Mama hamtaki Mpenzi wangu

Mama hamtaki Mpenzi wangu

Habari za saa hii wana Jf

Naomba msaada wenu wa mawazo juu ya swala hili, kama kichwa cha habari kinavyojieleza;
kwa miezi mi3 hii nmekua na mahusiano ya kimapenzi na kijana karibu na maeneo ninayoishi,
  • Mimi binti wa 28 yrs Mpenzi ana 38 aliwahi kuishi na mwanamke kwa miaka kadhaa zamani akaachana na mwanamke wake baada ya kuachishwa kazi ( kampuni ilifilisika)
  • Kwasasa ana biashara zake
-Wote tumeishia 0- level kielimu
-Anataka kunioa pale nikiridhia

Sasa tatizo linaanza baada ya mama kuhisi uhusiano baina yetu, anasema kijana hafai kwanza
-Ana vuta bangi/pombe
-Hajui kuvaa sio mtanashati
- Aliwahi kuishi na mwanamke
-Anatoka familia ya kawaida kama yetu kwahiyo hafai hatanisaidia chochote
- Hana mvuto mbele za watu
-Hana Cv nzuri hata nikimtambulisha
- Anahisi kaniroga ndo mana nmekua nae kimahusiano
-Kwanza anakaa maeneo ya karibu na nyumbani
-Hana hadhi ya kuwa na mimi

Sababu ni nyingi!!

Kwa kuliona hilo tukaamua basi ahame makazi tayari kashahama, mazingira yote tumeyafanya yawe mapya,kwa kila kitu cha hadhu anayoitaka mama,nmeshambadilisha huo muonekano kwa kiasi chake ili afanane na anavyotaka mama ila naona pamoja na kutaka aridhike ila kila siku anaanzisha sababu mpya ya kumkataa anasema anajitutumua tu ili anipate na pombe ameacha anipate akishanioa ntapata shida mana atarudi kwenye mambo yake yote!! Pia namdhalilisha kwa wamama wenzie kwa kuwa na mahusiano na jamaa

- Mama anasema yuko tayari kwenda kwa mganga yoyote akavunje mahusiano mana kwanza jamaa atakua kaniroga sio kawaida.

Sasa hapo nifanyaje wakuu? Maana naona nachanganyikiwa kila siku anaanzisha jambo jipya! ilihali nmemwambia mimi mwenyewe sijasoma! Kazi sina wala bishara yoyote na kijana wa watu ameridhia ana fanya kila jukumu lake bila kinyongo ila mama anasema anafanya mana hana hadhi ya kuwa na ww ndo mana inabidi afanye tu...

Kinachoniumiza ni hakuna siku amewahi niuliza changamoto za maisha yangu ya mahusiano. nmejaribu kumwambia wachumba wakija wakijua sijasoma/sina kazi wanagairi haelewi.. anasema umerogwa wewe
nikiomba space nitulize kichwa sipewi naambiwa mpaka utanielewa...

Nimepata feeling mama yangu ni Toxic /narcissistic mom ila nikieleza hisia zangu yeye ana cheka ndo ananiona kama mpuuzi..

Maana mimi nmemwambia kwanini tusimwachie Mungu tu kama Mungu hajapanga tutaachana tu ila kwa ridhaa yetu mengine tutarekebishana sitaki uwe kama unanipangia maisha ila haelewi kabisa , niko njia panda maana maisha nayaona machungu kabisa ni mimi ndo tatizo au mama? Nishaurini wakubwa kabla sijashuka presha nikazimika mana bi mkubwa kasema kama ntakufa nife mana ndo ilivyopangwa.
mama atakuwa na sababu. Huenda naye alishapitiwa na huyo jamaa na hawezi kukwambia.

Sent from my SM-A515F using JamiiForums mobile app
 
Nadhani umalaya ni nature/tabia ya mtu binafsi. Maana wapo wasio walevi au wavitaji, ila ni Malaya first grade.



Wapo wazazi ambao hawakusoma, ila watoto wao walifika mbali kielimu, ndio maana kuna shule na tuition. Wazazi wanatakiwa wawe committed kuhakikisha watoto wanapata elimu.


Huwa nadhani sisi wanaume ndio huwa tunatafuta wenzi, na nyie wadada mnatafutwa. Ana umri wa miaka 28, ameshasema wenye elimu wanamkataa, tokea akiwa early 20's. Soon at turn 30, then awe more stressed and depressed. Think like a woman in this.

Alaf kingine, elimu inawafanya watoto wapate roles model tofauti tofauti. Kati ya watoto 10, unaweza usipate hata mmoja atakayekwambia role model wake ni baba/mama yake.


