Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Mama mkwe na mwana wote wanapiga mbonji kwangu

Usioe mwanamke mwenye elements za kiswahili. Nyumbani kwako kutageuka kambi ya wakimbizi, hawanaga haya hao.
Hapa umeongea hii kauli nimeshaisikia kwa watu wasiopungua watano. Wanasisitiza kuwa kuna wanawake wanatabia za kiswahili, wao wanajionea kila kitu sawa.....
 
Hii haijalishi ni ndugu wa nani wanazungumziwa hapa, tatizo ni USWAHILI. Unaongea kwa uchungu kwa kuwa hata sasa unaishi kwa shemeji yako eeh? Toka hapo mama nenda kwako, utaharibu ndoa ya dadaako. Tujifunze pia kuzaa kwa mpango
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ukiwa unadate na binti wa kukuletea utitiri wa ndugu utamjua tu mwanzoni. Unamtoa out au mko kwenye maongezi yenu mara simu inalia anaongea anaanza kukutambulisha na kukupa simu sijui msalimie anti/uncle/mama/Dada/kaka/ mdogo wangu, n.k. ukioona hivyo ni dalili tosha huyo manzi chaka!
Hii ni kweli kabisa
 
mr.London, Kwa mama mkwe wa hivyo hamtamaliza hata miaka miwili mbele lazima wewe na mkeo muachane!
Tofauti na hapo wakupige limbwata uwe bwege then familia nzima wahamie hapo halafu wakubandike na kajina ka utani "kijeba" ni full kukusema kutwa nzima ukiwa job na kukuigiza unavyotembea na kuongea[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Watu wa ukumbi huu, habari zenu.

Nimeoa na sasa nina watoto 2 alhamdullah, nampenda sana mke wangu lakini kuna jambo hili linaendelea kila uchao nahisi moyoni nimeanza kulichukia chukia.

Kuna muda mamamkwe amekuja kumsaidia ulezi wife wakati wa kujifungua lakini akapitiliza ule muda nilioambiwa na wife kama angekaa, sasa akawa anakaa kama ndio mahali pa kuishi. Yeye ni age kidogo, mama mtu mzima, hana mume.

Kuna kipindi huyu mama anaumwaumwa, mara ikaja ni kuhusu haya mambo yaliyoingia; sijui kapewa jini, mara shetani tafrani nyumbani mpaka sasa amesafirishwa mji wa pili kwa matibabu zaidi lakini nahisi akimaliza matibabu kama aturidi hapa kwangu.

Suala lingine naona shemeji yangu mtoto wa kiume shababi naye amekuja. Siku hiyo wife akaniambia leo shemeji yako, yaani mdogo wake, atalala hapa nikasema safi nikamtolea kitanda na godoro ili achape usingizi kwa siku ile, lakini naona siku ya pili kaendelea mpaka imefika kama wiki akasafiri kidogo kaenda kukaa kama siku 4 karudi yupo tunaendelea naye anachapa usingizi kama kawaida.

Nilijaribu kumuuliza wife ananimbia anafuatilia kitambulisho cha Taifa. Sasa mimi najiuliza, ivi unaweza kuacha shughuli zako siku zote kwa kitambulisho tu? Kuna siku akasema ile namba tayari ashapewa lakini mzee yupo ameganda tu na sasa pale home majukukumu yanaongezeka.

Naomba fatwa watu wa hapa, vipi niendelee kuvumilia maana hata uhuru pale nyumbani naona umebanwa kidogo.
Mama mkwe wako ni sawa na mama yako mzazi (kumbuka ni mzazi wa mkeo)

Nakushauri kitu kimoja, kama angelikuja mama yako mzazi ungemfukuza, fukuza mama mkwe (kifupi mtende kama ambavyo ungemtenda mama yako mzazi.)

Kuhusu shemeji, hapo sina neno na wewe ila tu tumia njia nzuri ambayo si ya kumdhalilisha. Unaweza kumshauri kama mdogo wako tu.
 
