Mama mkwe mtarajiwa hataki binti yake aolewe na Kabila langu

Mama mkwe mtarajiwa hataki binti yake aolewe na Kabila langu

As long as ushatia mimba, wewe tulia mkuu. Acha waparuane wenyewe huko.

Mwafrika ni mbaguzi kuliko races nyingine nyingi, japo mbele za watu anapenda kuplay victim role.
 
Shida ya hili kabila huwa ni ukatili, hata mim mwanamke mkurya siwez kuoa, kwanza ukiwa na mke mkurya, mkipgana ndani halaf ugomvi ukaisha, kaa chonjo muda wote, ukipenda mambo ya kulala lala hawachelewag kukudunga kisu, au kukupasua na shoka! Hawa watu hasira zao haziishagi, hata mkisolve ugomvi, yeye anasolve usoni tu ila moyon kakutunza!
Hawa watu wana hasira, nilishadate mkurya kuna siku tulizinguana sana lakin baadae tukayamaliza na furaha ikarejea, zikapita siku kadhaa nipo nimekaa mchana kweupe yeye akiwa anaandaa chakula ghafla nashangaa mtu huyo na kisu kaninyooshea ananitishia, nikamuwahi mkono nikamnyang'anya akaanza kulia kwa hasira na kueleza bado ana hasira yale yaliyotokea hayajaisha. Nilibaki nashangaa ni hasira gani hizo mtu anazifuga na tayari tulishayamaliza.
Sasa fikiria ingekuwa nimelala si angenimalizia mbali kabisa.
 
Hawa watu wana hasira, nilishadate mkurya kuna siku tulizinguana sana lakin baadae tukayamaliza na furaha ikarejea, zikapita siku kadhaa nipo nimekaa mchana kweupe yeye akiwa anaandaa chakula ghafla nashangaa mtu huyo na kisu kaninyooshea ananitishia, nikamuwahi mkono nikamnyang'anya akaanza kulia kwa hasira na kueleza bado ana hasira yale yaliyotokea hayajaisha. Nilibaki nashangaa ni hasira gani hizo mtu anazifuga na tayari tulishayamaliza.
Sasa fikiria ingekuwa nimelala si angenimalizia mbali kabisa.
Ulikuwa umeisha

Sent from my SM-N975U using JamiiForums mobile app
 
Mimi ni Mwanaume 28yrs mkurya nilivyofika Dar nilikutana n'a bint mmoja nikamtongoza akakubali.

Huyu binti (21yrs) ni mgeni Dar from mkoa X nyanda za juu kusini anaishi kwa shangazi yake Dar

Hakuwahi kuniuliza Kabila nahisi alijua mimi ni from dar /pwan

kwasababu Mimi Sina ukabila sikuzingatia sana kwanini haniulizi Kabila langu.

Tuna mahusiano ya miez 11 kwa bahati nzuri alipata ujauzito kwenye uchumba manake sasa in animimba ya miez5 .

Shangazi yake aligundua ana mimbaa ikiwa n'a miez3 wakambana akanitaja.

Kwa sababu nilikua n'a malengo nae nikamwambia relax ntakuja kujitambulisha nitakuoa akakubali.

December nikarudi home kuset Mipango ya washenga na mahari.

December mwishon akanipigia simu anasema mama yake kamuuliza mwenye mimbaa/muoaji ni Kabila gani.

Nikacheka nikamuuliza umejibuje akasema amemwambia mimi ni Kabila X tofauti na mkurya.

Akadakia ghafila akasema ety mama amemwambia huyo Mwanaume /Mimi kama angekua mkurya asingekubalika ukweni

Straight nikajib Mimi ni mkurya pure Ila nmekulia dodoma wazaz mdugu karibu wote wako dodoma

nikachukulia ni masihara Kumbe ni serious nikamwambia mwambie tu ukwelii.

Akampigia simu akaniunganisha akamwambia ukweli mama akanza kufoka kumbe yupo serious anamwambia mara unatamaa, umeokoteza wAnaume Huko huwajui Mimi simtaki kama utamkubal ni Wewe mixer maneno kibao.

Nikamchunguza Bint akaniambia Kuna kaka yao aliwahi pata majanga huko mara miaka ya nyuma may be maana wanakisas.na makasiriko.

Binti ananipenda haswa Mimi pia nampenda

Binti kaniambia Yuko tayari kwa lolote Bora nimuoe hâta kama wakimtemga .

Kama Kuna Kuna namna ya kusolve hili ratizo naomba maelekezo/ushauri

Mahusiano ya kupewa ruhusa kama watoto wadogo ni yakijinga na kipuuzi.

Tafuta mwingine
 
Usitishwe na maneno mkuu, kikubwa mmekubaliani wewe na huyo mchumba wako. Ndoa ni ya wawili, watatu hana nafasi.

Na kama ni baraka, Mungu yupo atakusimamia wewe na mkeo mtarajiwa.
 
Kuna mawili kwanza anajua wakurya wanapiga ila pia atakuwa anajua tabia za Binti yake na akiunganisha matukio anaona utamvunja vunja mifupa.
 
Back
Top Bottom