Pre GE2025 Mama Maria Nyerere aitaka CCM kusimamia ipasavyo Serikali

Pre GE2025 Mama Maria Nyerere aitaka CCM kusimamia ipasavyo Serikali

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

the guardian 17

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
395
Reaction score
570
Mjane wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, Mama Maria Nyerere, amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuendelea kutimiza wajibu wake wa kuzisimamia Serikali zake zote mbili ili kuhakikisha nchi inaendelea kuwa na uwezo wa kujitegemea, hasa katika kujilisha.

Mama Maria ameyasema hayo alipokutana na Katibu Mkuu wa CCM, Balozi Dk Emmanuel Nchimbi, aliyefika nyumbani kwa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Msasani, jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kumjulia hali, leo Alhamisi, Februari 20, 2025.

“Naomba tu muendelee kusimamia sera ya msingi ya CCM kuhusu kujitegemea… Uhuru wa taifa unakamilika zaidi pale taifa linapojitegemea, hasa katika kujilisha na kuwa na chakula. CCM isiache wajibu wake wa kuzisimamia Serikali zake zote mbili ili nchi yetu iendelee kujitegemea,” amesema Mama Maria.

Screenshot 2025-02-21 122014.png

Source: Mwananchi

Soma pia: - Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom