Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Usithubutu kumuamini. Watu wasanii kwenye kutaka kufanikisha mambo yao. Usimlie yamini mlevi anayesema anafanyia kazi ulevi wake kwa ajili yako.
ni kweli ila sio kwamba ndio nmeingia kichwa kichwa tatizo nataka kuenjoy moment(when there is peace in the jungle, you gotta enjoy the quiet )
itakapoishia basi hamna neno tukishindwana ila hata hilo linashindikana kwa maneno ya bi mkubwa
 
Na hivyo vitu sio kivile, pombe ameacha tangu nimwambie mi pia staki hivyo vitu akishindwa kuacha tutakua tu casual amenielewa anayafanyia kazi hayo

ukimuuliza anasema umemtukana
sio kivile ndio jibu gani sasa? kwenye nyeusi weka nyeusi si habari ya kijivu,kama anakimbiza mwenge na kunjwa pombe msikilize mama.
 
Miezi mitatu michache sana...Kaa naye hata mwaka huweza utagundua dosari anazoeleza mama yako..
.halafu unataka kuolewa sababu nawe hujasoma na huna kazi? Hakuna kingine kinachowaunganisha zaidi ya hicho? Unamkubali sababu wapenzi wengine walikusumbua? Huna sababu nyingine? Nadhani mama ana point msikilize fanya uchunguzi.
 
Pole sana Mkuu

Isingekuwa heshima zetu kwa Wazazi ungeweza kumuuliza Bi Mkubwa kama nayeye alichaguliwa kuwa na Mzee wako au walipendana wenyewe [emoji848]

Anyways, Wanasema Wazazi wamewahi kuona jua kabla yetu, jaribu kumsikiliza pengine kuna jambo ameona kwa huyo Boyfriend wako
Ndo nilitakaa niseme mie amuulize huyo mama ake, yeye kuwa na baba ake alichaguliwa au kwa ridhaa yake, wala hakuna heshima kuvunjwa anapaswa kumuuliza.
 
-ana vuta bangi/pombe
Asiefunzwa na mamaye hufunzwa na Ulimwengu, aliemtanguliza kukuonyesha jua anakwambia achana na hii takataka umeng'ang'ania wembe ukishakukata unarudi tena kwa mama unakua ushajikata na wembe, mwanakulitafuta mwanakulipata endelea na huyo Kiranga komo yakikukuta usiseme hukuambiwa
Sasa hapo nifanyaje wakuu?
Msikilize mama yako ukiumwa maututi yeye ndie atakaekua anakupikia uji nyumbani na kukuletea hospitalinu sio hilo kulumbembe kashalistukia liweke pembeni wamama wanaona mbali usimdharau mama yako ipo siku utajuta utasema mama aliniambia Mimi
Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...
Juu nimesema umsikilize Mama Ila nilipofika hapa naomba umshirikishe mtu mwingine Shangazi, Mama mdogo au Mkubwa km wapo emu jaribu kuwashirikisha Jambo lako na wao waone je kweli mama yupo sahihi au kuna Jambo nyuma ya pazia ukiona na wao wanasema achana na huyu mtu aseee usibakize mda, watu wana macho na macho ya watu wanaona, haya mfikishe nilipokueleza nenda kwa Shangazi mwambie Shangazi nimemleta mwenzangu km utani tu ampigishe story amfahamu kidogo km kumpigisha interview ndogo kumjua na kumdadisi akitoka mpeleke kwa Mama mdogo au Mkubwa nae ampige interview ndogo amjue amdadisi kidogo, alafu wao wawili watacompare convo zao je anakufaa ikisoma NO hakufai asee usilazimishe utakutana na balaa la dunia huko mbele watu wana macho na macho hua yanaona mbali
nmepata feeling mama angu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..
maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama?
Wote kwa pamoja hili suala inabidi mshirikishe na watu wengine ndugu na jamàa ili mpate muafaka kua kweli jamaa anakufaa ama hakufai wao wataona km anakufaa au anapretend kwa muda mbele atakugeuka watamshtukia mapema tu unajua mapenzi na moyo wa mtu ni kichaka
 
Miezi mitatu michache sana...Kaa naye hata mwaka huweza utagundua dosari anazoeleza mama yako..
.halafu unataka kuolewa sababu nawe hujasoma na huna kazi? Hakuna kingine kinachowaunganisha zaidi ya hicho? Unamkubali sababu wapenzi wengine walikusumbua? Huna sababu nyingine? Nadhani mama ana point msikilize fanya uchunguzi.
mimi nataka kwanza mahusiano wala sina haraka ya ndoa, ni mama tu anapeleka mambo mbele
pia kinachofanya nimpende, ni upendo yeye amenipenda nimerudisha upendo na hio ni sheria yangu tangu zamani... amenionyesha upendo kipindi ambacho nimeuhitaji sana
 
Hata mimi nisingekuozesha yaani mwanaume an a kunywa pombe, bangi ,sigara mie hapana wanakuaga malaya mno

Afu pia wewe umeishia olevel na yeye olevel watoto wenu nani atawafundisha? Tafta hata mkaka mwenye diploma mtoto enu apate rolemodel awe inspired kusoma kwa bidii

Usitangulize hisia mbelembele
Wapo wavuta bangi na wanywa pombe si malaya. Umalaya ni hulka, wala haichochewi na vitu tajwa.

Swala la kuwafundisha watoto, wapo walimu watamsaidia. Tupo ambao wazazi wetu hawajui hata 'a' wala 'be' lakini walitusimamia kisawasawa.

Si vema sana kumkatalia mwanao kuolewa kwa sababu tajwa hapo juu. Kama kaacha bangi na pombe, basi yupo vizuri. Maisha ya kawaida si hitimisho. Watapambana watajenga yao.
 
Habari za saa hii wana Jf
Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-wote tumeishia 0- level kielimu
-anataka kunioa pale nikiridhia

sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- aliwahi kuishi na mwanamke
-anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- hana mvuto mbele za watu
-hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-hana hadhi ya kuwa na mimi
sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa
- mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...
Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...
nmepata feeling mama angu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..
maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.

ariana

Pole kwa hili, kinyamwezi wanaita dilemma.

Hata hivyo, ingawa vitabu vinasema waheshimu Baba na Mama, msisitizo ni kuwaheshimu kwenye kutenda righteousness (yanayompendeza Mungu).

Sasa basi, uchaguzi wako ni ima kuacha na kijana uambatane na Mama ama uachane na Mama kisha uambatane na kijana.

Mbili, kumbuka maisha ni kubahatisha maana hakuna aijuaye kesho.

Ushauri wangu, as long as mnapendana na kijana, nyie songeni mbele. Yakiwashinda mtaanza upya. Mapenzi hayalazimishwi wala mtu hachaguliwi wa kuambatana naye. Bible inasema mali na Fedha zinatoka kwa wazazi, mke/mume mwema ni biashara za Mungu hizo.

Kila la heri.
 
Back
Top Bottom