Mama Kilango apiga Kambi Moshi mjini; kumng'oa Ndesamburo?


Mkuu FMES,Mimi binafsi nimeukubali msimamo wako pale tunapoweka maslahi ya taifa mbele,undugu, ufamilia, ubinafsi vyote tunaacha nyuma, tunatanguliza taifa mbele.Ushauri, FMES, take advantage ya proximity, umshauri mama, haukuna ubishi, yuko juu, mpe ushauri, asijione amesimama, aangalie asianguke.Mshauri amaintain msimamo wake, asianze kuharibu.Kwa gia unazoondoka nazo sasa, lazima mwenye masikio atasikia.Asante.
 
Wanafiki utawagundua tu, mama Kilango na wenzake walipoenda kuchangia kule kwa Lowassa, kuna watu hapa wakashangilia. Sasa amerudia ujinga wake huo kwa kuacha ya kwake Same na kwenda kwa Ndesamburo, vilio na matusi kibao.

Personalities hata siku moja hazitatusaidia Tanzania zaidi ya kufurahisha nyoyo zetu JF. Tuunge mkono sera, tuunge mkono maadili ya aina fulani na tuunge mkono utiifu wa sheria.

Hii ya kupoteza muda kujadali watu, tumekuwa tukifanya miaka na miaka na kila siku nchi inazidi kuwa maskini. Wengi wa viongozi wetu ni wajanja ambao wako tayari kufanya lolote ili waendelee kuwa madarakani.

Mama Kilango tayari kesha jiona ni mtu maarufu wakati hakuna tangible results ambazo zinaongozana na huo umaarufu wake. Huo ni umaarufu wa kwenye makaratasi ambao unaweza kuungua moto wakati wowote.

Bado mimi naamini mijadala yetu ingelenga kwenye sera, je tunataka viongozi wanaoamini kwenye kitu gani ndio wapete 2010? Kutamka kwamba ni mpambanaji wa ufisadi mbona ni rahisi mno, lakini kutekeleza kwa matendo au dhati ndio ngoma nzito.
 
kundi la wapambanaji wanajipanga kumsimamisha ...REGINALD MENGI moshi mjini mwaka 2010......thats confirmed!!...check this forum..
 
Kuna kitu kinaitwa DAY DREAMING. Mama Kilango (mimi nanjua kwa jina la Anna Nyange) ana haki ya kuota mchana na ameitumia haki yake vilivyo. Wachagga sio mbu mbu.
 
Huyu mama hajaenda Moshi hivi hivi, katumwa na fisadi nyangumi aliyebadilisha kituo cha kadi ya CCM kutoka Ilala kwenda Moshi. Kuna kitu wanakitafuta pale, ila kajishusha sana kupambana na Mb. Ndesa, hakupata washauri, kwani yeye moto wake na Mama Simba bado hajauzima yeye anaongeza petrol subiri uone Ndesa atakavyomshushua kiulaini.
 
mdomo wa ndesa hauna breki ..mrema mwenyewe alikuwa anamjuwa...amuulize mama minde.........."alimuambia mama minde kama anataka amuachie ubunge aache kunywa pombe na kuwashika vijana....,na offcourse watu wanajuwa hiyo ndiyo tabia ya mama minde ...pombe zinakimbilia miguuni badala ya kichwani....na mume alikuwa amefukuza..kama specioza...,na akamuambia ampelekee museveni mtoto wake[its known kuwa mama minde walikuwa wanafundisha pamoja na museveni chuo cha ushirika ,,,,and they were..]......sasa mama k...naye ajiandae kurushiana makombora na ndesa pesa...yule mzee hazimo!!.....na Mengi naye this time kama amemuomba mama kilango ampigie kampeni....alkienda mwenyewe akiaza kuumbuliwa na siasa za ndasa asiite polisi au kulia kwenye ITV...kama ni ngumi za kisiasa wapigane kavu kavu!!
 
Nadhani hizi ndo indicator za kuwazindua CHADEMA kuamka kama wamelala wajipange uchaguzi ndo huoooo!!!

Ila sijafahamu kwenye uchaguzi wa CCM wafanyabiashara je wanaruhusiwa kwenye hizi chaguzi zijazo??? kama ni ndiyo basi tunakazi ya ziada kuongeza mafisadi 2010.
 
Tuone mashtaka dhidi ya Sophia Simba yataifikisha wapi ngonjera hii,huku makamu mwenyekiti wa CCM ameshasema Sophia hana makosa.Uwii!!!
 
