Mimi naona asitoke ccm bali abaki huko huko akiwasha moto labda kama ccm wenyewe wataamua kumfukuza baada ya kuona amekuwa moto mkali zaidi.
Mama Anna kilango na wengine kama wakina Kimaro waendelee kubaki huko huko wakiwasha moto. si unajua akina Kimaro walikuwa NCCR mageuzi? naona bado hali ya siasa za huku upinzani bado ccm hawakuzisafisha kuzimaliza. Ila niliota ndoto kwamba wamezaliwa wapinzani wengi sana wa uovu ndani ya ccm yenyewe. Sijui ilikuwa ya kweli au ilikuwa ya uchovu wa kazi nyingi nilizokuwa nazo siku hiyo.
Nayaheshimu maoni yako....Ila maoni yangu ni kuwa asibakie humo ccm ni kuchafu mno kwasasa na akijaribu kusema awageuke akiwa ndani watamwua!
Nadhani umeshindwa kusoma hiyo makala ya Ngurumo hapo juu.....Isome utaelewa ni kivipi hawezi kufanya lolote humo ccm.
Kimaro na wenzake tutawashauri tu..Hatutaweza kuwapangia..Wanajua nani ni nani..Na sisi pia tunajua.
Hakuna atakayejipenyeza...WAZALENDO WANAJULIKANA NA KAMA KUNA WENGINE WATAJULIKANA KWANI TUNA VIPAJI VYA KUWATAMBUA!
NB
😛ia kumbuka kuwa usanii wa ccm..Umevilazimisha vyombo vya dola kuijiingiza kwenye siasa!
Niliwahi kuonya huko nyuma kuwa...ILE KAMATI YA EPA YA RAIS HAIKUWA NA MAANA!
Wao walidai kamati hile ni kukusanya ushaidi na kuwahoji watuhumiwa!
Watuhumiwa HAWAKUHOJIWA...Badala yake ni wananchi.
Ndugu zangu ushahidi uko na ulikuwa nje nje hivyo hakukuwa na maana kuanzisha kamati kwani nadhani hiyo kamati ilikuwa na majukumu pamoja na mengine haya:
1)Kuhakikisha ushaidi UNAKUFA AMA KUPOTEA.
2)Kuwataka watu wenye TAARIFA WAENDE POLISI WAKATI TAARIFA HIZO ZILIKUWA TAYARI MIKONONI MWAO...NI ISHARA KUWA WALIKUWA WANASUBIRI VIMBELE MBELE ILI WAWABANE NA KUJUA TAARIFA HIZO WAMEZITOA WAPI!
Kwa kifupi walikuwa kwenye uchunguzi mwingine kabisa wa kuangalia ni kivipi issue ili liki ili waweze kumpata mchawi wao!
Hivyo wale whistle blowers kuweni makini kama bado hamjajulikana maana mchezo ushakuwa mchafu mno!
Hii kamati ya kina mwema ilikuwa na madhumuni ya kuwatafuta nyie mliotoa siri kwa udi na uvumba ili kuwafutilia MBALI!
Kama ni ushahidi...RIPOTI ZOTE ZA UKAGUZI ZILITOSHA NA ZINATOSHA NA NDIO TUNATAKA KUZITUMIA!
Hiyo ripoti washajua hawawezi kuibadili na hivyo tumeshtukia...Tuendelee na maombi!