Mama lishe walikimbia soko la Kisutu, warudi mtaani kisa ushuru wa shilingi 500

Mama lishe walikimbia soko la Kisutu, warudi mtaani kisa ushuru wa shilingi 500

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Uongozi wa soko la baba na mama lishe Kisutu jijini Dar es Salaam wamesema Serikali iwashughulikie kundi la mama lishe na baba lishe ambao wanaondoka sokoni hapo na kurejea mitaani kwa kigezo cha kushindwa kulipa ushuru wa shilingi mia tano.

Akizungumza nasi katibu wa soko hilo, Bakari Hussein amesema utaratibu uliopo kwa sasa baada Serikali ya mkoa kuwahamishia katika soko hilo kuna baadhi yao wameanza kurejea mitaani na kupika chakula katika maeneo yaliyokatazwa na kukiuza kwa bei chini hali inayoleta upinzani kibiashara.

Wamesema kwa siku utaratibu kwa kila mfanyabiashara anatakiwa kulipa shilingi mia tano kupitia control namba maalum hivyo kurejea kwa mitaani kunapoteza mapato ya jiji lakini pia kuwaumiza wengine wanalipa ushuru huo.

Kwa upande wao mama lishe na baba lishe hao wamesema biashara sokoni hapo inabadilika kulingana na siku wakiiomba Serikali ya Mkoa kudhibiti wote walioko mitaani ili kurejesha utulivu wa kibiashara.

Chanzo: EATV
 
mama lishe na wengine mama poa basi kaazi kweli kweli, ila hao ni wanyonge jamani na mtetezi wao ashakufwa pole ssna kwao wajemeni
 
Tumezoea mazingira machafu kwa hivyo kwenye eneo la usafi hatuwezi kula.
 
Naona Kuna shida sana ndani ya Jiji, Hali ya Jiji kuwa kama gulio inarudi Kwa Kasi kubwa!! Nashindwa kuelewa kazi ya uongozi WA mkoa
 
mama lishe na wengine mama poa basi kaazi kweli kweli, ila hao ni wanyonge jamani na mtetezi wao ashakufwa pole ssna kwao wajemeni
Wanyonge?!! Mpk kulipia jero kwa siku nayo shughuli?! Nchi ngumu sana hii
 
Sio kwamba wamekimbia hiyo 500 ya ushuru hapanaaa.
Amini nakwambia kama sehemu kuna biashara hata ushuru ungepangwa sh. 10,000/= wangelipa tuu.
Inshu ni kwamba hakuna biashara pale kwa sasa na huwa ni za msimu.
2019 mimi nilikuwa nalipa sh 700 pale kwa kizimba
 
Back
Top Bottom