Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Ni mama yangu wa ubatizo,hence in my eyes she can do no WRONG.
nakuelewa kaka ukizingatia wewe mwenyewe umepelekwa huko London kwa hela hizohizo za ufisadi lazima umteteeeee but get prepared coz the cheques will stop coming your way.............uuuuh sorry ....stopped alrealdy...................utashinda na njaaa kaka tukuleteeeee dagaaaa wa ukerewe na unga wa donaaaaaaaaaaaaa?
 
Mwenyewe Agoma Kuzungumza!

Rais wa Bunge la Afrika, Mama Getrude Mongella, anatuhumiwa kutenda makosa ya kukosa uaminifu, Wizi na utoaji ajira kinyume na taratibu za kazi yake:-

1. WIZI:- anatuhumiwa kutafuna Dola za US, 138,000 ambazo ni sawa na shillingi 180Millioni za Tanzania.

2. UAJIRI:- anatuhumiwa kuajiri ndugu zake kinyume na sheria za kazi yake, akiwemo mkwe wake, yaani mke wa mtoto wake.

Katika kikao cha AU kilichopita nchini Ghana, nchi za Afrika zilimuamuru mama huyo kurudisha hela hizo mara moja huku uchunguzi ukiwa unaendelea, kikao hicho pia kilihudhuriwa na Rais Kikwete.

Mama Mongella, anatuhumiwa kujilipa US/Dola 800, kwa siku akilifanyia kazi bunge hilo la Afrika, na huku akiwalipa US/Dola 400 kwa siku ndugu zake aliowaajiri huko AU, wakati pia akilipwa na bunge la Tanzania kwa kazi hiyo hiyo. Mkwe wake mama huyu tayari ameshaachishwa kazi na bunge hilo na wengine wako njiani kurudishwa tayari Tanzania.

Katibu wa Bunge la Tanzania, ndugu Foka, alithibitisha kupata habari hizo za tuhuma dhidi ya Mama Mongella, na amekiri kwamba ni kweli Bunge letu la Tanzania limekuwa likimlipa mama huyo fedha zote anazostahili akiwa analifanyia kazi bunge la Afrika, kwa mujibu wa makubaliano na bunge hilo la Afrika, ambalo liliwaomba mwanzoni wakati anaanza kuwa liwe linamlipa ili asilipwe na bunge hilo la AU.

Taarifa za uchunguzi tayari zimefanyika na SADC, ikishirikiana na kampuni ya KP GM ya Kenya, ambazo izmeshauri mama huyo kufukuzwa kazi na kurudisha mapesa hayo kwa AU, mara moja. Mbunge mmoja wa bunge hilo la AU, Ndugu Wanyancha,(Serengeti-CCM) amekubali kuwa kweli Mama anakabiliwa nashutuma nzito sana ambazo zitatukosesha urais huo kwa muda mrefu sana ujao, juhudi zote za kuzungumza naye kuhusu hiii sualazimakwama kutokana na kukataa kwake, mama huyo.



Source: Mwana-Halisi.
Kwa kweli ni vema hata Serikali ya Tanzania ikamchunguza Mama huyu kwani hata Tanzania kuna ndugu na Wakwe zake amewapa kazi katika taasisi za Serikali na NGOs na wengine walipwa mishahara na sehemu mbili na zaidi wakati Watanzania wengine hawana ajira.Pia sheria ichukue mkondo wake kwa Mama huyu kwa kuiaibisha Tanzania.
 
nakuelewa kaka ukizingatia wewe mwenyewe umepelekwa huko London kwa hela hizohizo za ufisadi lazima umteteeeee but get prepared coz the cheques will stop coming your way.............uuuuh sorry ....stopped alrealdy...................utashinda na njaaa kaka tukuleteeeee dagaaaa wa ukerewe na unga wa donaaaaaaaaaaaaa?
In line with the constitution of the united states,i plead the fifth amendment-the right to remain SILENT
 
In line with the constitution of the united states,i plead the fifth amendment-the right to remain SILENT
Yeah, but the main audiance of this blog is wabongo.This may not help you very much if you profiteered on dirty stolen money!
 
Huyu mama ! amechezea heshima yake, ukizingatia kwamba ni kati ya wanachama waanzilishi wa TANU na alibahatika kushika madaraka tofauti. Hii ni halisi ya viongozi wetu, uwizi mtupu !!!! uongo mtupu ! hata umri hawauonei aibu. Hii inadhihirisha uzoefu wao katika fani ya kuiba mali ya umma........ kui kui kuiiiiiii
 
ka slogan huko AU pia wanakajua! Origin ni mwenyewe Kwame Nkrumah!
JK anapigwa pande zote, na kama hatoanza kuwa mahiri, yote yatamtokea puani!
 
lakini hii habari ya Mongella mbona ya long- yaani kitambo nilishawahi kuisikia, mategemeo yangu ni kujua matokea na siyo stori zilezile. au mkuu kanukuu mwanahalisi ya zamani?
 