We jamaa hupendi ndugu....yaan nikajua bhc wamekaa kwa muda kweli kumbe miezi tu...
Ulafi tu unakusumbua
 
Pole sana ndugu yangu:-
Sijui mlianza kuishi vipi na shemeji yetu, lakini baadhi yetu Kuna mambo tuliyawekea misingi kabla ya kuanza kuishi pamoja kama mke na mume
1. Wageni wanakaribishwa kwa kipindi maalumu na wataishi kwa muda maalumu wakiwa na sababu maalumu pia.
2. Ugeni utategemea natasi iliyopo. Masuala ya kulazana koridoni au sebuleni tuliyapiga marufuku. Mgeni anaelezwa wazi kuwa hakuna nafasi.
Baadhi ya familia unaweza kutembelewa na shemeji yako akiwa na mumewe pamoja na watoto wao wanne, Sasa unajiuliza utawaweka wapi?!
3. Kaa chini na mkeo na uzungumze naye kwa utarabitu kabisa kuwa hiyo hali haikufurahishi. Ni vyema kusema ukweli kuliko kuwa mnafiki moyoni.
4. Mkeo atachukia lakini mweke wazi kuwa inawezekana pia huna uwezo wa kumudu hizo gharama za maisha.
5. Jiandae kununiwa kwa muda na shemeji baada ya kumueleza huo ukweli kwa sababu yeye atadhani tatizo ni roho mbaya yako wakati wewe umeangalia mustakabali wa familia yako.

Pole sana.
 
Chukua likizo ya ghafla uondoke ww mke na watoto wako 2. Wataondoka wenyewe
si utaulizwa unawaachaje achaje... dawa wanunulie unga kilo 10 dagaa kilo moja na maharage kilo 3 , Tokomea wiki 2-3 hivi
 
Huyo ma’mkwe na mwae lao 1 tu. Jitie unafiki wa kutomwambia ukweli huku unaumia mwambie achague yeye/binti’ye yupi abaki!
mwangushie vipigo mke daily kwa wiki moja mfululizo, lewa kila siku anzisha fujo na matusi... kama mamamkwe +shemejiyo wakiweza kustahamili hayo jua Taraka ndo mwokozi pekee au Lete nyumba ndogo nayo iishi apo
 
mr.London, Kwa mama mkwe wa hivyo hamtamaliza hata miaka miwili mbele lazima wewe na mkeo muachane!
Tofauti na hapo wakupige limbwata uwe bwege then familia nzima wahamie hapo halafu wakubandike na kajina ka utani "kijeba" ni full kukusema kutwa nzima ukiwa job na kukuigiza unavyotembea na kuongea[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
We jamaa nimecheka eti full kukucheka
 
mr.London, Kwa mama mkwe wa hivyo hamtamaliza hata miaka miwili mbele lazima wewe na mkeo muachane!
Tofauti na hapo wakupige limbwata uwe bwege then familia nzima wahamie hapo halafu wakubandike na kajina ka utani "kijeba" ni full kukusema kutwa nzima ukiwa job na kukuigiza unavyotembea na kuongea[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
huo upuuzi unaulea tuu....haya mambo ya kusema jamii itanionaje mie sina kabisaaaa....hali ya kiuchumi ni tete sana......hukuoa ukoo...furumusha blaza.....msaada huko huko kijijini utakuja.....wacha waseme wapasuke.....nyumba yangu, nke yangu maisha yangu......hapo wewe anza kurudi late mtungi wa kufa....kimya wala usimsemeshe ntu....jua tuu ndoa yako iko hsptl........daktari ni wewe....tibu au tibua....
Wamakonde bhana!!!

Am kidding[emoji3][emoji3]
 
Pole aisee. Ndio maana wenye pesa wanakua na nyumba ya wageni. Ndani kuna kila kitu wewe kazi yako kununua chakula ujipikie sio kuharibu budget za watu [emoji2][emoji2]
 
No retreat no surrender, Wanakuja tu dar familia ngapi zinaishi chumba na sebule na ndugu karibia watu8 humohumo na maisha yanaenda?!

Tuache utani wangekua ndugu wake yeye mwanaume angelalamika?!
Ndugu zake angewaambia tu direct hana haja kufungulia uzi. Shida inapokuja ataanzaje kuwaambia ndugu wa mwenzi wake?
 
Back
Top Bottom