Wewe unayetaka ku prove kwamba kuna flaws ndiye unatakiwa kuniambia mie flaws ni zipi, usisubiri nizi extract kama dentist anayetaka ku extract a molar.
Wakubwa wa nadharia ni wale wanaofikiri kwamba dunia hii haibadiliki, mwanamke anaolewa, mwanamme anaoa, mtoto wa kike anatakiwa kutaka kuolewa siku zote, na hawezi kukataa kuolewa hata kama jamii yake inamshurutisha kuolewa kwa mfumodume.
Wanaokata nadharia ni wale wanaosema dunia inabadilika, dhana ya kwamba mwanamke anaolewa na mwanamme anaoa inaweza kuwa challenged, mtoto wa kike anaweza kuchumbiwa akaona kuolewa gozigozi akataka kusoma, hususan kwa sababu ndoa zenyewe zimekuwa predicated katika mfumo dume unaomtaka yeye "aolewe" na mwanamme "amuoe".
Nani kasema kuna watu waliostaarabika duniani? Dhana nzima ya "kustaarabika" ni ya kumdharau muafrika kwa sababu mzizi wa neno "kustaarabika" ni "arabika" na "arab". Kwamba huwezi kuwa enlinghtened mpaka ugeze waarabu. Mi natafuta vingine, si kustaarabika, kwani kwangu mimi kustaarabika ni utumwa wa kumfuata muarabu.
Naenda kwa etymology, inayoangalia mizizi ya fikra katika mizizi ya maneno ya lugha.
Zaidi ya hapo, siamini kwamba kuna watu walio "enlightened" zaidi ya wengine kama nisivyoamini kwamba kuna zaidi kati ya mwanamke na mwanamme. Kuna wanawake wengine wako zaidi ya wanawake na wanaume wengi, kuna wanaume wengine wako zaidi ya wanawake na wanaume, lakini kama kuna tofauti kati ya wanawake na wanaume it is purely social, nothing inherent.
Kama vile kuna wazungu wengine walio zaidi ya waafrika, na kuna waafrika wengine walio zaidi ya wazungu, social, nothing inherent or biological.
Kwa msingi huu notion nzima ya "waliostaarabika" inakuwa suspect kama sio a relic of the past.
Kuna concepts zilizo enlightened, nyingine hazipo hivyo. Zaidi ya hapo, open season.