Na Aristariko Konga

BALOZI Getrude Mongella, Rais wa kwanza wa Bunge la Afrika (PAP) amelazimika kujiuzulu kutokana na tuhuma za matumizi mabaya ya fedha na ajira za upendeleo katika ofisi hiyo.

Hatua ya kulazimishwa kuachia ngazi imekuja baada ya mlolongo wa malalamiko kutoka kwa wabunge wa PAP kutokuridhika na mwenendo wa matumizi ya fedha na uendeshaji wa ofisi hizo.


Nafasi yake imechukuliwa na Dk. Idriss Ndele Moussa, Mbunge kutoka Chad, katika uchaguzi uliofanywa na bunge hilo 28 Mei mwaka huu. PAP ina makao makuu katika mji wa Midrand, nchini Afrika Kusini.

Dk. Ndele aliibuka mshindi baada ya kuwashinda wagombea wenzake wawili; Lassane Sawadogo, mbunge kutoka Burkina Faso na Mustafa El Gendy, kutoka Misri.

Dk. Ndele aliapishwa na Dk. Mongella kuchukua wadhifa huo mpya, akiwa na kazi ya kufanya mabadiliko makubwa ya uongozi na utendaji wa PAP, kutokana na maagizo ya wabunge ya 19 Mei, mwaka huu huko Midrand.


Bunge la Afrika pia lilichagua makamu wanne wa rais ambao ni Bethel Amadi (Nigeria), anayewakilisha Kanda ya Afrika Magharibi na Mary Mugyenyi (Uganda) anayewakilisha Afrika Mashariki.

Wengine ni Laroussi Hammi (Algeria) anayewakilisha kanda ya Kaskazini, na Joram Gumbo (Zimbabwe) anayewakilisha kanda ya Kusini mwa Afrika.

Mabadiliko yanatokana na kuwapo tuhuma dhidi ya Mongella kuwa chini ya uongozi wake, ajira zilipatikana kwa misingi ya upendeleo na bila kufuata taratibu za ajira wala sifa za watumishi.

Habari zinasema kuwa katika siku za karibuni, kabla ya mabadiliko hayo, Mongella alijaribu kungangania ili aendelee na wadhifa huo, lakini alishinikizwa kuachia ngazi, jambo ambalo lilikamilika 28 Mei mwaka huu.

Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Dk. Thomas Kashilila, alipoulizwa juzi Jumatatu, alikiri kuwa na taarifa za Mongella kuacha wadhifa huo, ingawa ofisi yake haikuwa na taarifa rasmi kutoka PAP.

Tumepata taarifa kupitia njia nyingine, lakini hatuna taarifa rasmi kuwa kaacha wadhifa huo, alisema Dk. Kashilila.

Mwenendo wa Mongella uliishakuwa hoja hadi wakuu wa nchi za Afrika kuunda kamati maalum ya kufanya uchunguzi wa usimamizi na uendeshaji wa PAP.

Taarifa zinasema bunge lilijadili kwa kina taarifa ya kamati hiyo na kujiridhisha kuwa kulikuwa na matumizi mabaya ya fedha.

Katika hatua ambayo haikutarajiwa, inaelezwa kuwa serikali ya Tanzania imekubali kubeba mzigo wa kulipa fedha zote ambazo Mongella alituhumiwa kuzitumia vibaya.

Taarifa zinasema awali, hata baada ya serikali ya Tanzania kuchukua mzigo huo, Mongella alishauriwa ajiuzulu ili kulinda heshima ya Tanzania, lakini aligoma kufanya hivyo.

Wabunge wa Bunge walilalamika kwa viongozi wakuu wa nchi za Afrika juu ya uongozi wake kwa ujumla, ambao wanadai haukuwa na dira wala tija.

Kuna madai pia kwamba alingangania kubaki katika nyumba ya Bunge na alipolazimishwa kuondoka akaamua kuhama na fenicha zote za ndani akidai ni zake, jambo ambalo si la kweli, alisema mbunge mmoja wa Bunge la Afrika kutoka Tanzania ambaye hakupenda kutajwa jina.

Aidha, uongozi wa Mongella umelalamikiwa kwa kushindwa kufanya jambo la maana wakati uliendelea kugharimu rasilimali za nchi za Afrika.

Mjadala wote wa kumuondoa Mongella ulikuwa unaripotiwa moja kwa moja kwenye vyombo vya habari vya Afrika Kusini na Namibia. Kuna wakati Mongella alilazimika kukatisha kikao cha Bunge hilo na kufanya mazungumzo ya faragha na makamu wake wawili.

Baada ya kikao hicho cha siri, Mongella aliamuru waandishi wa habari waliokuwa wakifuatilia kikao waondoke, jambo ambalo lilifanyika.

