Uwongo kuna mahali hukwama mkuu!hakuwa na leseni?haakufanya birthday ya miaka 18?sasa amefikisha apate adhabu stahiki kulingana na kosa lake.Kanumba alikuwa na makosa yake ya kutembea na under age,na he has paid an expensive price.He died period.Hakuwa na miaka 18 wakati yanatokea
Yaani mm tu hata nikijaribu kutafakar tu kichwa kinawaka moto ni hatar sana mkuuOmba sana yasije upande wako
Mfalme who??
MFALME ZUMARIDI.Mfalme who??
Mama ni kigeugeu tu. Kashatafuna Mali zote za mwanae akimuona Lulu yuko mtaani anatesa kaona aliamshe afungwe, alishasema sijui kamtupa sijui nini.Huyu mama jamani.
Uko sahihi mtoto anauma saana jamani watu wanashindwa kumuelewa huyu mama anaendeshwa tu na uchungu Na si vingineMungu amtie nguvu tu maana mtoto anauma jomoni
Ni kuweweseka tu. Akirudi ndio uasama itakuwa mkubwa sana. Lulu ataendelea kuigiza Na kupata pesa. Na kanumba ayupo kaoza
kweli kabisa,tulioingia labour ndio tutaelewana lugha hapa, uchungu wa mtoto haupimikiUko sahihi mtoto anauma saana jamani watu wanashindwa kumuelewa huyu mama anaendeshwa tu na uchungu Na si vingine
Siku moja baada ya Elizabeth Michael 'Lulu' kuhukumiwa kifungo cha kutumikia jela miaka miwili kwa kosa la kuua bila kukusudia, mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Frora Mutegoa amesema wanaombeza kwa kuishukuru mahakama wamuache kwa kuwa hakuna mwenye uchungu zaidi yake.
Jana baada ya Mahakama Kuu kumtia hatiani mwigizaji huyo na kumpa adhabu ya kifungo cha miaka miwili jela, Mama Kanumba aliishukuru mahakama akisema imetenda haki jambo ambalo lilizusha gumzo wengi wakisema hakupaswa kufurahia adhabu hiyo.
Akihojiwa na waandishi wa habari nje ya mahakama kuu jijini Dar es salaam jana Jumatatu baada ya hukumu kutolewa alisema anashukuru kwa kuwa haki imetendeka na kwamba atakwenda kumzika rasmi mtoto wake.
Hata hivyo, Mwananchi leo Jumanne amenukuliwa akisema asibezwe kwa kauli hiyo kuwa hakuna anayejua uchungu anaoupata kila siku.
"Mimi sijui kama ninafurahia kama wanavyodai, waulize kwamba, yeye Lulu alipokufa mwanangu Kanumba alifurahia? Mimi ni mkristo, sipendi kuona baya likimfika binadamu mwenzangu, lakini Lulu ameenda miaka miwili jela na atarudi, je mwanangu atarudi lini? nitamwona wapi tena"? Amehoji.
Lulu kwa wakati anatembea na kanumba alijifanya ana miaka 18 hata club alikuwa anaenda nk .Kanumba angejuaje umri wake?Mimi nafikiri wazazi wa Lulu wana makosa zaidi maana walijua umri wa mtoto wao ila hawakuuweka wazi ingemsaidia mtoto wao kutokuingia matatizoni.Chini ya miaka 18 lakini akili na mambo yake ni kama ana zaidi ya miaka 25 hapo inakuwaje?