Mama kanikimbizia mchumba wangu

Mama kanikimbizia mchumba wangu

Mama Yangu Kanikimbizia Mchumba Wangu!

Mimi ni binti wa miaka 30, sijaolewa ila niko kwenye mahusiano na Kaka mmoja huu ni mwaka wa saba. Mwaka jana tuliongea kuhusu ndoa akaniambia itakua mwaka huu, basi nilikubali nakukaa kimya, lakini mwezi wa sita alisimamishwa kazi hivyo nilishindwa kumuambia kuhusu mambo ya ndoa kwani alikua hayuko sawa kiakili kabsia.

Ilinibidi kunyamaza, lakini nyumbani walikua wnanipigia kelele sana, ilifikia kipindi mpaka Mama akanitafutia mwanaume kwakua tu alikua anahitaji mjukuu, basi kuna siku nilienda kuonana na huyo mwanaume, tukabaidlishana namba ili tu nimuangalie. Lakini nilijikuta namchukia tu kutokana na tabia zake na kwakua bado nilikua nampenda mwanaume wangu niliamua kumpotezea.

Mwezi wa 8 mwanaume wangu alirudi kazini, akawa sawa na kuniambia kuongea na nyumbani kuhusu ndoa, kweli nilifanya hivyo, lakini kabla hawajaja kwetu kuna siku akakuta meseji zangu na yule mwanaume, zilikua meseji za zamani wakati Mama aaniunganisha naye, nilijua nishazifuta lakini sijui nini kilitokea basi nikawa sina namna zaidi ya kumuambia ukweli.

Nikamuambia kuwa nyumbani walinitafutia mwanaume lakini baada ya kuongea naye mimi nilimkataa, aliniuliza inamaana ungemnkuta ni mzuri ungeenda kuolewa naye, nilibaki kimya, tuligombana sana, aliumia sana alikua mpaka analia kwa hasira mwisho akaniambia hahitaji tena kunioa kwani kama tatizo kidogo tu nimetaka kumaucha vipi tukiingia kwenye ndoa.

Kakatisha kila kitu, kachukua kila kitu chake na kunirudishia kila kitu changu, nimejaribu kumuomba msamaha, nimetumia rafiki zake lakini wapi. Naumia sana kwani tulikua vizuri sana, ananijali, ananihudumia yaani kila kitu kilikua sawa lakini sasa hivi hawezi kuwa na mimi, naomba ushauri wako sijui nifanye nini Kaka kumrudisha kwani nampenda sana nilionana na huyo mwanaume mwingine kwaajili ya Mama tu.
Kwanza Pole! Naelewa hali unayopitia kwa Sasa. Nakuombea neema ya Mungu iwe juu yako na kukulinda..

Sijui kila kitu ila nitasema Machache niliyo nayo.

Ni asili ya mwanaume japo si wote, kushindwa kuendelea na mtu aliyetambua na kujua kama alimsaliti!

Hili ni kwa Sababu wanaume wengi Wana asili ya kumiliki wao pekee yao, wakigundua kuwa yupo mwingine katika eneo la umiliki huingia hasira na maumivu makali sana.

Hivyo kubali kama ulikosea! Hii ni hatua ya kwanza katika utatuzi wa matatizo ya kimaisha.

Usitupe lawama kwa mama, kwa sababu wewe ni mtu mzima ulikuwa na nafasi ya Kufanya maamuzi ya kukakataa!

Sitaki kukulaumu ila nataka hili jambo kiingie ndani yako kuwa ulikosea.


Pili; Kubali umesababisha maumivu kwa mwenzio uliyedumu nae kwa miaka Saba! Vaa viatu vyake! Kubali umejeruhi moyo wake! Kubali umevuruga mipango ya maisha yake kwa Sasa.

Ukikubaliana na Mimi katika hayo Machache hapo juu! Fanya haya yafuatayo;


1. Sijui Imani yako! Ila Rudi kwa Mungu kwa Toba . Hakuna msaada Bora duniani kama kusaidiwa na Mungu..

2. Muombe mwenzi wako kwa Mungu ampe uponyaji wa ndani! Ni Mungu pekee anayeweza kubadilisha moyo wa mtu hata kufikia hatua ya kukupenda Tena..

3. Since umekuwa na huyo mtu kwa miaka Saba, tambua you people mna great attachment sana! Hivyo si vyepesi hata yeye kukuacha na kukusahau kwa haraka. Kwa sababu hiyo usikate tamaa kulipambania penzi yako.

4. Omba Mungu akupe neema na huruma zake juu ya jambo hili (His grace and mercy) ... Muombe Mungu akustahilishe usivyostahili ... That's grace!

Speaking by experience ... nakuombea
 
Duuuh hatari sana ๐Ÿคฃ๐Ÿคฃ, nilijua 30 ni binti mbichi kabisaa
Mdada wa umri huo kama ndo umekutana nae ukaamua kuwa nae unamdate Kwa tahadhari kubwa na baadhi ya vitu inabidi uvumilie maana ni ngumu kubadilika tofauti na binti wa miaka 18-23 ambae kichwa chake bado hakina mambo mengi unaweza fanya inducement ya falsafa zako akawa aina ya mke unayemtaka
 
Mdada wa umri huo kama ndo umekutana nae ukaamua kuwa nae unamdate Kwa tahadhari kubwa na baadhi ya vitu inabidi uvumilie maana ni ngumu kubadilika tofauti na binti wa miaka 18-23 ambae kichwa chake bado hakina mambo mengi unaweza fanya inducement ya falsafa zako akawa aina ya mke unayemtaka
Hahaha ๐Ÿ˜ƒ sawa mzee wa kumtengeneza future wife, 30 yrs ni mshangazi stage 1 siyo?
 
Kila mwanamke anataka wa kumhudumia ila wao hawana cha kuhudumia zaidi ya uchi na kuosha vyombo
Kuzaa na kulea watoto??? Hiyo sio kazi ???

Fikiria anatumia maisha yake kuzaa na kulea kizazi kinachobeba jina la ukoo wako na sio ukoo wake yeye.

Mitoto yako pengine haina hata shukrani, anaizaa kwa uchungu, anainyonyesha na kuifuta mavi hadi wawe wakubwa, huo muda si angeutumia kujitafutia riziki yake binafsi
 
Back
Top Bottom