Mama katangaza mchakato wa katiba mpya; Tanzania yote ina furaha

Wananchi walishatoa maoni yao hamkuyapenda sasa mnataka kulazimisha matakwa yenu kupitia kwa watu wenu mliowachagua halafu muhalalishe kuwa katiba ya wananchi!
Maoni hayo huenda yamepitwa na wakati,hakuna ubaya wowote kuanza kuchukua maoni mapya.
 
Kama hiyo katiba itakuwa ya wananchi na sio kiini macho, italeta Mazingira ya kutengeneza pesa zaidi kwa walalahoi .
 
Issue siyo katiba mpya issue ni katiba yenye manufaa kwa taifa
 
Uku ni kukosa shukrani ndugu mtanzania. Wananchi kupitia wawakilishi wao bungeni watatuletea katiba iliyo bora kabisa. Maoni yalishatolewa kwenye tume ya warioba.
 
Kwa vilaza waliopo bungeni ndio wajadil mchakato???
Hatuwahitaji hawa wabunge waliopo bungeni kwa Sasa kushiriki kwa namna yoyote kwenye mchakato wa kupata katiba mpya. Labda kwa uwakilishi wa wabunge wawili kama taasisi. Hawa ndio waliovuruga tangu mwanzo otherwise tungeshakuwa na katiba mpya tangu kitambo
 
Itakuwa imebadilisha kitu iwapo italeta sera za majimbo, yaani kupeleka mamlaka ya kuunda sera karibu na wananchi. Mengine yote yatakuwa blah blah tu.
 
Maoni hayo huenda yamepitwa na wakati,hakuna ubaya wowote kuanza kuchukua maoni mapya.
Haiwezekani kuwa maoni yote yamepitwa na wakati! Kama yapo yaliyopittwa na wakati yarekebishwe kwenye ile rasimu!

Wezi na mafisadi wa awamu zilizopita ndio walihujumu Rasimu ya Warioba; Samia hana sababu ya kusikiliza ushauri wao kwani yeye sio Mwizi.
 
Uku ni kukosa shukrani ndugu mtanzania. Wananchi kupitia wawakilishi wao bungeni watatuletea katiba iliyo bora kabisa. Maoni yalishatolewa kwenye tume ya warioba.
Kama hujui uliza! Acha ushabiki wa kitoto
 
Utavurugika tu ,na kitakachouvuruga ni kipengele Cha muungano!! The best option NI watuachie wananchi tuupigie kura Aina ya muungano tunaoutaka !!
 
Uku ni kukosa shukrani ndugu mtanzania. Wananchi kupitia wawakilishi wao bungeni watatuletea katiba iliyo bora kabisa. Maoni yalishatolewa kwenye tume ya warioba.
Kwa wale vilaza waliojazana mule,,, hii process waangalie namna nyingine tu, ila kama hao vilaza ndo watakua wahusika wakuu basi majanga ni yaleyale tu
 
Unaweza ukawa sahihi.
 
Rais Samia akiipatia nchi katiba Bora atakua kafanikiwa kuweka kumbukumbu ya vizazi na vizazi hasa kwa mapinduzi ya utawala bora na nchi itamkumbuka kwa hilo
 
Katiba haitungwi na mtu au chama kimoja ndio maana umesikia wadau wote hata wasio na chama watahausika. Kuna kuwa na bunge la katiba ambalo lina uwakilishi toka kila makundi ya kijamii.
 
Katiba haitungwi na mtu au chama kimoja ndio maana umesikia wadau wote hata wasio na chama watahausika. Kuna kuwa na bunge la katiba ambalo lina uwakilishi toka kila makundi ya kijamii.
Ile iliyopita hujui ilikwamishwa na wajumbe kutanguliza maslahi yao? Hii Unadhani kwa vile si JK ni mama itapita! Kunatakiwa kuwepo na sheria ya kukataza watakaopitisha kutogombea kwa muda kama miaka 20 ili kukwepa maslahi binafsi. Nani apunguze mamlaka yake ili akufurahishe. Fikiria nje ya box
 
Majadiliano yasio na muda maalumu yanafikirisha, 98% ya bunge ni CCM, hayo makundi maalumu yote kwa uzoefu lazima yaunge mkono msimamo wa CCM, na ndivyo ilivyokuwa kwenye bunge la Katiba lililopita, ndio maana vyama vya upinzani vilijitoa. Bado ni giza
 
"Mwisho wa siku wawakilishi wetu bungeni watatupatia katiba iliyo bora. Hatutegemei wasiotutakia mema nchi yetu wavuruge mchakato"
Kama nchi inataka iwe na katiba iliyo bora itakayokaa hata miaka 50, basi bunge la katiba liundwe liwe na watu mchanganyiko, kutoka makundi mbalimbali, kusema kuwatumia wanasiasa pekee haitapatikana katiba zuri yenye kungusa maeneo mbalimbali ya raia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…