Mama kabadili upepo. CCM wamegeuka wapinzani wa mama, na wapinzani wamegeuka kuwa wafuasi wa mama

Mama kabadili upepo. CCM wamegeuka wapinzani wa mama, na wapinzani wamegeuka kuwa wafuasi wa mama

Heshma kubwa kwa CCM
Uwekezaji wao kwenye rasilimali watu na ukomavu wao kisiasa wana uwezo wa kendelea kushika dola miaka mingine 100
Leteni tena mtu dizaini ya mwendazake
 
Waonye
FB_IMG_1617728213402.jpg
 
Bila shaka haya mahusiano siyo ya kutuhubiria Tanzania ni masikini na kwamba bila wafadhiri hamna tunachoweza.
Akiyasema haya hatutamwelewa

KPI tuliyoachiwa inasema Tanzania ni tajiri tunachotakiwa ni kujitambua tu
 
Binafsi nilimpenda hata kabla ya kuapa sijui kwa nini lakini nilikua nawaambia wenzangu moyo wangu ulikua mweupe kwake
Nawasalimu kwa jina la jamuhuri ya muungano.
 
Speech ya leo ya mama imegeuza milengo ya watanzania upside down. Wale ccm kindakindaki wa humu JF wafia chama wa ccm wamekuwa wapinzani wa mama, na wale wapinzani wa ccm wa siku zote wamekuwa wapenzi na washabiki wa mama.

Binafsi pia nimekuwa mshabiki na mpenzi wa mama. Naomba mnielekeze utaratibu wa kuwa mwanachama wa ccm. Nilikuwa na mpango wa kugombea urais 2025 lakini nasema mama anatosha. Nitampa tu madesa yangu ayafanyie kazi kama itampendeza. Nataka nimuunge mkono mama kwa vitendo. Tanzania yenye furaha italetwa na mama. Nani kama mama? Mama ukimzingua mnazinguana.
Tofauti na mwendazake hata usipo mzingua yeye anakuxingua.
 
Umesema ukweli na hapa chama chetu kiwe makini kikimpinga Sana mama kitapoteza umaarufu hata mh lissu umaarufu wake ili ubaki asimpinge Sana mama maana umaarufu wa lissu ulibebwa na mwendazake sasa mwendazake analiwa na mchwa huko most likely lissu umaarufu ukashuka.
Haiwezi shuka kwa haraka hivyo, kwakuwa aliyokuwa anayapigania juu ya uongozi wa meko, ni kweli yametokea, unadhania hasara hizo za ndege, zitakapowekwa wazi, kuna nini?!utoroshaji madini mererani, umekwisha?!!na hayo hayo ndio atazidi kuyasema, ili watu waone kuwa walikuwa wakiongopewa?na huu uhuru wa habari ambao mheshimiwa rais, ameuruhusu, ndio unakwenda kumuweka peupe kabisa mwendazake!!kumbe hadi leo huko barrick bado ni shida!!!na ndio maana hadi sasa lisu bado hajaafikiana moja kwa moja na haya matamko, yeye anajielewa anataka yaendane na mabadiriko ya sheria zilizotufikisha hapa.Najua MATAGA, sasa hivi mnahali ngumu sana, kuona ile faraja ya watanzania inataka kurudi.
 
Siyo CCM wamegeuka wapinzani.
CCM halisi inachekelea mapigo ya mama,, ila wale wenye genge lao ndo hao wanalialia humu daily,, mama anasambaratisha genge bila kupepesa macho. Genge lilikuwa linakula na kusaza huku watz wakiumia kwa mateso ,sasa linaeverporatiwa lifutike kabisa.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Heshma kubwa kwa CCM
Uwekezaji wao kwenye rasilimali watu na ukomavu wao kisiasa wana uwezo wa kendelea kushika dola miaka mingine 100
Hakuna shida yotote ili mradi iimarishe utawala bora.
Sasa lile genge lilikuwa linakanyaga katiba kwa mslahi yake yeye binafsi.
Ndiyo maana watu wana raha na mama, mama akiongoza hivi siku zote ,,hatuna ubaya na ccm wala chadema.

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Mimi nakwambia Kuna muda waja watatafutana.. maana Watanzania wenye kujipa muda kung'amua mambo tupo Wachache Sana.
 
Speech ya leo ya mama imegeuza milengo ya watanzania upside down. Wale ccm kindakindaki wa humu JF wafia chama wa ccm wamekuwa wapinzani wa mama, na wale wapinzani wa ccm wa siku zote wamekuwa wapenzi na washabiki wa mama.

Binafsi pia nimekuwa mshabiki na mpenzi wa mama. Naomba mnielekeze utaratibu wa kuwa mwanachama wa ccm. Nilikuwa na mpango wa kugombea urais 2025 lakini nasema mama anatosha. Nitampa tu madesa yangu ayafanyie kazi kama itampendeza. Nataka nimuunge mkono mama kwa vitendo. Tanzania yenye furaha italetwa na mama. Nani kama mama? Mama ukimzingua mnazinguana.

mkuu we hatuwez kukupa nchi utaiuza wewe kwa namna ulivyomgalagaza khumbu hapana mkuu
 
Kitu kizuri ambacho wengi hawajaelewa ni kwamba, mama anacheza muziki wake, CCM wenzie hawamuelewi sababu washazoea ngoma za kusukuma unacheza na manyoka tu lakini huku sasa unapigiwa ngoma za mwanakwerekwe na Jambiani pembeni unafukizwa ubani na marashi ya karafuu. Ile ngoma anaijua yeye mwenyewe mama.

On the other side, wapinzani sio kwamba wapo na mama, Ila hii biti ya ngoma wanaijua sababu walishaomba ipigwe Ila jamaa wa kisukuma walikuwa wanakataa kabisa wakidai hiyo ni ngoma ya watu walainilaini wao wamezoea kula maugali tu wanataka kurukaruka kama vichaa.

Sasa kwa mdundo huu wapinzani wanausherehekea kwa sababu mama kumbe yeye anataka kila mmoja wetu ajue kwamba hiyo ngoma ndio ya kwao na yeye ndio kaomba ichezwe, anayependa aingie tucheze, asiyependa atupishe.

Haimaanishi wapinzani sababu wanamsherehekea ndio kwamba upinzani umeisha. Mama akivurunda hatakosa spana za uso. Ila kwa sasa bado anacheza biti ya nyumbani mwanakwerekwe. Mje tucheze nchi yetu site hasira za nini kwani si anatembea kwenye kurasa 303 au vipi wakulungwa?
 
Back
Top Bottom