kwao....
 
Huyu Mama ana IQ ndogo sana, bila shaka alitumika sana
 
View attachment 747024

Mama wa mwanamitindo, Hamisa Mobeto, Shufaa Rutiginga amesema katika maisha yake alikuwa anamuombea mtoto wake huyo aolewe na mzungu.

Akizungumza na MCL Digital, Shufaa amesema sababu ya kutaka aolewe na mtu wa aina hiyo ni kutokana na wanaume wa kiafrika kutokuwa na mapenzi ya kweli.

“Unajua mtoto wangu ni mzuri, mrefu ana shingo nzuri nataka mwanaume atakayemuoa amuangalie kama malaika, kama malkia kwa kuwa ni mwanamke mwenye misimamo yake na ametulia sio muhuni kama watu wanavyomfikia.

“Wazungu hawana ‘stress’ wanajua namna ya kujali mwanamke, hawanaga mambo ya longolongo linapokuja suala zima la mapenzi tofauti na wanaume wetu wa kiafrika,”amesema.

Kuhusu suala la kuzaa na wanaume tofauti, mama Hamisa amesema hilo kwake halimpi shida na angependa amletee wajukuu wengi zaidi kwa kuwa yeye alijaliwa kumzaa peke yake na kudai kwamba hao ndio ndugu zake.

Ni kutokana na hilo, amesema anatamani amzalie watoto sita, kwa kuwa sasa hivi ana nguvu za kulea wajukuu zake na siku hayupo duniani hao ndio watakuwa ndugu zake na kuweza kumsaidia.

Mpaka sasa Hamisa ana watoto wawili.

Chanzo: Mwananchi
Duh.! Kumbe haka kasichana kana watoto wawili!
 
ulimbukeni unamsumbua mbona, wabongo tunaendekeza ulimbukeni wa kutukuza rangi nyeupe ka wao ndo wako perfect kwakila jambo.
 
Kweli, wazungu wanapenda wanawake waliozaazaa ma wanaume wengi, hasa micharuko inayopenda mabwana yenye pesa...
Mama mcharuko, mtoto mcharuko, tuwaombee wajukuu tu..
Tizama tabia za bibi zao, mama yao na baba yao =wajukuu sijui watakuweje
 
Kwa hiyo anahamasisha utengano kati ya mwanae na Mondi
 
Back
Top Bottom