Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Hata mimi nisingekuozesha yaani mwanaume an a kunywa pombe, bangi ,sigara mie hapana wanakuaga malaya mno

Afu pia wewe umeishia olevel na yeye olevel watoto wenu nani atawafundisha? Tafta hata mkaka mwenye diploma mtoto enu awe inspired kusoma kwa bidii

Usitangulize hisia mbelembele
Ushauri wa hovyo
 
mbona vitu vya kawaida kuachana tumeachana na wangapi mpaka sasa

Usiweke akilini kwamba kuachana ni kawaida, find your mr perfect ili kuachana kusiwepo. Mama ni Mungu wa pili duniani kuna kitu ameona msikilize na jipe muda utapata mwanaume sahihi usilazimishe!
 
Kwa ulevi na sigara sawa ila kwa hayo mengineyo nakupinga.

Usijidanganye dear kumbuka muoaji ndio anajua anamuoa nani sio muolewaji. Si ajabu huyo kaka na utayari wake wote akipewa go ahead akapiga u turn Moja hiyo ikamuacha Dada wa watu kwenye maumivu makali na majuto.
Angalia na uhalisia
Nyie hamjui mwanaume mwenye akili timamu akiamua kuoa huwa katuliza kichwa
 
Pole sana binti.
Ila epuka sana ushauri unaopewa na single mother's wa humu, wengi walishaachika hivyo nia na kauli mbiu yao ni "Kataa Ndoa" maana hawapendi kuona binti akifanya kile walichoshindwa wao.
Hakuna binadamu asiyebadilika hata km itachukua muda gani na km ni makosa yalitokea yanaweza rekebishwa. Hii namaanisha huenda jamaa yako alishawahi mtongoza bi. Mkubwa wako kabla hajawa na wewe ndiyo maana kakaza. Muulize vzr bi. Mkubwa wakooo
 
kwasasa ni kama ameacha tangu nimkataze hajanywa na wala hakua mlevi ivyo ni mnywaji tu
- mama hakuchaguliwa baba
-ninae kaka angu ila hamfikii wa lolote kwenye kujituma mpaka maendeleo huyu jamaa yuko mbele sana
jamaa yeye amesema tumpe muda ajithibitishe kuwa ni sahihi na anajitahidi ila mama hamtaki
mpaka biashara anataka kunifungulia ila mama hataki
Jamaa boya umemshika masikio, umesema umemkataza pombe?

Na bado anaomba ajiprove na akufungulie biz ili tu mama amkubali, for what? huyu akikuoa baadae atakuboa na mama atakwambia nilikwambia.
 
Ukikutana na mazaangu sasa si ungechoka[emoji16][emoji16][emoji848]

Yaan nisingejipindua kukataa maushauri yake ningedoda[emoji38]

Kila mwanaume hamtaki sasa sijui alikuwa anamtaka Bill Gates [emoji848]
Princess anatakiwa kuwa bandidu sio mara zote wazazi wako sahihi
 
Na hapo yawezekana kijana keshalamba sukari ya mama so anakanya yai la kuku sema ndio hivyo mama anashindwa kumfungukia bint kwamba ni kiben teen chake kile kimeshamvua pichu
Mh sidhani km hili linawezekana
 
Pia wamama ambao hawajaolewa au wanaoishi kisingo Maza huwa hawapendi watoto wao kuolewa au kuwa na ndoa za amani au kama ndoa yake ilikua na matatizo.
Uko sahihi na wale ambao ni wajane au wana muda mrefu wameachika na hajapigwa mashine wanakuwaga na vigubu vya kijinga kinoma, wengi wao ni kuvuruga tu hawana jema kwao
 
Ndoa ni wewe na mwenzako; wazazi watakushauri tu, na si lazima kuchukua ushuri wao; ingawa mi kama mzazi nakuwa na matazamio fulani kuhusu maisha ya kijana wangu
 
Wamama wengine nuksi sana. Hapo jamaa angekua tajiri hata kama anakunywa hizo pombe na kuvuta bangi huyo mamako wala asingeona tatizo. Hapo inshu kubwa ni kwamba jamaa hana hela na mamako anataka upate bwana tajiri ili akamilishe yale ambayo yeye alishindwa kuyakamalisha enzi zake alipoolewa na babako maskini.
 
Sasa national,dada kasema hana kazi wala biashara na jamaa ndo hivyo mama mkwe anamkataa,akisema azae na jamaa huoni huyo mtoto anaweza pata shida ya matunzo baadae jamaa akichoshwa na drama za mama mkwe?
aisee, sikusoma vizuri. Ila mie binafsi simshauri bidada kuendelea na huyo brother. Kuishi na mtu kwa matarajio atabadirika mbeleni ni hatari sana .
 
Ana vuta bangi/pombe
Je ni kweli?
-Hajui kuvaa sio mtanashati
Katika maisha cha kuangalia ni 'Mindset' ya mhusika.

Je ana uwezo wa kuwa na familia?, Je ana uwezo wa kuhudumia familia?, Haya ni baadhi ya maswala ya msingi.

Na sio eti "mavazi" , "Mtanashati"
Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
Ye wewe mtazamo wako ni upi?

Je unaelewa maana ya "materialistic"
 
Yani anataka kunifungulia baishara nijipambanie hata kabla hajanioa
ila anamuogopa mama na mimi ndo mshika dau
ila watu hawajui, wanakazana kusema bangi ooh havutii
sasa leo mama anasema kwanza kwao kuna zezeta baba yao atakua mchawi yani sababu haziishi jamani [emoji119] asubuhi kaniumiza sana mana nilimwambia hao wanaosema hafai pamoja na wewe mnajua mpaka hapa nilipo nmekutana na mangapi??? mnajua ugumu nmepitia kihisia mnajua nmepambana kiasi gani kupata mtu mwenye spirit kama yake nyie mnachoona ni muonekano! mkaka wa watu kanifanya hata shida ndogo ndogo sina! anajitoa muhanga hasa
nmemwambia hao wanaonisema nikikaa home sijaolewa watasema pia ndo mana nmeona nichukue kilichobora kwangu ama ni enjoy wakati huu..
ila akacheka kwa dhihaka na kusema we mpumbavu sana wakati huo mimi naongea kwa machozi
nmeumia sana kuona hajali kabisa hata jinsi ananiumiza. hio picha haifutiki rohoni mwangu ndio ikanifanya nianzishe hii mada nmeumia sana

Aiseh!
Sema mama ako anaonekana ana matarajio makubwa sana juu yako
 
Msikilize mama ako asije kuwa mke mwenzako dunia ishakuwa duara hii, eneywy ila sio vyema kuolewa na mtu wa mtaani kwako tafuta wa mbali
 
Back
Top Bottom