Mama katangaza mchakato wa katiba mpya; Tanzania yote ina furaha

happyxxx

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2020
Posts
604
Reaction score
1,970
Ni furaha kila kona wapinzani wamejaa furaha CCM wamejaa furaha watanzania wote tumejaa furaha. Mama katangaza mchakato wa katiba mpya uanze. Aliyenuna sisi hatuna cha kumsaidia.

Mwisho wa siku wawakilishi wetu bungeni watatupatia katiba iliyo bora. Hatutegemei wasiotutakia mema nchi yetu wavuruge mchakato.

20230507_162641.jpg
 
Anapoteza muda SGR na Bwawa la umeme vinamsumbiria, afanye mambo kwa focus issue za katiba hawezi anasumbuka bure
 
Katiba mmewapa vilaza wa Bungeni ambao hawana exposure na Maisha ya maendeleo ili wajadili if yes don't expect anything Great to happen

Katiba Mpya mgetuachia sisi wananchi tuchambue na tutoe mapendekezo na sio kulazimisha kuwapa wabunge ambao hawajitambui.
 
Ni furaha kila kona wapinzani wamejaa furaha CCM wamejaa furaha watanzania wote tumejaa furaha. Mama katangaza mchakato wa katiba mpya uanze. Aliyenuna sisi hatuna cha kumsaidia.

Mwisho wa siku wawakilishi wetu bungeni watatupatia katiba iliyo bora. Hatutegemei wasiotutakia mema nchi yetu wavuruge mchakato.
Wale wapinzani woote wa katiba Mpya.....kimyaaaa😅😅😅
 
Ni furaha kila kona wapinzani wamejaa furaha CCM wamejaa furaha watanzania wote tumejaa furaha. Mama katangaza mchakato wa katiba mpya uanze. Aliyenuna sisi hatuna cha kumsaidia.

Mwisho wa siku wawakilishi wetu bungeni watatupatia katiba iliyo bora. Hatutegemei wasiotutakia mema nchi yetu wavuruge mchakato.
... never ever! Kama tunategemea wanaonufaika moja kwa moja na Katiba iliyopo watatupatia Katiba bora hizo ni ndoto za alinacha!
 
Ni furaha kila kona wapinzani wamejaa furaha CCM wamejaa furaha watanzania wote tumejaa furaha. Mama katangaza mchakato wa katiba mpya uanze. Aliyenuna sisi hatuna cha kumsaidia.

Mwisho wa siku wawakilishi wetu bungeni watatupatia katiba iliyo bora. Hatutegemei wasiotutakia mema nchi yetu wavuruge mchakato.
Una uhakika kupata katiba itakayopunguza madaraka ya viongozi kwa kutumia wanaotafuta uongozi huo huo? Mfano tunatumai kupata katiba ambayo itapunguza madaraka ya Rais! Je, Rais atakubali kusaini katiba itakayotaka Rais ashitakiwe kwa makosa aliyoyatenda akiwa Ofisini? Je, wabunge watakubali kipengele cha Waziri asiwe mbunge wakati wao wanagombea Ubunge ili wawe mawaziri? Tafakari kuhusu uchaguzi huru iwapo tunasema wabunge waliingia kwa kupitia uchaguzi Usio huru na haki?
 
Je Rasimu ya Jaji Warioba au tuanze upya?
 
Ukweli CCM hakuna anayetaka Katiba mpya maana Vyeo vya kupewa ndo mwisho
 
Je Rasimu ya Jaji Warioba au tuanze upya?
Kwanini mnataka kuwapa mzigo wananchi kwa matumizi yasiyo ya lazima? Rasimu ya Warioba iliyotokana na wananchi ipo mnaogopa nini kuanzia hapo?
 
Tunataka kuwapa mzigo wananchi kwasababu katiba hii ni ya Wananchi.
 
Katiba Mpya haitakuletea Chakula mezani, haitakujazia pesa kwa akaunti yako.
Pambana, jitume fanyakazi kama kichaaa, weka akiba kama mwendawazimu, weka Vitega Uchumi kama hayawani hayo makatiba yawe mazeee au mpya hayana nyongeza yoyote kwetu walalahoi. Kikubwa amani iendelee kutamalaki.
 
Tunataka kuwapa mzigo wananchi kwasababu katiba hii ni ya Wananchi.
Wananchi walishatoa maoni yao hamkuyapenda sasa mnataka kulazimisha matakwa yenu kupitia kwa watu wenu mliowachagua halafu muhalalishe kuwa katiba ya wananchi!
 
Back
Top Bottom