Siyo kosa la mama mkwe. Ni kosa la hao wanandoa. Hivi mwanaume mzima unaoa alafu unaenda kujibanza kwenye chumba kimoja? Hakuna cha binti wa kazi wala dharura ikitokea akaja mgeni muhimu hakuna pa kumweka? Hainiingii akilini. Namsifu rafiki yangu fulani alikuwa amepanga chumba kimoja, alipokaribia kuoa alifanya kila aliwezalo kuondoka hapo, alinifuata kuomba ushauri, nikamwambia aamue either akapange sehemu nyingine apate vyumba viwili au kama ana ubavu afanye finishing ya nyumba yake haraka, kweli jamaa akajilipua na mkopo benki. Mara baada ya kuoa ndani ya mwezi mmoja alihamia kwake. Huo ndo uanaume, siyo kuvaa suruali tuu.