JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 685
- 1,124
Tafiti zinaonesha kuwa virusi vya Korona haviambukizwi kupitia njia ya kunyonyesha
Hivyo mama aliyethibitika au kuhisiwa kuwa na Virusi vya Korona anaweza kuendelea kunyonyesha mtoto wake isipokuwa atazingatia yafuatayo:-
Kuosha mikono mara kwa mara na sabuni na maji tiririka au kwa kutumia Sanitizer haswa kabla ya kumgusa mtoto
Kuvaa barakoa ya kitabibu wakati wowote anapomshika mtoto, pamoja na wakati wa kunyonyesha
Kuziba mdomo na pua kwa kutumia sehemu ya ndani ya kiwiko cha mkono wakati wa kukohoa au kupiga chafya
Mara kwa mara kusafi sehemu ambazo mama amegusa
Upvote
0