Kuna kosa huwa tunafanya ktk majibu tunayotuma ktk mitandao ya jamii.Aisee miezi miwili umeshindwa kumpachika mke wako mimba?????
Tunajibu mambo ya msingi kwa majibu mepesi na ya ajabu ajabu kama vile kila kitu ni mzaha. Kibaya zaidi, jamii inasoma kila tunachoandika. Pengine waweza kuona ni sifa, japo mimi naona ni ''sifa za kijinga'' (Mniwie radhi kwa maneno hayo pengine yakawakwaza baadhi)
Ni vyema ukampa mtu ushauri wenye tija ktk jamii nzima ya JF maana sote tunasoma na mpaka mtu aamue kutuma thread kama hii humu, ni jambo limembana. Kwa vile hatulingani kwenye kufikiri, basi tupeane majibu yenye tija. Unafikiri mwanamke anajazwa mimba kama ndoo ya maji bombani hata uone miezi 2 kuwa muda mrefu sana????
Chonde chonde ndugu zanguni.
Sent using Jamii Forums mobile app