Mama mkwe ana mwezi hana dalili ya kuondoka, chumba kimoja, nimemmisi mume wangu

Rahabu

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
5,526
Reaction score
3,341
Wana sisi wazima huku najua hakuna fujo sana, na kuna watu makini wa kunisaidia.

Wapenzi,

Nina mdogo wangu ana kama miaka 26, kaolewa na mtu wa Dodoma. Naishi nae karibu kama nyumba 5 kutoka kwangu amepanga chumba kimoja self container.

Sasa kama mwezi mkwewe alikuja kumsalimu.

Na alisema anakaa siku 3. Jamani, hadi leo mume wake analala kwa marafiki zake. Juzi nasikia anaongea na ndugu zake kuwa atarudi hadi pasaka iishe jamani mwezi na siku kadhaa na analala kitandani bila aibu.

Anaogopa kumwambia mumewe atahisi anamchukia mama yake na hivyo anataka jumamosi kuondoka kwenda kwao Morogoro ila mkwe haoneshi hata dalili ya kuondoka; kasema kama haukai sana utanikuta.

Hebu mshaurini mdogo wangu jamani.
 
Wewe kama dada mtu ulimshauri vipi dogo?

Huyo mama nae hana hata aibu,hajiongezi aaagghhr
 
Mmmh........hapo pagumu. Aongee na mumewe watafute nyumba yenye vyumba kama vitatu hivi ili kuweza ku-accomodate wageni kama hao.
 
Aisee pole kwa mdogoo wako,ni pagumu sana hapo lakini hao wawili, yani mke na mume ni swala ambalo lipo ndani ya uwezo wao so inabidi wajadili in a positive way naamini watafkia mahali pazuri tuu

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Wewe kama dada mtu ulimshauri vipi dogo?

Huyo mama nae hana hata aibu,hajiongezi aaagghhr
Chocs mpnz utashaur kwenye ndoa ya m2 mwisho wa cku dada mbaya ila nilimwambia azidishe mapenzi kwa mkwewe mana yawezekana ndo mtihan mkwe anampima kwa kosa dogo asimpe nafasi mkwe ya kumpa sifa mbaya.
 
Last edited by a moderator:
Duh hizo ndo changamoto za ndoa..avumilie tu kaja kwa mwanae kula bata loh si mnajua wamama wakwe wengine?! ! Lakinii......inamana huyo mdogo wako na mumewe hawawezi kutoka hata siku moja kwenda mahali pa faragha wakamalize shida zao huko then wakarudi maisha yakaendelea?? Aaah jamani mbona simple hivyo embu mwambie afanye hivyo kwanza ....
 
Pagumu sana hapo,dah vitu vingine bhana mtu unajishtukia mwenyewe,ina maana huyo maana hata hajishtukii!
 
Mpe pole shosti lakini kama angekua mzazi wake angesikia vibaya? mwambie hata akikaa miezi miwili ni sawa tuu kwani ni sawa na mama yake,kwaupande wangu mimi namchukulia mkwe wangu ni sawa na mzazi wangu ila langu la ndani hatolipata
lakini kwakukaa nyumbani akae hata mwaka as long as ni mkwe na yeye mume anaona sitafuti ushauri wala ukwaju,kama kukidhi haja ya ndoa siamini kama huyo mama anakua ndani 24/7 na hata kama anashinda nyumbani unaweza wewe dadake ukamualika kwako huyo mkwewe yeye na mumewe wala raha kwa raha zao bila kumkera huyo mama au toka nae nenda nae madukani nenda nae Beach, asishindwe nakupika akasingizia Moshi,kuna vitendo vyengine wala havitaki masaa
na vinakuwaje vitamuuu !!! ebu msaidie japo kwa hilo kama ameshikika sana.............
 
Kina mama mkwe mara nyingi wanakuwa hawakubaliki, mara nyingi wanatafutiwa hadi visingizio vya uongo.

Nilichogundua mke akileta wazazi wake hata wakae mwaka mzima sio tatizo lakini mume akitembelewa na mama yake wiki moja tu nongwa zinaanza, vijisababu vingine vya kutunga ataambiwa baba mwenye nyumba ili mradi mama wa watu aondoke. Na kama unavyojua tena katika ndoa nyingi(ingawa sio zote) mwanamke ana nguvu, mama wa watu lazima ataondoka
 
Mmmh........hapo pagumu. Aongee na mumewe watafute nyumba yenye vyumba kama vitatu hivi ili kuweza ku-accomodate wageni kama hao.

Huwez jua wamejipanga vp kiuchumi na wakipanga vitatu sindo ndugu watakuja kuhamia kabisa
na Katavi. Miez kama sita walikuwepo mashemej 2 walikua wanakula pale na kushinda jion wanaenda kulala kwa marafiki walikaa karibu miez3
 
Last edited by a moderator:
hivi huyo mamamkwe nae hajisikii aibu hata kidogo alitakiwa asome mazingira kama yanaruhusu ugeni au lah
 
Wawe wanaenda kulala guest house ikifika asubuhi wanarudi nyumbani pale wanapohitajiana.
 
Thubutu mkavu kama kipande cha papa
 
huyo ni mzazi wako huna budi kumvumilia,mwambie ajibebe na mume wake wakamalizane hotelini then maisha yanaenda bila kukwaruzana,asiumie maana ndo ndoa zilivyo,afurahi na ajiachie kwa raha zake.Maisha yenyewe mafupi haya ebooo
 
Mmm ila mapenz ya nyumbani kwako ni kwako2
 
Unafikiri kila mtu ana ufahamu na utashi wa kusoma mazingira?
a.rahabu Kuanzia huyo mwanaume na mama yake wamekosa huo utashi. Mwanaume ndio alipaswa kuliona hilo mapema hata kabla hajaja na awe amepanga ramani nzima.

We unafikiri na huyo Mume huko aliko hawajamchoka? Ukweli nae wamemchoka. Mume anapaswa atumie hekima kidogo tu. Aende akanunue vizawadi vya pasaka haswa vyakula (Mafuta, mchele etc) na hela kidogo ampelekee mama yake amwambie akale na familia kusheherekea pasaka nyumbani. mchezo umeisha. Ila kwa wabongo tulivyowanafiki, mdada akijidai kwenda kumwambia Mumewe ajue imekula kwake maana inaonekana na mumewe hajitambui vizuri kupembua mchele na mpunga.

Kwa tamaduni za kikwetu nyumbani Mkwe au hata mama ajue una kachumba kamoja, Hata Umhonge na hela Juu hatakaa afikie kwako kamwe.

hivi huyo mamamkwe nae hajisikii aibu hata kidogo alitakiwa asome mazingira kama yanaruhusu ugeni au lah
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…