Naye mbunge mpya wa Tanzania katika PAP, John Cheyo amesema Mongella atakumbukwa kwa kuwa rais wa kwanza wa PAP.

Ni MwanaHALISI iliyowahi kuandika katika toleo Na. 73 la Novemba 28 hadi 4 Desemba 2008, kwamba Mongella alikuwa anatuhumiwa kutenda makosa ya kukosa uaminifu, wizi na utoaji ajira kinyume cha taratibu.

Kuhusu wizi, Mongella anatuhumiwa kutafuna dola za Kimarekani 138,000 sawa na Sh. 180 milioni za Tanzania, mali ya PAP.

Katika tuhuma za utoaji ajira, Mongella anatuhumiwa kuajiri jamaa zake ndani ya Sekretarieti ya Bunge hilo, kinyume cha taratibu. Tayari Bunge limeagiza kufuta ajira zilizofanywa na Mongella.


Omugasi
Re: Mama Mongella - Aghushi na Kutafuna Mamillioni Ya Pesa!

Lakini hii habari ya Mongella mbona ya long- yaani kitambo nilishawahi kuisikia, mategemeo yangu ni kujua matokea na siyo stori zilezile. au mkuu kanukuu mwanahalisi ya zamani?
 
Katika hatua ambayo haikutarajiwa, inaelezwa kuwa serikali ya Tanzania imekubali kubeba mzigo wa kulipa fedha zote ambazo Mongella alituhumiwa kuzitumia vibaya.

  1. Kwa msingi gani serikali imechukua huu mzigo wa mama Mongela, mtuhumiwa wa wizi?
  2. Je Mama Mongela atazilipa vipi hizo pesa ambazo serikali imeamua kumlipia?
  3. Nijuavyo mimi ni kuwa ana mali TZ ikiwa ni pamoja na ile nyumba yake pale Makongo, kwa nini visifidie wizi wake?
  4. Je, mashtaka gani yanamsubiri mama Mongela au atapewa ukuu wa Mkoa akapumzike?
Kwa kweli nchi imeharibika. Unapokuta Mama Mongela ameamua naye kuwa mwizi, Mzee Kingunge kuwa fisadi n.k., basi ujue hakuna aliyebaki safi kwenye timu JK.
 
Anagoma nini?lazima alazimishwe azungumze kwani huo ni ufisadi na usanii wa hali ya juu,tunataka azungumze kwa sababu tayari serikali kupitia hela za walala hoi wa tanzania imeamua kuzirudisha.Huyo mama hafai kabisa na hao ndio wanajifanya waumini wa Mwl J.K.Nyerere ubinafsi kila sehemu jamani tutamwamini nani?
 
Mama yangu weee, si jui tumwamini nani ,ufisadi kila kona ,huyu mama ni mama EPA,tuhuma kila mahali kwa hawa tunawowaita viongozi kuanzia akina Kingunge,Mkapa,Lowasa,Warioba loo mbona mkono umechoka kuandika orodha ni ndefuuu sana,inatia kichefuchefu ama kweli naamini rupia ilimsaliti hata Yesu,
Hii nchi inaenda kwenye zile zama za.......
 
Naomba msaada kwa kuwa sijaelewa.

Mbona original post ni ya mwaka 2007, je kua habari mpya au ni zilezile. tupeni ili tuweze kuchangia. Thadhari! Kama ni ile ya mwaka 2007 basi tutakuwa tunaigeuza hii forum sehemu ya fitina.
 
Naomba msaada kwa kuwa sijaelewa.

Mbona original post ni ya mwaka 2007, je kua habari mpya au ni zilezile. tupeni ili tuweze kuchangia. Thadhari! Kama ni ile ya mwaka 2007 basi tutakuwa tunaigeuza hii forum sehemu ya fitina.

Hii thread kuna mtu alianzisha mwaka 2007. Sasa member mwingine akatoa data nyingine kuhusu huyu huyu mama so wakaamua kuziunganisha mkuu.
 
sasa huyu mama mbona ametufedhehesha sana wajameni..haya bana...kweli alielelewa na ccm hata aweje ataiba tu...huyu mama ni uzao wa ccm..na ni mwanachama wa ccm...kwahiyo hatushangazwi tunaojua wizi unaofanywa na ccm
 
...halafu alikuwa anautaka urais wa nchi!

Sasa pale Ikulu sijui ndio ingekuwaje kama angeupata,i'm sure yule mtoto wake ambaye ni DC Kigoma huko labda angempa ubosi wa PCB!

Jamani,hao ndio viongozi wetu...always drooling where theres $$$

Angekua Waziri Mkuu
 
Mnataka wakale wapi? polisi? acheni kununuliwa wakati wa kupiga kura ndo mtapata viongozi safi.

Atatumia hizo hela kununua kura tena!
 
Back
Top Bottom