Mama huyu asaidiwe vipi mtihani huu?

Nameless-

Member
Joined
May 21, 2009
Posts
47
Reaction score
1
Wada nauliza hekima zenu:

Kuna jamaa katembea hadi kuzaa na shemeji yake (mdogo wa mkewe); imemuumiza sana mke na kumvunja moyo, ana watoto 3 na huyu mume wa ndoa, uhusiano na mumewe uko hatarini, na undugu na mdogo wake pia uko hatarini, hivi anatakiwa afanyeje?
 
hee yaani!!!!!!!! Au sijakufahamu,,,, itakuwa ni visa hivi sasa u mean dada na mdogo wake wanashare mume mmoja na mdogo mtu keshazaa mtoto mmoja au sijakusoma sawa sawa??? Ya allah....ya rabb tusamehe waja wako,,,,kila kukicha mambo yazidi kugeuka,,, subhana llah!!!!!!!!
 

Huyu dada aache wivu, amkubali mdogo wake na mtoto wake ili huyu mwanaume awalee wote. Mie bibi yangu alimruhusu mdogo wake azae na mumewe. Hao baba zangu walio zaliwa kwa mama mdogo na mkubwa kwa baba mmoja wanaelewana vibaya mnooo.
 
huyo mdogo wake hana hata haya.uchafu gani jamani...!halafu haya mambo yapo sana nchini wanaume kula mashemeji zao.ningeweza kushauri kama ningesikia wakwe wa huyo jamaa wanasema nini.
ila mie kwangu sitotoka mdogo wala wifi.mie na mume wangu kwisha kazi.undugu wakati mwingine kazi,kama wanashida saidia hukohuko sio kuongeza matatizo ndani kwako
 
Titizo mke akishapata watoto anajisahau na kuwajali zaidi watoto na mume kumuona kama mtu wa kawaida. Sasa hapo kwa nini shemeji asiliwe k........ .
Na tatizo mashemeji nao hawana maana wakija kwa dadayao ni full kumtega shemeji yake mara apite na kanga moja mara nusu uchiii basi ilimradi amweke roho juu shemeje yake. Plz kina dada mlio kwenye ndoa hebu muwe makini na wadogo zenu wa kike mnao kaa nao
 
ndo maana tunataka mahakama ya kadhi!
ili muwe munawapiga mawe watu wafe, hilo halitatokea hapa tz. ujue kuna wakristo walioolewa na waislam, hivyo usijeona mchagga mmoja akisikia binti yake aliyeolewa na mwislam anaenda kupigwa mawe ananoa panga mapemaa? hivi unafikiri mtu na akili zake atakubali mwanae akapigwe mawe ati kwasababu amezini?...si atachukua bunduki akawafyatulie hao wauaji wote na mahakama ya kadhi ndo itaishia hapohapo..watasahau hata jiwe lililokuwa wamelishika mkononi.
 
...... Plz kina dada mlio kwenye ndoa hebu muwe makini na wadogo zenu wa kike mnao kaa nao....

Hili nalo neno, ni kweli hawa mashemeji wana hila nyingi mno, lakini pia mume ukiweka mipaka na heshima mbele, hawapati kitu, uzembe ni pale ambapo nawe unajiweka ki-kutegwategwa...
 
Font yako 2 ndo inanifanya nianze kutahamaki UREMBO wako!!

 
Tuyachape viboko yote mawili hilo lililopewa na hilo lililotoa, baadhi yenu hapa jamvini sijui mkoje sasa una-quote habari nzima halafu comment ni kijimstari tu unamaanisha nini? go straight to wat you want to tell us, usilete ushamba wa CCM wa kumuunga mkono hoja ya mjumbe...
 
afunge ndoa nyingine na mdogo mtu na mtu na mdogowe wasameheane
 
Huyu dada aache wivu, amkubali mdogo wake na mtoto wake ili huyu mwanaume awalee wote. Mie bibi yangu alimruhusu mdogo wake azae na mumewe. Hao baba zangu walio zaliwa kwa mama mdogo na mkubwa kwa baba mmoja wanaelewana vibaya mnooo.

Umeshasema bibi yako na hatujui kwanini bibi yako alikubali hilo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…