Mapenzi ni hisia, why asitangulize hisia mbele?
That's my dogo[emoji11]

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Pole sana binti.
Ila epuka sana ushauri unaopewa na single mother's wa humu, wengi walishaachika hivyo nia na kauli mbiu yao ni "Kataa Ndoa" maana hawapendi kuona binti akifanya kile walichoshindwa wao.
Hakuna binadamu asiyebadilika hata km itachukua muda gani na km ni makosa yalitokea yanaweza rekebishwa. Hii namaanisha huenda jamaa yako alishawahi mtongoza bi. Mkubwa wako kabla hajawa na wewe ndiyo maana kakaza. Muulize vzr bi. Mkubwa wakooo

Na wanawake wa humu wengi wao status za mahusiano yao ni za hovyo mnoo. Inawezekana wanamuonea wivu tu mwenzao. Princess Ariana wewe kama vipi endelea na mshikaji tu kama yatakuja kutokea yasiyo tarajiwa mbele ya safari basi utajiandaa kukabiliana nayo. Dunia hii ina

kutokea yasiyo tarajiwa mbele ya safari basi utajiandaa kukabiliana nayo tu, Kimsingi
 
Wamama wengine nuksi sana. Hapo jamaa angakua tajiri hata kama anakunywa hizo pombe na kuvuta bangi huyo mamako wala asingeona tatizo. Hapo inshu kubwa ni kwamba jamaa hana hela na mamako anataka upate bwana tajiri ili akamilishe yale ambayo yeye alishindwa kuyakamalisha enzi zako alipoolewa na babako maskini.

Mama zetu wa kiswahili ni Materialistic mnoo. Akipelekwa Diamond Platnumz kwa huyo Mama atamkubali bila hata kujiuliza. Kumbe huyo Diamond Platnumz tabia mbovu zote anazo sema tu kwa sababu ana hadhi na pesa 😂😂😂😂
 
Ariana utakuwa ni kazuri fulani hivi mama anaona you deserve better. Jamii ina expectations kubwa sana juu ya wasichana hasa wakiwa wazuri, msichana mzuri unatakiwa utembee na akili yako kila sehemu la sivyo jamii itakutoa kwenye reli.

Nina rafiki yangu anafanya kazi UN agency moja Dodoma, ananiambiaga hivi unajua kipindi nimeanza anza tu kazi nilitakaga kumuoa fulani? Huyo fulani ni rafiki yangu mwingine alikuwa pisi ya moto sana, enzi hizo. Nikamuuliza what happened…. Akasema mamaake alikataa, akanimbia kwa maisha yako huwezi muona “huyu” labda nikupe “yule” (dada mtu). Miaka imepita huyu rafiki yangu pisi kali ni single mother wa mtoto mmoja na uzuri wote kwishney anapambana na hali yake tu.

Katika situation yako unaweza kupata matokeo ya aina mbili, either upate mtu “bora” zaidi ya huyo kwa mujibu wa mama yako, au usipate mtu yeyote na ipo siku mama yako atakulaumu. Fanya maamuzi kwa makini ukiwa unajua kuna matokeo mawili yapo mbele yako.
Sasa alimuoa huyo dada mtu?

Sent from my vivo 1906 using JamiiForums mobile app
 
Mkristo R.c

Kama kuna kitu kitakachokuokoa apo ni kuingia kwenye dini yako mazima hakikisha unasali unabadilisha mwonekano wako kua muumini wa kweli usikubali mambo ya machafu ndani ya ndoa yako pia marafiki, tabia and etc, hata mambo ya ujana punguza au acha kabisa na hakikisha mume naye anaacha pia, jiunge kwenye magroup ya dini and etc alafu mwambie na uyo mchumba wako atubu na mfatane wote kwenye njia ya dini na mungu atawabarik mtatafta maisha polepole na mtapata amani ila kwa ivo ulivosema msipokua watu wa dini kuna uwezekano siku za mbeleni mkaja kupata shida sana.

Kumbuka ili historia ya mtu ibadirike kabisa inabid yankute ajute na achukie kabisa alikokua ila sio kubadirika kwa kua tu kakuona wewe ilikua ni vyema akabadirika bila hata uwepo wako yani sababu isiwe kisa wewe iyo ni WEAK REASON kumbuka alishawahi kua na mwanamke na wakaachana na wewe age yako siyo yakujaribu maisha unatakiwa uingie kwenye ndoa ukiwa unatambua unachokifanya usichukulie maskhara maana effects utazopata ndani yandoa kwa sasa zinaweza determine maisha yako yote yatayofata yatakua vipi mf MIMBA, MAGOJWA, SIFA MBAYA, ANGUKO, MUDA, UZEE. Ila kwa mwanaume ye vyakupoteza ni vichache kuliko upande wako.

