Mama Kanumba:Nataka heshima kwa Lulu

Mama Kanumba:Nataka heshima kwa Lulu

Opera Min

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
890
Reaction score
658

Wadau nimejaribu kuusikiliza huu ujumbe wa Mama Kanumba kwa LLulu,nikajiuliza kama Lulu angekua mtiifu kwa Mama kanumba je angeweza kuomba mahakama ifute kesi? Je kukomaa na ile kesi ilikua ni kisasi ama nini? Watu wa Sheria leteni ufafanuzi kwa hilo swali langu la kwanza...
 
Fikiri kabla yakuandika Mama Kanumba alimpoteza mtu mhimu sana ktk Maisha yake,Kwanza ni mtoto ambae alimzaa mwenyewe pili alikua Msaada ktk maisha na aliyabadilisha sana maisha yake,kwa Mantiki hiyo Kisaikolojia hayuko sawa ukizingatia Wadau mhimu waliomwahidi Kumpa sapoti Wameingia mitini so huyu mama kusema hivyo nikama kujifariji tu,Mwisho kabisa Lulu ni mtu Maarufu na Visenti anavyo alikua na wajibu wakua karibu na huyu Mama maana Sio siri Kanumba alipoteza maisha ktk Mazingira ambayo ni ngumu kumuweka kando huyu binti na Mahakama imeliona hili ndio Anatumikia kifungo
 
Huyu Bi.Mkubwa angetulia na asinge jihusisha na ile kesi,ingemletea heshima kubwa sana kwa baadae
Huo ni mtazamo wangu lakn!
 
Kwanza kosa lilikuwa la marehemu la kufanya maagano ya kishetani, pili lilikuwa ni kosa la marehemu kujihusisha kimapenzi na mtoto mdogo,
Unaandika kitu ambacho ni upuuzi sana wakati akijihusisha kimapenzi lulu alikua na Umri gani? Ulishawahi kujiuliza Kunumba alikua mwanaume wangapi kwa lulu?
 
Huyu Bi.Mkubwa angetulia na asinge jihusisha na ile kesi,ingemletea heshima kubwa sana kwa baadae
Huo ni mtazamo wangu lakn!
Kisheria huyu mama hakuwa na uhusiano wowote na kesi, sidhani hata alikua ktk list ya mashahidi. Kesi ilikua ni ya Jamuhuri dhidi ya Lulu. Kesi za jinai zinabebwa na serikali, hata kama wewe mwanao aliuawa utabakia shahidi tuu au mtazamaji, huna uwezo wakufuta kesi hata kama unania hiyo. Hata mkielewana wenyewe bado kesi itaendelea. Jaribu kugoogle tofauti ya kesi ya jinai na kesi za madai, itakuongezea uelewa mpendwa.
 
Unaandika kitu ambacho ni upuuzi sana wakati akijihusisha kimapenzi lulu alikua na Umri gani? Ulishawahi kujiuliza Kunumba alikua mwanaume wangapi kwa lulu?


Sisi hatujiulizi maswali ya kijinga, tunachojua Kanumba alikuwa anamfanya Lulu wakati bado alikuwa mdogo. Kuwa mwanaume wa pili au wa nne haiwezi kuwa excuse ya kuwaingilia kimwili underage. Kanumba kifo kimemuumbua, maana hata wakina Shigongo walikuwa hawajui kinachoendelea.
 
Back
Top Bottom