Huyu mama anachofanya ni kumpigia mbuzi gitaa ili acheze. Si rahisi kumtoa Ndesa moshi kwani amekuwa mstari wa mbele kuwapelekea maendeleo pale moshi na mara nyingi amekuwa akitoa pesa zake mwenyewe.

Je mama umepewa pesa na nani this time? maana tumepata taarifa kuwa zamani ulikuwa ukichukuwa posho kwa JITU Patel!!!!
 

Hahahaha! So Mr. Clean man (Mengi) is involved.
 
CHADEMA wakiguswa JF huwa pananoga! This is like chickens coming home to roost.

Huyu mama leo atatukanwa matusi yale yale ambayo mama Simba alipoyatamka, wengi tu hapa JF walikubaliana huyo mama akapimwe Mirembe.

Sijui na sisi wana JF tukapimwe Mirembe pia?
 
Debe tupu .....................

Mfupa ukimshinda fisi.....................

Kila la heri Mama K
 
kundi la wapambanaji wanajipanga kumsimamisha ...REGINALD MENGI moshi mjini mwaka 2010......thats confirmed!!...check this forum..

Mwana wa Mikael hapo umesema kweli,
Mimi nilijua tu kuwa huyu mama anamwandalia mzee wa NICOL hasa baada ya mzee kuhamishia uanachama wake Moshi. Sasa kasheshe itakuwa kati ya Mengi na rafiki yake Ndesa. Je Chadema wataamua kumwachia Mengi maana amekuwa akiwapiga tafu? Hapo kwa kweli ni pagumu. CCM wanaweza kumpitisha Mengi ili wachukue jimbo. Sasa swali lingine je Chadema hawakuyaona haya mpaka wakavutwa na hao wanaojifanya wapambanaji au Chadema nao ni mpango mkubwa wa CCM kuua kabisa upinzani Tanzania. Yaani kwa sasa siamini Chama cha Siasa na Mwanasiasa yeyote
 
nilipomuona mama Kilango anapambana bungeni nilifikiri anapigania maslahi ya taifa kumbe anaendeleza siasaza uCCM, watu wa aina hii hawatufai kabisa katika uongozi wa kitaifa
 
Naam, Mama Kilango anachemka na kufulia kwenye suala la kuamua kwenda kuweka kambi kwenye majimbo ya wengine. Hizi mbinu mie naziona zina walakini. Nilidhani kunakuwepo na 'mikakati' maalum inayopangwa kichama na kufanyiwa kazi kichama na si kila mtu kivyake vyake. Kwa ujinga wangu nilidhani Chama kama cha CCM kinapofika kipindi cha kukaribia uchaguzi basi kuna vikao vinavyokaa kuangalia ni majimbo gani ambayo Chama kinaweza kurudisha/kupata wabunge bila matatizo na ni majimbo yepi ambayo yanaonekana magumu kuyapata na hayo ndiyo yanapaswa kuwekewa mikakati maalum kichama ili yaweze kupatikana. Hii habari ya Mama Kilango kukurupuka bila utaratibu unaoeleweka kichama, naiona ina walakini. Anajitafutia matatizo. Labda amelewa na kudhani kwamba yeye ni maarufu sana kwa hiyo popote atakapotua anaweza kushangiliwa. Asijidanganye na asidanganyike.
 

Lingine ninalohisi ni kwamba huenda Mzee Ndesa keshasema kwamba yeye anataka kupumzika. Kwa hiyo pilika pilika zote hizi za Mama Kilango na jina la Mzee Mengi kuhusishwa ni baada ya kujua kwamba Mzee hatagombea? If this is the case then the whole scenario makes sense. Huenda Chadema hawana candidate ambaye wamemtayarisha vizuri kuweza kuchukua nafasi ya Mzee Ndesa au kama yupo basi CCM wanaona wanao ubavu wa kuweza kupambana naye na kumshinda.
 
Mkulima, Ndesa hazungumziwi kwa sababu ni mbuge kutoka Chadema, bali ni kwa style yake ya kuwatumikia watu wake kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kujitolea kwake kwa watu wa Moshi.
Huyu hata angekuwa ni Mbunge kutoka CCM, nahakika hata watu wa Chadema wangemuunga mkono.
Wana JF hatuhitaji kupelekwa mirembe, apelekwe yuleyule aliyependekezwa na Tingatinga.
 
mimi nadhani ana kazi kubwa sana pale jimboni kwake same, sasa aende kupiga kambi mpaka 2010, nani atafanya kazi za jimbo lake?
 
Jimbo gani analoliongelea Moshi Mjini au Same? naona anapoelekea kunafuka moto aangalie tu asipoteze hata hilo jimbo la Same!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…