KUMBUKA ANAVYOKUONESHA MAPENZI SAIVI HAITOKUA IVO MIAKA YOTE KWENYE NDOA YENU, usije ukawaza kwenye ndoa ndo mambo yatakua ivo ivo NO.

Dini itawasaidia sana kuwaongoza mtapokua mnakwazana na kukosana na mtapokua chini kimaisha haitowapa shida maana mtakua na amani na imani mungu ndo alieyetenda na ndo atawatoa kwenye ayo matatzo.

Byee.
 
Hata mimi nisingekuozesha yaani mwanaume an a kunywa pombe, bangi ,sigara mie hapana wanakuaga malaya mno

Afu pia wewe umeishia olevel na yeye olevel watoto wenu nani atawafundisha? Tafta hata mkaka mwenye diploma mtoto enu awe inspired kusoma kwa bidii

Usitangulize hisia mbelembele

Wazazi wangu walikuwa na elimu ya kawaida ila walipata watoto wa5 na wote tumesoma . wa mwisho yuko UDSM anamalizia degree yake.


NI WANGAPI HUMU JUKWAANI WAZAZI WAO HAWAJASOMA ILA WAO WAMESOMA


SI SAHIHI KWA MAONI YAKO HAYO
 
Wazazi wangu walikuwa na elimu ya kawaida ila walipata watoto wa5 na wote tumesoma . wa mwisho yuko UDSM anamalizia degree yake.


NI WANGAPI HUMU JUKWAANI WAZAZI WAO HAWAJASOMA ILA WAO WAMESOMA


SI SAHIHI KWA MAONI YAKO HAYO
Aah mi navoona ni kua mzazi kua na elimu au chochote kile lazima mtoto ashawishike mfano baba mwanasiasa kuna mtoto mmoja lazima ashawishike awe kama baba ake

Mama nesi lazima girl child awe inspire we call it 'GENERATIONAL TRANSITION'
 
Aah mi navoona ni kua mzazi kua na elimu au chochote kile lazima mtoto ashawishike mfano baba mwanasiasa kuna mtoto mmoja lazima ashawishike awe kama baba ake

Mama nesi lazima girl child awe inspire we call it 'GENERATIONAL TRANSITION'

Upendo ndo mkuu kuliko vyote.

Anaweza akaolewa na mwenye degree au Diploma na wakazaa watoto na wakaachana na watoto wasifikie malengo kama ya wazazi sababu ya malezi au shetani kuiingilia kati.


Ushaambiwa huyo jamaa ana biashara zake, kwahyo mtoto hawez kuwa mfanyabiashara?

yani mwanaume wa degree/diploma ndo aoe mwanamke asiye na elimu? kisa nini uchi au?, hata wanaume tunahitaji wanawake wa level yetu siyo chini sana

Huyo dada hana elimu hivyo akubali tu kuolewa.
 
Upendo ndo mkuu kuliko vyote.

Anaweza akaolewa na mwenye degree au Diploma na wakazaa watoto na wakaachana na watoto wasifikie malengo kama ya wazazi sababu ya malezi au shetani kuiingilia kati.


Ushaambiwa huyo jamaa ana biashara zake, kwahyo mtoto hawez kuwa mfanyabiashara?

yani mwanaume wa degree/diploma ndo aoe mwanamke asiye na elimu? kisa nini uchi au?, hata wanaume tunahitaji wanawake wa level yetu siyo chini sana

Huyo dada hana elimu hivyo akubali tu kuolewa.
Ni sawa pia mkuu haina noma
 
Umri wenyewe unaenda machweo,ukija kushtuka giza limeingia mwisho wa siku utampelekea mkwe mzee ambaye wanalingana umri na mama yako.
Kuna umri ukifika lazima mzazi na mtoto msikilizane
 
Beba mimba. Mama atatulia.

Kwa design ya mama yake sio wa kutulia hata akiwa na mimba. Kumbuka ashasema atawaendea hata kwa mganga ikitokea binti akaghairi kuachana na huyo kijana.
 
Hata mimi nisingekuozesha yaani mwanaume an a kunywa pombe, bangi ,sigara mie hapana wanakuaga malaya mno

Afu pia wewe umeishia olevel na yeye olevel watoto wenu nani atawafundisha? Tafta hata mkaka mwenye diploma mtoto enu awe inspired kusoma kwa bidii

Usitangulize hisia mbelembele
Duuu kweli nimeamini wa Afrika na wa Zungu akili zetu ni tofauti kwenye mahusiano, wazungu woa sijui niseme wajinga.

Sent from my TECNO BB2 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom